sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Ni ushauri kwa vijana na wazazi wenye vijana ambao wanataka kuingia kwenye haya mambo,
Kwa nchi yetu tuwaase zaidi vijana wanaotaka kucheza mpira kuna chance nzuri ya kufanikiwa ila hawa wanaotaka kuimba watafute shughuli zingine, mziki waufanye kwa burudani tu maana chance yake ni ndogo sana kwa wachache sana.
Diamond naomba tumuondoe kabisa kwenye list, huyu ana vitu vingi sana kuanzia ujasiri wa kipekee ndie msanii wa kwanza kuwadindia clouds Fm na wakamuomba msamaha, Ana connections nzito sana, Ana nyota ya kupendwa (Ngekewa), licha ya umaarufu hana dharau wala kiburi wala kujisikia, ana uwezo wa kujifunza vitu haraka kama lugha na sasa kajifunza biashara ni muwekezaji ambae anaingiza mabilioni nje ya mziki, n.k. Awekwe pembeni.
Binafsi nachoona ni wasanii ni wachache sana wanaoingiza hela kwa mziki pekee na kinachoumiza wasanii wengi ni kulazimika kuishi maisha ya juu ili kuendana na maisha ya muziki, mfano kuishi nyumba za milioni 3 kwa mwezi, kuvaa nguo za gharama, bando la laki 3 kwa mwezi, n.k. hapa unakuta pesa yote inayopatikana inaishia kwenye matumizi na mambo yakibana ndio wanaanza kuishi maisha feki na stress ndipo zinapoanza wengine huingia kwenye ulevi na madawa ya kulevya, Hata Vanessa Mdee aligusia hili kuwa cha pombe maana mziki ulikuwa haumlipi vizuri ila analazimisha kuonekana pesa zipo.
Tukija kwa wachezaji wa mpira wa ligi kuu wapo zaidi ya 300 na wote wana uhakika kuingiza mkwanja kila mwezi ila ni kwamba wanatofautiana mishahara, wanaweza kutunza esa zaidi maana hawana msukumo wa kuishi maisha ya kifahari, sihning fee wanayopewa wakinunuliwa ni pesa zinazoweza kujenga hata nyumba, Pia kumbuka Bakhresa anatoa shilingi milioni 50 kila mwezi kwa kila timu ya ligi kuu kwa hio hata mchezaji acheze timu ndogo uhakika upo.
CONCLUSION: Kucheza mpira kuna uhakika zaidi kuliko Muziki?