Kubezwa kwangu kulinipunguzia presha nikawa mshindi vipindi vyote

Kuna watu ni wadogo sana humu aisee, hivi humu mkubwa Mimi tu au
Mwaka niliograduate University ,ndo dogo anamaliza la7🤣🤣sisomi Tena nyuzi zake,ndo anabalehe,hapo aliko shawaha bado zinanuka ule uchangah

Kumbe kalisoma diploma,manake kamejisifu kalisoma chuo,kumbe chuo Cha kata mamaeeh 🤧🤧🤧
Nakaweka ignore list asap,sitaki kusoma story za teeneger,it's rubbish.
 
Duuuuh shahawa zinanuka au zinanukia?
 
Mitihani ya taifa ya msingi hufanyika siku za Jumatano na Alhamisi. Wewe ulifanyaje Jumatatu?

Au mimi ndo sielewi majina ya siku? Hapo tu nimeishiwa hamu ya kusoma.
 
Tuendeleee................

Nilirudi home ilikuwa shangwe sana, bro angu alokuwa anajiandaa na kujiunga saint kayumba alifurahi pia japo alikuwa anaumia kwasbb alitamani pia kusoma skul ya private.

Nilianza form one, yule bro mtoto wa babamdogo alikuwa anakaa mtaani japo skuli ile ilikuwa ni wewe tu kuamua ukae bweni au utokee kitaa.
Baba aliamuanikae mtaani na yule bro katika room moja ili kusev gharama za bweni.

Nilikubali na maisha yakaanza. Kumbe yule bro alikuwa anavuta ganja, pombe anapiga na alikuwa mtoro sana skuli yani kifupi alikuwa muhuni.
Miez ya kwanza nilikuwa mwanafunzi nzuri tu, nawahi skul nashiriki usafi yani nilikuwa po kabisa.
Mambo yalianza kuharibika kwenye mwez wa 3 mwishoni. Nilianza kumfata sana yule bro na wenzake, bro alikuwa na wenzake wavuta bangi na wanywa pombe .
Huyu bro kichwani alikuwa njema alikuwa anajiweza darasani ukiachana na ujinga wake, japo hakuwa anaongoza class nafikiri kilichomuathiri ni ulevi wake uhuni.

Nilipojiunga rasmi na hili kundi la bro nilishuka kimasomo kwa kiasi ya 4G. Nilianza Kuban suruali zangu zikawa modo sana, nilianza kugomea na kuwakimbia walikuwa hadharani, nilianza kuruka uzio wa skul na kutokomea geto muda wa masomo.

Kuna siku tulikuwa hatuna kitu geto yani vyakula vimekata, ilikuwa ni j4 jioni tukakumbuka j5 ni siku ya nyama skul n Huwa inaandaliwa jioni then asubuhi inakatwakatwa na kuanza kupokea.

Siku bro na wenzake walipanga twende skul usiku tukaiibie ile nyama ili tuje tuliishi nayo magetoni.
Tulikubaliana tukaenda skul, tuliruka fensi tukawatafuta tukaingia ndani then tukaenda mbali na jiko kama 1.5km tukachoma moto ili walinzi wote waende kule sisi tupate nafas ya kuioiga ile nyama.

Tulifanikisha na walinzi kweli walikumbilia kule kuzima moto tukachukua nyama yote ilikuwa ni paja kubwa la ng'ombe.
Kesho yake mchana skul palipikwa maharage badala ya nyama kama ratiba ulivokuwa inasema na walitangaza nyama imeibiwa katika mazingira ya uzembe wa walinzi. Wanafunzi walisonya sana na matusi juu.

Maisha yalisonga na skul ile wastani wa mwsho wa mwaka ili upande kidato ulikuwa ni 50 kwahyo nilikuwa najua kabisa mimi kwenda form2 nisingetoboa.
Mpka mwez wa tisa bado nilikuwa mwanafunzi mtukutu sana sana.

Mwez wa 9 katikat tulikuwa tunatakiwa kulipa kod na pesa ya kod alikuwa anapewa bro, bro alipewa Ile pesa lakini aliitumika katika vilevi vyake na washkaji kwasabb mimi nilikuwa mhuni ila sikuwahi kutumia kilev chchte mpka hii leo.

Nilishangaa bro kutoweka ghafla pale magetoni akawa anaishi mtaa mwingine mbali kabisa na tulipokuwa tunakaa. Nilipokuwa nikimwambia kuhusu kod alikuwa ananizungusha tu hakutoa majibu ya kueleweka. Nikiwapigia cm home wanasema nimtafute bro ashapewa pesa ya kod.

Nakumbuka siku hiyo saa tano usiku, msimamizi wa vile vyumba alikuja kudai kodi nikishanga kwanini aliamua kuja usiku. Lakini nafikiri aliamua kuja usiku kwasababu alijua kabisa ni lazima angetukuta. Jamaa nakumbuka jina lake ni Hamad.

Hamad alikuja kafyum sana akanambia nimpe pesa la sivyo nihamie usiku uleule. Majirani walimsihi asifanye vile lakini aligoma, ilikuwa ishafika saa6 kasoro jamaa alianza kunitolea vitu nje skuamini chumba mpka kikabak kitupu akapiga kufuri lake akasepa.

Nashukuru kuna bro alikuwa pia anasoma skul hiyo hiyo huyu alikuwa mbele yangu madarasa kama ma3 hvi huyu bro anaitwa Daniel. Bro Daniel alinipa hifadhi na akanambia nisihame mpka tutakapo maliza ule mwaka wa masomo ambapo yeye alikuwa anamalizia form4 mda huo kimi nipo form1.

See you..........
 
Mitihani ya taifa ya msingi hufanyika siku za Jumatano na Alhamisi. Wewe ulifanyaje Jumatatu?

Au mimi ndo sielewi majina ya siku? Hapo tu nimeishiwa hamu ya kusoma.
Nimekumbuka mkuu ni j5 na alhamis, ni miaka mingi and kwa experience ya olevel mpka chuo mitihani mingi huanza j3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…