Kuchelewa kwangu kunanitisha sana

Kuchelewa kwangu kunanitisha sana

yaani kwa kifupi UMECHELEWA punguani wahed wewe, umekaa kwenu unasubiri mafao ya dingi yako? Hovyo kabisa
.. painful ila nalmeza kshujaa...

Ila sadhan kama kuna shida kama mtu akitoa kauli Za kukupa msaada(mtaji) haijalishi uo msaada chanzo chake n wap

Klcho bak n madhaifu tu ya ubinadam bas

Ila kama kusaidiwa n upunguani ..
sawa sidhan kama na ww umepona ktk
Upunguani huo
 
HUJACHELEWA,

Ni nani aliyekwambia, "UMECHELEWA"?

Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kutoka nyumbani.

Aliyekuumba ana "MAKUSUDIO" makubwa juu ya yako kwa kuanza maisha wakati huu.

KUTOKA 4:2 "BWANA akamwambia Musa, Ni nini hiyo uliyonayo mkononi? Musa, Akamwambia, Ni "FIMBO" "?

Wewe una nini mkononi mwako kama "FIMBO" kwa sasa?

Ulichonacho mkononi mwako kitumie kama "FIMBO" kwa sasa. HAPO NDIYO MAHALI PA KUANZIA KWAKO.

Je, Kwangu mimi ipi ilikuwa "FIMBO" yangu wakati naanza maisha? MAEMBE.

Sikuwa na KAZI, AJIRA, wala SHUGHULI iwayo yoyote wakati namaliza shule.

Nikatoka nyumbani nikachume "MAEMBE" kwenye miti nikajaza ndoo kubwa (ya lita 20) ili niende kuyauza kwa wakulima.

Pale nilipochuma MAEMBE kuna jirani mmoja wa kike akaniomba EMBE MOJA wakati naondoka.

SWALI, Jirani yule, ana MIEMBE zaidi ya KUMI (10) ya MAEMBE tena yako karibu, "kwa nini aliniomba EMBE moja tu wakati yamejaa pale pale kwake?"

Akachukua EMBE moja akala, akaniuliza, "Kuna kazi nikikuunganishia utaweza kuifanya"?
 
usikate tamaa kuna jamaa namfahamu alikuja kufanikiwa maisha umri umefika 49.

tena mafanikio yake kila biashara akifanya ilikuwa inatoboa mambo yakawa safi na kununua gari na baadae kupata mke huku upande wa mke wananyumba kariakoo tena katikati ya mji na mrithi ni huyo mtoto wa kike.

kikubwa tumaini mungu ukiomba peke yako.

sikiliza wimbo goodluck -hipo siku tu
 
Inawezekana Baraka na mafanikio yako umeacha kwenye Tumbo la Mama yako.
Unahitaji maombezi kuzitoa kule ziliko fungwa
 
SI Bora ungenitengenezea Mimi app nikupe hata laki Moja duh ila asee yaani amekupa 20000,30000 tu halafu Ni ma star...wakati mm kapuku ningekuwezesha nyingi Zaidi pole Sana ndo maana naonaga Bora mtu ufanye kazi na maskini kuliko na matajiri maana Wana dharau hawalipi madeni

Miaka 30 mbona huna tofauti na Mimi 28.

Sina mke
Sina mtoto
Sina mchumba

Bht nzuri tu Mimi Nimefanikiwa kuingia Serikali mwaka huu pole tusikate tamaa, tutafute mademu wa vijijini ndo rahisi kuwazalisha Hawa wa mjini cum a Nina zao
John ukija Iringa nitafute kuna chimbo lina komoni nzuri sana.
 
Habari zenu binadam wenzangu, wanajamii wenzangu, natumai ni wazima wote.

Swali linalo nisumbua na kunitesa hadi sasa ni kwanini nipo kwenye mfumo wa kuchelewa chelewa sipati jbu.

Umri wa mwanadamu wa kuishi ni miaka 60 tu, na mimi miaka 30 sasa ni Nusu ya umri wa binadam kuishi duniani ila sioni nilichofanya hadi sasa najiona nimechelewa.

Mfano halisi ,baadhi ya sehemu nilizochelewa

Mzee wangu alinipa matumaini makubwa sana ya kusapoti life pindi mafao yatakapo toka(pensheni) ila mafao yake yalipoingia tu akanipiga chini na kunifukuza home kabisa bila sababu za msingi (30yrs now) NIMECHELEWA

Sasa Nina miaka 30, ila nina miezi mitatu tu hadi sasa ya kupanga sijawahi kupanga, NIMECHELEWA

Sijawahi kuajiriwa hata siku 1. Ila nimewahi kufanya kazi chuo kikuu ya kurekebisha na kutengeneza vifaa vya maabara mfano kutengeneza test tube, kuripea burrets zilizovunjika kwa muda wa miaka 3 pale chuo kikuu (UDSM) bila malipo. (30yrs now), NIMECHELEWA

Nina majonzi ya kutengeneza app tokea nna miaka 25 ninajfunza tu ninajfunza Ila hazijanipa muelekeo wowote. (30yrs now) NIMECHELEWA

Napenda sana kufanya project zangu mwenyewe lkn Kila nikipanga mipango haitimii kwa wakati, inachelewa sana sana na haijatimia hadi sasa. (30yrs now) NIMECHELEWA

Sasa Ndugu Wameanza kunitamkia live, mbele ya sura yangu nioe wameniona ..NIMECHELEWA

Marafiki zangu wote wana watoto kasoro mimi tu, (30yrs now) NIMECHELEWA

Hadi sasa sina mpenzi wakusema huyu nifanye nae life hahaha. (30yrs now) NIMECHELEWA

Miaka 14 imepita tokea nimalize form 4, sioni jambo la msingi nililofanya (30yrs now) NIMECHELEWA

Pesa yangu siielewi inaingia kimazabe zabe, niliwatengenezea watu wawili website, mmoja ni mtu maarufu tu star mkubwa mwenye kanisa lake town hapa ila aliishia kuniahidi tu, mwisho wa siku niliambulia elfu 20 yake kutoka kwenye makubaliano ya 600,000sh nayo alinipa kwa sababu alijistukia kupoteza muda wangu.

Mwingine ametoka kunipa elfu 30 wakati alitakiwa kunipa 500,000 sh na story kibao za kuninyima haki yangu. Miaka 30 nafanya dili dhaifu kama hizi kweli NIMECHELEWA

Almost kila siku tokea mwaka huu uingie nawaza kusafisha nyota ila mwez wa kumi sasa

-------NIMECHELEWA------

Ok huku kuchelewa nakuona sio kwa kawaida

Yoyote Aseme kitu kinaweza kuwa mwanga wa safari yangu.
KILA JAMBO LINASABABU. KUMBUKA PIA UMECHELEWA MAMBO YAFUATAYO;
1. KUFA
2.KUWA KICHAA
3.KUWA MLEMAVU
4.KUUGUA KISUKARI,PRESHA,CANCER,COVID19
5.KULAZWA HOSPITALI
6.KUFUNGWA JELA
7.KUJINYONGA
 
Pambana bongo life n ngumu sana mm aliekua ananipa ushauri ye mwenyewe alijinyonga nikabak mm niliekata tamaa kwahiyo maisha hayanaga mwenyewe yakiamua kukuchenjia yanakuchezeshea bakora ujana wako wote na kukuacha uyafaidi uzeeni, au uyafaidi ujanani na uteseke uzeeni au yakucharaze bakora mwanzo mwisho japo wapo wanaoishi vizuri mwanzo mwisho haya yote kaandaliwa mwanadamu ndo maana mwsho wa siku kuna kifo kwa wote pale ndo usawa unarudi ila dunian hakuna usawa Cha msingi tufanye kaz kwa bidii na tumuombe Mungu.
[emoji847][emoji16]
 
Kiuhalisia kuna kuchelewa na kuwahi.
Kwenye maisha hamna kuchelewa wala kuwahi na kila jambo na majira na wakati wake ka ilivo maandiko, so usihuzunike panga mikakati ya kuvuka kwenda hatua nyingine imagine miaka hyo 30 ni wangapi hawapo duniani ka wewe.

Imagine trump kapata Urais na miaka 70s while Obama alipata Urais kwenye umri wa 50s ka sikosei, Joe biden alijaribu mara nyingi ila amekuja kupata Uraisi mda sahihi kwake huku umri ukiwa mkubwa kabisa.

So usi regret njoo na new strategy za kukuvusha mengine huchelewa kwenye maisha Ili kujifunza na tu grow kwanza ku handle situation. Pia waweza pata mafanikio ghafla lakini ukafariki mapema, tushukuru kwa kila jambo jamani
 
HUJACHELEWA,

Ni nani aliyekwambia, "UMECHELEWA"?

Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kutoka nyumbani.

Aliyekuumba ana "MAKUSUDIO" makubwa juu ya yako kwa kuanza maisha wakati huu.

KUTOKA 4:2 "BWANA akamwambia Musa, Ni nini hiyo uliyonayo mkononi? Musa, Akamwambia, Ni "FIMBO" "?

Wewe una nini mkononi mwako kama "FIMBO" kwa sasa?

Ulichonacho mkononi mwako kitumie kama "FIMBO" kwa sasa. HAPO NDIYO MAHALI PA KUANZIA KWAKO.

Je, Kwangu mimi ipi ilikuwa "FIMBO" yangu wakati naanza maisha? MAEMBE.

Sikuwa na KAZI, AJIRA, wala SHUGHULI iwayo yoyote wakati namaliza shule.

Nikatoka nyumbani nikachume "MAEMBE" kwenye miti nikajaza ndoo kubwa (ya lita 20) ili niende kuyauza kwa wakulima.

Pale nilipochuma MAEMBE kuna jirani mmoja wa kike akaniomba EMBE MOJA wakati naondoka.

SWALI, Jirani yule, ana MIEMBE zaidi ya KUMI (10) ya MAEMBE tena yako karibu, "kwa nini aliniomba EMBE moja tu wakati yamejaa pale pale kwake?"

Akachukua EMBE moja akala, akaniuliza, "Kuna kazi nikikuunganishia utaweza kuifanya"?
Amina... somo la fimbo nmelielewa sana
 
Kiuhalisia kuna kuchelewa na kuwahi.
Hizo zote ni mindsets tu ambazo hufanya watu wawe na stress Kuna people Wana hustle na wako smart ila progress Yao ni slow wengine kawaida tu mambo yananyooka so hyo kuchelewA kuliko wekwa na standard za jamii kusikatishe watu tamaa ya ku fight kwenye maisha
 
Pole sana mkuu, ulivyokuwa unaandika nikahisi unaniandika mimi kabsa maana ulichondika ndyo Maisha yangu mimi na umri wangu ni hvyo hvyo.

Sina mchumba, sina kazi, sina asset yeyote Ila bado sijakata tamaa. Wadogo zangu wanafamilia zao na watoto Ila mimi naamini kuwa wao ni tofauti na mimi.

Pamoja na nilivyo siachi kupanga yajayo.

See you at the top
Komaa kijana utatoboa
 
Back
Top Bottom