Kucheza mpira kuna uhakika zaidi kuliko kuimba Bongo Flava. Ewe kijana ama mzazi mwenye kijana, Mpira Ruksa ila Bongo Flava iwe burudani tu

Kucheza mpira kuna uhakika zaidi kuliko kuimba Bongo Flava. Ewe kijana ama mzazi mwenye kijana, Mpira Ruksa ila Bongo Flava iwe burudani tu

Naona Konde boy jana alikuwa anapiga Njombe, show za nje zimepungua sana
Tanzania ingeweza ''kuzalisha'' wachezaji kandanda wengi kama tungekuwa na mikakati mizuri. Wala haihitaji fedha nyingi lakini CCM ku',m. nina. Ilaaniwe.
 
Amefanya Vizuri kukumbuka kujiwekeza

Ni aibu mchezaji uliyecheza kwa mafanikio huku ukilipwa mamilioni ya fedha kupita pita mtaani kuomba omba kama baadhi yao.

Wakumbushwe kuwa Wataweza kucheza vizuri hadi miaka 35 lakini baada ya hapo wataelekea kustaafu hivyo maisha yao yatategemea namna walivyojiwekeza.

Ukiwa mtu wa sketi na pombe hutaweza kufika hata umri wa miaka 35 ukicheza
Nyongeza lkn wasanii mpaka miaka 70 hadi 100 wanaendelea kushika mic mfano bi kidude, koffi, papii kocha, na kitambaa cheupe.
 
Nyongeza lkn wasanii mpaka miaka 70 hadi 100 wanaendelea kushika mic mfano bi kidude, koffi, papii kocha, na kitambaa cheupe.
Wasanii wengi wanaoforce game wakishazeeka hua aidha wanafia jukwaani au wanakufa siku 1 kabla ya show

Papa Wemba kafia jukwaani tatizo la moyo
Pepe Kalle kafia hospital issue imeanzia nyumbani tatizo la moyo
Madillu System kafia hospital issue imeanzia nyumbani tatizo la moyo
 
Hapo vyote majanga tu

Mpira majanga maana waliopewa dhamana ya Michezo hawaibui vipaji wapo tu maofisini huko wanakula Pesa za Serekali

Muziki huku mpaka upigane mwenyewe na ligi yake kutoka underground mpaka uwe star uwe na watu wa kutosha nyuma yako

Young Lunya nyuma yake kuna Bobo, Tajiri Abbas, Petiman Wakuache na wadau wengine km Roof Top Ent hapo bado hujaigusa Sony Music

Sasa kijana kufikia hatua hio ni Safari ndefu yenye majasho mengi na kula vumbi sana Ila Sanaa inalipa Barnaba msanii mwanamuziki anamiliki Nyumba 2 za kifahari kwa kupitia mziki

Mziki ni Pesa mziki umebadirisha Maisha ya watu tena huu mziki wa sasa hivi huu ukiingia studio ukabahatisha dundo ukiingia studio ukabahatisha hit song ukadondosha ngoma kali km zile alizotoa Jux bila kumsahau Marioo tukiwa km pipo tutakutana.. wewe unakula bar unalala bar Ila deni langu hunilipi.. wewe kesho unaamka tajiri mirabaha kila club kila bar mziki wako ukipigwa unalipwa kila mwezi kwa mwaka unakuja kibunda hata cha kuagiza Kajala 1&2
 
Ngumu mno mpira mpaka uonekane na mtu mwenye connection ndani huko ndio unaingia na wewe hivi hivi utachezea cha Ndimu mpaka unakua Veteran huendi popote
Kuna jamaa yangu alikua anatumia mguu wa kushoto, aisee yule mwamba alikua foward matata sana.
Ila ndo ivo akaishia kucheza ndondo tu mpaka sasa kaacha hata hizo ndondo.
 
Mpira huu huu tunaoujua sisi.
Wadogo zetu wakiwa Off season wanaomba buku,jero na vizinga vingi.
Wameenda wazima wamerudi Wala bange, wapenda Waganga na majeuri Kama sio matapeli.

Mpira wa Bongo uskie hivyo hivyo. Na kibaya zaidi wachezaji wengi wanatokea uswazi na ni wapenzi wa kuu wa visingeli ....nafkiri unajua sifa ya hivyo visingeli.
 
Nyongeza lkn wasanii mpaka miaka 70 hadi 100 wanaendelea kushika mic mfano bi kidude, koffi, papii kocha, na kitambaa cheupe.
Sahihi Mkuu

Ila wasiache kujiwekeza kila wanapofanikiwa kuzipata.

Kila siku Wanaibuka Wasanii wapya, kwahiyo kuendelea kubaki on top inaweza kuwa mtihani kwa wakongwe.
 
Back
Top Bottom