Uzi umeibua hoja mchanganyiko, zenye hisia, ila ni muhimu kufahamu kuwa Kuna Sheria zinasimamia mambo ya utoaji wa adhabu, Kuna mdau huko juu alishazigusia, Sheria ya Kanuni za Adhabu (Penal Code), Sheria ya Mtoto (Law of the Child Act) na zingine..
Pamoja na hisia zote, tunapaswa kucheza humo kwenye Sheria,
Adhabu haikatazwi popote pale, ila iwe inawiana na uwezo wa mtoto kuhimili, na pia isitoke nje ya lengo la adhabu, ambalo ni...kurekebisha tabia.
Kama adhabu Iko nje ya uwezo wa kuhimili, hayo ni mateso, ambayo humletea madhara muhanga, ikiwemo ya kimwili na kisaikolojia, (unatibu tatizo A unafungua matatizo B na C ambayo hayatatibiwa) wapo waliopoteza maisha kutokana na adhabu kutozingatia uwezo wa kuhimili, wako watoto wamepata Ulemavu, wapo watoto wamechomwa moto mikono, na mambo mengine ambayo ukiyaangalia unabaini hayakuwa na lengo la kurekebisha tabia, bali kuondoa hasira za mzazi/mlezi/mtoa adhabu, au kulipiza kisasi kwa mtoa adhabu, kwa vile naye alipita kwenye mateso kama hayo (vicious circle of violence) na ambae mara nyingi huja kujutia baadae.. kama huyu mwalimu.
kwa kulinda afya ya muadabiwa na muadabishaji, ni vyema kuwe na kiasi kwenye kila tunalofanya, kinyume na hapo ndo kama haya yanatokea, Sheria zipo na Kuna watu zimewaharibia maisha.
Kila jambo huwa ni la kawaida, na unaweza kuwa na mifano mingi ya jambo kama hilo kufanyika pasipo kuleta madhara, lakini siku madhara yakitokea kwako..ni wewe against The Law