A
Anonymous
Guest
Wakuu, naomba mlifuatilie suala hili, mimi ni mgonjwa ninayepatiwa matibabu katika Taasisi ya Mifupa-MOI.
Kuna changamoto kubwa katika idara ya Radiolojia, hasa kuhusu kuchelewa kwa majibu ya vipimo vya MRI na CT Scan. Wagonjwa hufanya vipimo lakini majibu huchukua muda mrefu kutoka, wakati mwingine hadi zaidi ya wiki moja, hali inayosababisha kuchelewa kwa matibabu.
Kila mgonjwa anapoulizia majibu katika mapokezi ya Radiolojia huambiwa bado hayajatoka, lakini hakuna maelezo ya kutosha kuhusu sababu ya kuchelewa huko.
Mfano, mgonjwa wangu alifanya kipimo cha MRI ya goti tarehe 18/7/2026, lakini hadi tarehe 22/7/2026 majibu yalikuwa bado hayajatoka.
Pia kuna malalamiko kuwa baadhi ya madaktari wanaosoma majibu ya vipimo (Radiologists) hawapatikani ofisini muda mwingi. Inadaiwa kuwa ukifika majira ya saa 7 au saa 8 mchana, ofisi zao huwa hazina wataalamu wengi au baadhi yao huwa wameondoka, jambo linalochangia kuchelewesha majibu ya wagonjwa.
Naomba uchunguzi ufanyike kuhusu utendaji wa wataalamu wa Radiolojia, kwani licha ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wataalamu hao, bado kuna changamoto ya kuchelewa kwa majibu ya wagonjwa. Pia ni muhimu kuwepo kwa usimamizi na uwajibikaji ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa wakati.
Naomba kuwasilisha.