Hapo vyote majanga tu
Mpira majanga maana waliopewa dhamana ya Michezo hawaibui vipaji wapo tu maofisini huko wanakula Pesa za Serekali
Muziki huku mpaka upigane mwenyewe na ligi yake kutoka underground mpaka uwe star uwe na watu wa kutosha nyuma yako
Young Lunya nyuma yake kuna Bobo, Tajiri Abbas, Petiman Wakuache na wadau wengine km Roof Top Ent hapo bado hujaigusa Sony Music
Sasa kijana kufikia hatua hio ni Safari ndefu yenye majasho mengi na kula vumbi sana Ila Sanaa inalipa Barnaba msanii mwanamuziki anamiliki Nyumba 2 za kifahari kwa kupitia mziki
Mziki ni Pesa mziki umebadirisha Maisha ya watu tena huu mziki wa sasa hivi huu ukiingia studio ukabahatisha dundo ukiingia studio ukabahatisha hit song ukadondosha ngoma kali km zile alizotoa Jux bila kumsahau Marioo tukiwa km pipo tutakutana.. wewe unakula bar unalala bar Ila deni langu hunilipi.. wewe kesho unaamka tajiri mirabaha kila club kila bar mziki wako ukipigwa unalipwa kila mwezi kwa mwaka unakuja kibunda hata cha kuagiza Kajala 1&2