Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Maneno Meier,

Kwa taarifa yako kwa tulipofikia ni bora kuendelea kushitaki kwa wazungu kuliko kujifanya mzalendo kwenye nchi yenye uonevu wa wazi na utawala wa kihuni. Na ikitokea uchaguzi wa haki huyo Lissu na Zito watapata uongozi bila shida. Ni bora kutawaliwa na wazungu kuliko viongozi weusi wenye mitazamo ya kijamaa, yenye kila chembe ya umasikini.

Sasa hivi mifumo yote imetawaliwa na mtu mmoja, na hakuna uwanja wa mawazo tofauti kuheshimiwa, na chaguzi za nchi yetu zinanajisiwa wazi wazi, katika mazingira hayo ni bora kwenda kwa wazungu na kuweka wazi huo uhayawani wote, waweke vikwazo mpaka turudi kwenye mstari wa kuheshimu mawazo na uhuru wa watu. Zito ahakikishe anazunguka huko kwa wazungu na kuweka wazi matumizi yote mabaya ya madaraka humu nchini.
 
Msimutukane Wala kumulaumu dogo zitto kabwe yawezekana barehe inamurudia ndo maana Akili zinamuruka na chunusi kumutoka( hizi Ni dalili za barehe). Kwahiyo huruma na maombi yenu yanahitajika kabla huyu kijana hajarejea barehe yake totally.

Note: Ni vigumu Sana kumukuta mtu mzima anaejielewa anafanya unafiki Kama huo. Hata H.clinton hawezi kufanya unafiki wa namna hiyo kwa marekani licha ya kushinda kwa kura nyingi za Wamarekani.

Anachokifanya Zito yuko sahihi, hakuna kuendesha siasa za kinafiki, kwenye nchi ambayo uchaguzi unanajisiwa, na chama kimoja kulazimisha kupita nchi nzima bila kupingwa, hakuna kukaa kimya hapo. Zito azunguke huko nje na aseme ukweli wote wa huu uhuni unaoendelea humu nchini.
 
Hata yule, na yule mwingine, na Erick Kabendera walikuwa wanashangiliwa na kutiwa hamasa hivyo hivyo.
Siku ya majanga wengi hujikuta peke yao, sasa wamebaki peke yao na majuto makubwa.

Kwa taarifa kinachomkuta Kabendera ni uonevu ambao ndio huo unabackfire, na bado hatua zaidi zitazidi kuchukuliwa. Hiyo mwingine mtaje wala usiogope na majibu yake tunayo.
 
Zitto hodari sana kwa kushangilia na kuwatia moyo wenzake baadaye anaingia mtini. Tatizo wenzake hawajastuka wala nini. Kama CHADEMA wasingemtoa baruti sidhani kama leo chama kingekuwepo. Hatari sana huyu mwanasiasa..

Kaingia mitini wakati saa hii yuko anakata mitaa huko ulaya na wanaccm wanatoa povu kama lote?
 
Z
Kama ni kweli kwamba barua hiyo imeandikwa na mheshimiwa Zitto, basi amekuwa muungwana sana, kwani hayo yote ndiyo yalisemwa na Jiwe katika hotuba yake ya kuwapatia kibali watanzania wawafyatue watoto kadri wawezavyo ili naye awasomeshe.

Sijaona uongo wa Mh. Zitto hapo. Wanalumumba msijaribu kupotosha ukweli wa alichokisema Meko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania tuna Memkwa, Tuna QT, Tuna Private Candidate au nyie mnachomaanisha na Zitto Kabwe @Shog ni kipi, kwani hata Mkeo amezuiwa kwenda kusoma. Mnamaana gani. Zitto alichokiandika kinaakisi uwezo wake mdogo wa kufikilia.
Zitto Kabwe nakujumbusha IQ yako imepungua imeenda chini ya zero. Wewe ni Popo unaweza kuruka usiku, unazaa wakati unamabawa haueleweki ant Zitt Kabw kama upo kundi gani .
We tired with u Zigo, go go.
 
Elia thamani yako humu JF imeporomoka mithili ya visivyomithilika, unatia aibu mno!
Uwezo wa Elia huwezi kuufananisha na Zitto Kabwe, ndiyo maana Zitto Kabwe alienda kumpigia Magoti akimuomba ajiunge na ACT Wazalendo lakini aligoma.

Sababu za kugoma kufanya kazi na Zigo ni kutokana na tabia zake chafu za upigaji dili, kufanywa, kujiita Kiongozi Mkuu wakati ni Zero brain na aliondoka patupu UDSM, kujifanya mzalendo wakati Maisha yake yote ni uongo na utapeli
 
Elia F Michael,
Umepiga porojo ndefu sana lakini hiyi barua unayisema ya siri, ukweli ni kuwa siyo ya siri.

Barua ni rasmi kutoka kwa mbunge kwenda world bank. Ina nembo za serikali na bunge na imetoka kwa mbunge. Na siyo ya kwanza kwani ukiisoma anakumbusha pia barua zake za kanla za kwrnda huko World Bank.

Kama upinzani hauna haki ya kuwa wapinzani kwa kupinga hapa ndani ya nchi unategemea watapeleka wapi pingizi zao?

Kwa mtazamo wangu, Zittoyupo kazini anafanya kazi yake iliyompeleka bungeni.

Sijaona baya aliloandika Zitto na sijaona baya kutoka World Bank baada ya barua hiyo.

Hiyo batua ingekuwa siri ingeandikwa neno "secret" kwa kuwa ni barua rasmi.

Wabunge ikiwa kazi zao zitakuwa siri basi wana faida ipi ya kuwa wabunge?
 
Nimekuwa nikiangalia tabia ya Zitto tangu alipounda chama chake, akitoka CHADEMA. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kujilazimisha kuunga mkono hoja za CHADEMA zikiitwa ni za UKAWA. Tangu Mwanzo yeye hakuwa na wenzake na ndo maana aliwaacha wenzake na kuingia bungeni wakati rais akihutubia Bunge.

Baadaye kapata njia, kupitia kwa Maalim lakini, ana tatizo jipya la uwezekano wa kukosa ubunge. Uwezekano huo ni mkubwa kwamba, hatarudi bungeni kazi aliyoizoea kwa miaka mingi bila umahili wowote kwa kazi nyingine.

Nimuonavyo, sasa anahangaika kupata umaarufu. Naamini anahanigika kupata ajira nje, Kwenye mashirika hayo akiaminia kwa sasa watauona uelewa wake. Nampa hongera kama kweli atapata ajira aina hiyo lakini aelewe hana uzoefu wowote nje ya shughuli za Bunge.
Mi nakuunga mkono maana naona kuna mlipuko wa waunga mkono wa hoja ya Zitto. Tangu lini raia, Mbunge akaishinikiza serikali nje ya Bunge? Eti anaadika barua. Ni yale yale ya Lissu kuamini bunge la ulaya litamsaidia apate anachokitaka Tanzania. Ni upuuzi tu! Au CHADEMA kwenda ubalozi wa EU kuishitaki serikali wakijua staff ya EU iko nchini kuwasiliana na serikali na si vinginevyo. wako wapi?

Ni suala la muda. Wanajaribu kuonesha kwamba wanajali hoja zake lakini Benki ya dunia hutoa mikopo, siyo misaada na wangependa sana nchi zertu zikope. Hawajali unapeleka wapi pesa hizo labda isikike kwamba unapeleka kwa Osama.
 
MLETA UZI WEWE MWENYEWE AJIRA HUNA, HATA MILO 3 HUPATI. PELEKA UJINGA WAKO KWA MACCM WENZAKO
 
Anachokifanya Zito yuko sahihi, hakuna kuendesha siasa za kinafiki, kwenye nchi ambayo uchaguzi unanajisiwa, na chama kimoja kulazimisha kupita nchi nzima bila kupingwa, hakuna kukaa kimya hapo. Zito azunguke huko nje na aseme ukweli wote wa huu uhuni unaoendelea humu nchini.
Bwashee...
mwenzio zitto Watoto wake hawasomei shule anazohangaika nazo kila siku zinyimwe msaada. Mwisho wa siku atakaekuja kuumia Ni wewe ambae Watoto wapo kwenye hizo shule zinazotegemea msaada.

Na kwa akili yako na ya zitto inaonesha wazi kabisa kuwa nyie ndo wale wanaume ambao mkigombana na wake zenu, ugomvi na chuki zenu mnazipeleka Hadi kwa Watoto wenu.

Jitafakari Kaka hizo misaada haziendi kwa Magufuli Bali zinaenda shule za Watoto wa masikini walio na uhitaji wa misaada. Tofauti zenu za kisiasa na Uchumia Madaraka wenu Usifanye Watoto wasome kwa shida.

Kumb: "Unapopambana na Hali yako angalia Sana usitikise ya mwenzako"
 
Anachokifanya Zito yuko sahihi, hakuna kuendesha siasa za kinafiki, kwenye nchi ambayo uchaguzi unanajisiwa, na chama kimoja kulazimisha kupita nchi nzima bila kupingwa, hakuna kukaa kimya hapo. Zito azunguke huko nje na aseme ukweli wote wa huu uhuni unaoendelea humu nchini.
Nawe unakuwa bwege wa wanasiasa. Zitto siyo mnafiki? Kuna mwanasiasa ambaye siyo mnafiki? Alipokuwa anapiga rushwa kwa mambo ya Buzwagi alikuwa anakutetea wewe? Shiiiit!
 
Mtaimba mapambio yote..Tunasema wachochea kuni ongezeni kuni.
Kwa maoni yako unadhani utapata nafuu ya maisha kwa hizo kuni? Najua wengi tatizo hata siyo mkopo maana hamkujua hata huo mkopo. Tatizo ni maisha magumu. Pesa! Lakini, nani akugawie?
 
Back
Top Bottom