Mkuu... hauko peke yako. Wapo vijana wengi tu wana hiyo hali na wengine wamekata tamaa na kujiingiza kwenye tabia hatarishi ama wengine kujidhuru.
Shukuru MUNGU kwa kuwa una akili timamu mpaka umeona hiyo hali siyo ya kawaida. Mimi kuna mtu namfahamu tangu ana 2011 anajitahidi kutoboa lakini hivi ninavyoongea yupo mkoani amehama dar amejianzishia maisha simple tu mkoani, ana familia na ana furaha. Huyu ninayemtaja hapa ameshaandika proposal kibao, alifungua kampuni, ameshaenda ofisi nyingi hapa dar akitafuta tender, ameshaingia mabalozi kibao kutafuta fursa za kupata grant afanye kazi au hata aende nje ya nchi. Huyu amewahi hadi kupeleka proposal ikulu akitafutafuta maisha.
Hawa wapuuzi wanaotutuma halafu wanatupa shilingi elfu 20 ya nauli pamoja na lunch hata mm nimekutana nao. Wapo wengi tu hapa mjini. Nimewahi kuandika proposal kwa makubaliano ya laki 4 lakini nilichezewa mchezo nikaambulia elfu 50 tu. Nimewahi kutengeneza website sikumbulia kitu. Jamaa aliionyesha kwa wadau aliotaka waone hyo website alipopata anachotaka akaitelekeza ikiwa sijaikabidhi (yaani nikiwa sijampa credentials za login).
Ili uamini hauko pabaya, mimi nimekuzd kidogo umri ila sijafka 35.
Sina mke, au mchumba au mwanamke ambaye ninaona tunaweza kujenga maisha pamoja. Wanasumbua tu.
Sina kiwanja.
Sina mradi wowote wa maana kusema unaniingizia kipato cha maana.
Nina mshahara wa mhindi ambao naona unanilemeza niendelee kuishi kwenye mwamvuli wa wazazi wangu. Nawaza niwaache kazi yao.
Cha kufanya, change direction. Nina maana,
Tafuta watu wapya, wenye uchungu na maisha kama wewe na ambao hawataishia kukutmia tu. Nina maana, hyo idea yako ya app ifanye na like-minded people ambao mtasogea pamoja huku mkitafuta support ya kuifanye iwe implemented.
Usiache shughuli za hapa na pale, mfano kutengeneza website. Cha kufanya, be organized. Kuwa na ofisi, kuwa na documentation, fanya branding, halafu jitangaze. Kazi na malipo yake yanakuja according to how you present yourself.
Ondoa watu ambao ni mzigo kwenye maisha yako. Marafiki wasio na machango chanya, mahusiano, mazoea yoyote yasiyo na tija achana nayo. Take control of your life.
Nisikuchoche sana bado yapo mengi sijaandika hapa ila kikubwa jipe moyo bado muda upo, kwa ushauri zaidi karibu sana inbox.