Kuchelewa kwangu kunanitisha sana

Usiogope mdogo angu.Hiki ndio nimekua niki hold kwenye mind yangu.Hujui utatobolea wap cha msingi chagua jambo moja focus kweny hilo kwa mipango na mikakati huku ukiomba sana Mungu.Unaweza ona jamaa zako wamekupiga gap kimaendelepo (age mates wako) ila mitikas yako ikaja ikajibu kwa "exponential rate" kias kwamba ndan ya mwaka mmoja ukafanya mambo ambayo ume delay kufanya kwa miaka mi 5.
Nakuambia haya kwa experience yangu kabisa yan wala simuongelei mtu hapa.
Nilishakaa sina mwelekeo kwa mwaka m1 kipindi flan ila nikafumania deal ya miez 6 ambayo iliniingizia pesa ambayo sikuwah ipata kwa miaka miwili nilipokua nafanya kazi.

Now at 32 by age, nikaamua sasa acha nianze kujipambania kutengeneza stream yangu ya pesa ya kwangu mimi kama mimi (kwa kutumia skills na proffeaion yangu). Nikiwa sipati kitu hata 10tsh yan nikajipa muda and I started constructing my lifetime project.Ikafikia hatua flan nimeiingiza sokon nikaanza kutafuta wateja..kwa miez 4 ya kwanza nikapata mteja mmoja ananilipa 40k kwa mwez....nikaendelea hivyo hivyo huku nikijifunza skills hasa marketing n sales kushawish wateja waiamin service yangu..kwa kifupi mpaka sasa kaz inaniingizia 250k monthly..bado sikati tamaa and i see this very big picture ahead of me though kazi sio rahis has linapokuja suala la kujitengenezea pesa yako mwenyewe kwa kumshawish mtu akupe hiyo pesa in return for solving their problems or improving their lives / works/buznes...
Imagine am 32 years...But i have this COURAGE kwamba things always worka the best for those who BELIEVE in what they do..Believe in their abilities but mostly believe in God in what they do (optional)..na ni waz naona baada ya miaka michache nita collect more than what i collected kwenye ile deal ya miez 6 nilofanya as i explained above..

work hard ..work smart..never giveupp...do not entertain "lezafea"
 
Daaah!!! Umetema madini tu, Safi sana na hayo ndiyo mawazo ambayo Kama vijana tunatakiwa kushirikishana.
Halafu mtu Kama wewe bado upo nje ya system, inasikitishaaa!!!
 
Thankx brathor umeeleza uwalisia kabisa.. yaan umeongea ktu from experience kabisa..
 
Sure
 
Mkuu mimi sitaki kuwa mnafiki,kiuhalisia umechelewa na unazidi kuchelewa na sio peke yako ambae unapitia hiyo hali.

Hiyo misemo tu ya life linaanzia 40,sijui Biden kapata uraisi akowa na 78 years na kitu wanachosidwa kukuweka wazi ni kwamba je hao wakiwa na umri kama wako wa sasa je walikua na hali kama yako kimaisha?
Jibu ni hapana,so si rahisi kuvuka hali kama yako ya sasa ikiwa hata kesho yako hujui unaamkaje.
 
Watu wengi tumekua tukisahau kwamba hata uzima tulio nao ni zawadi tosha toka kwa Mwenyezi Mungu.
 
Hilo la kutochelewa lina maana pana sana.
Mwaka fulani nilihitim kidato cha 4 na ndugu yangu mmoja hivi, tulipohitimu mm nikaenda advance na yule ndugu yangu hakufanikiwa kufaulu akaingia katika mishe mishe, ndani ya hizo mishe mishe akawin sana kimtindo, namaanisha akawa na chenji kwenye account, akajenga nyumba japo hakuweka finishing then akawa na wazo anunue costa ya biashara.


Siku moja akasema atahakikisha anajitahid kufanya vitu vya msingi ili mm nikimaliza chuo nimkute mbali sana, asee kwel vile ninavyorud home hata nauli sina yeye ndo anakuja kunichek, ananichukua kwa pikipiki yake yale makubwa honda na kunizungusha hapa na pale.

Kusema ukwel yale maneno na matokeo yake yalikuwa yananiumiza kichwa sana hadi naona elimu ninayokoma nayo napoteza muda, ila nikajipa moyo kwamba ngoja nimalize kisha niingie kitaa labda mambo yatakuwa sawa.

Anyway nikamaliza chuo nikaanza mishe mishe.

Baada ya miaka 3 baadae jamaa mambo yakaanza kuwa sio, yani hata buku ngumu kuiona. Hapo mishe plus ka ajira vikaanza kuonesha matunda kwa upande wangu.
Kwa kifupi nikaja nikawa vizuri zaidi alipokuwa.

1. Nilipenda vile tulikuwa tunafanya vitu kwa kuwaziana yani niwe mbele zaidi ya mtu fulani, huu ushindani mm huwa naupenda sababu unaleta hamasa na kukupa mood utafute zaidi.

2. Nimetaka kukupa funzo ww mkuu, unayeona leo yuko vzr zaid yako endelea kutafuta zaidi itafika mahala unampita kabisa na unakuwa mbele ya usukani.

Cha muhimu weka juhudi katika kutafuta, weka malengo ya mwaka, mwka na nusu miaka 2. Kisha huo muda ukifika fanya tathmin uone umefika wap na ulifeli wap na usahihishe wapi.

Umri wako ni umri wa kuchukua maamuzi magumu ta kukubadilisha, ila ukweli mwingine mbaya ukivuka huo umri hapo mbele kidogo unafuatia umri wa kuogopa risk, kupuuza vitu, kuogopa kushtakiwa, kufa n.k

Hapo mbele ndio pana umri wa kusema zile kauli

a). Wewe si wakongwe miaka mingi hilo swala haliwezekani na hutaliweza

b). Wewe hiyo hela bora upeleke kanisan usubirie maajabu (magics)

c). Ww unataka kufanya hicho, unajua makato ya serikali, unajua serikali itakufilisi n.k

Mafanikio mema kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee mpili katoboa ana 70+ sasa umechelewa nn? YESU anakaa kwao na anakula kwa baba na
alipokuja Kujitegemea dunian waja wakamletea zengwe akaona isiwe tabu akarudi kwao na anamiaka zaidi ya 2000, we ndo kwanza una 30 hujachelewa popoma kaza
 
Nashukuru kaka umeongea vzuri
 
Hakuna kitu kuchelewa na kuishi mpaka 60 unaweza ishi 80 au 90
 
Majibu yako humu!
 
Zawaya maisha ya kwanza ni kuishi , mungu amekupa uhai na afya yako sasa unaishi.

La pili , jiamin utoke nyumbn ukaanzishe kaz zako ndogo ndogo hope ndio sehemu ya kuanzia

Never lose Hope.
 
Miaka mitatu uliyopoteza hapo ud ungeenda kubeba zege ungepata zaidi ya milioni 2..


Hata hivyo hujachelewa bado
Ni kweli ila kuna baadhi ya matukio katika maisha huwezi ukayazuia .. kwa sababu yanakuwa yana dalili ya kubeba hatma ya maisha yako kama yakienda kama inavyo takiwa ila yakipinda tu unajikuta umepoteza direction ya maisha k
 
Ni kweli ila kuna baadhi ya matukio katika maisha huwezi ukayazuia .. kwa sababu yanakuwa yana dalili ya kubeba hatma ya maisha yako kama yakienda kama inavyo takiwa ila yakipinda tu unajikuta umepoteza direction ya maisha k
Kwel kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…