Kudai Israeli ni Taifa la Mungu huku Wayahudi wakimkaata Yesu, ni ushahidi hizi dini zimejaa uongo mwingi

Kudai Israeli ni Taifa la Mungu huku Wayahudi wakimkaata Yesu, ni ushahidi hizi dini zimejaa uongo mwingi

Suala la wayahudi ku ni wateule wa Mungu ni uongo uliopachikwa kwenye bible
Ila uzuri hulazimishwi kuamini hivyo sawa na ambavyo hupaswi kumlazimisha mtu aamini unachokiamini wewe, hiyo ndio maana ya imani tofauti na sayansi.
 
Kuwa IsraeI ni taifa takatifu hilo ni la Mwenyekiti Mungu mwenyewe muumba wa Mbingu na nchi na yeye ndiye anayejua kwanini amelichagua taifa hilo kuwa takatifu.hilo halituhusu na sisi binadamu hatuna uwezo wa kuhoji.wewe kiumbe tu unahoji maamuzi ya Mungu?unajua nini wewe?
 
Israel na wayahudi ni vitu viwili vinachanganywa.
Uyahuni ni kabila na ambalo japo Kuna wakristo waislamu na wafuata Torati.
Ardhi takatifu Kwa Sasa ni maeneo yanayokaliwa na wapalestina na waIsrael .
Kuna wanaosema wapalestina ni waarabu lakini ushahidi wa DNA unaonesha wapalestina Wana ukaribu wa nasaba na wayahudi wa miaka iliyopota.
Kuna muamko wa kizayuni /Zionism ambao ktk Israel ni kama vile ulokole wa hapa nchini ,wao wako kinyume na makanisa ya asili kama RC Lutheran au Anglican.
Zions ni walokole wa kiyahudi ambao wanachalenge mfumo wa Asili , orthodox , shughuli yake ni nzinto ni kama Leo watu wa upako waambie kuhusu meza ya bwana.Hivyo na mapigano wataendelea na hakuna wa kuwashauri labda nabii arudi.
Hii ni screen shot kuonesha watu wenye akaribu wa NDA na wayahudi wa Asili Kwa takwimu ya Sasa.
Screenshot_2023-11-12-12-01-53-968_com.twitter.android.jpg
 
Kuwa IsraeI ni taifa takatifu hilo ni la Mwenyekiti Mungu mwenyewe muumba wa Mbingu na nchi na yeye ndiye anayejua kwanini amelichagua taifa hilo kuwa takatifu.hilo halituhusu na sisi binadamu hatuna uwezo wa kuhoji.wewe kiumbe tu unahoji maamuzi ya Mungu?unajua nini wewe?
Mungu asie na upendeleo, kapendelea Taifa moja!!

Contradictions tupu!
 
Kuwa IsraeI ni taifa takatifu hilo ni la Mwenyekiti Mungu mwenyewe muumba wa Mbingu na nchi na yeye ndiye anayejua kwanini amelichagua taifa hilo kuwa takatifu.hilo halituhusu na sisi binadamu hatuna uwezo wa kuhoji.wewe kiumbe tu unahoji maamuzi ya Mungu?unajua nini wewe?
Tatizo husomi Neno alilokupa Mungu. Utajuaje sasa?

👉42. Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?

👉43. Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. ~Mathayo 21:42, 43
 
Hebu nikubali hoja yako for the sake of argument......Sasa nini kifanyike.....Maana kila attempt toka 1948, 1967, 1973 inashindwa......tunaona Gaza inamegwa vipande viwili mbele ya kadamnasi ya dunia....Iran, na mataifa ya kiarabu yanatoa matamko tu....What is the solution.....Wanachoweza kulia ni cease fire...cease fire...Humanitarian aid....Humanitarian aid.....Solution ni nini ndugu yangu Steven.....Ponda kajaribu kwenda kufanya Maandamano, Plosi CCM imemzua....labda ingesaidia......Nini kifanyike...?
Hao wana uhasama wa kudumu, tulizaliwa wanapigana na tutakufa tukiwaacha wanapigana.
 
Wengine kumkataa Yesu ni sawa na kumkataa Mungu, ila wengine wanamkataa wazi wazi na bado wanaitwa ni Taifa telule la Mungu!!

Kuna logic hapa kweli?
INRI (IESVS NAZARENVS REX IVDÆORVM) au kwa Kiswahili "Ywsu Mnzareti Mfalme wa Mayahudi"

Hayo ni maneno ya Pontius Pilato (Yohana 19:19). Mimi ni nani nimkatae Mfalme wa Mayahudi?
 
Kabla sijaenda mbali, kwanza nikiri mimi ni Mkristo, ila Ukristo wangu sio sababu ya kutohoji hata kama mtasema imani yangu ni ndogo.

Tukirudi kwenye mada, huku kwetu ukimpinga Kristo, hutaeleweka na utachakuliwa kuwa ni mwenye dhambi na unastahiili kuombewa.

Hata hivyo, cha kushangaza, wakati sisi tunaodai Israel ni Taifa telule la Mungu, Wayahudi wenyewe hawamkubali Yesu, na wameukataa kabisa Ukristo.

Kwa kifupi, jambo hili linaweza kuwa ni ushahidi tosha kuwa katika hizi dini, kuna mambo ya kutunga katika hivi tunavyovitta vitabu vitakatifu na huenda ni maandiko/aya zote ni uongo au baadhi ya maandiko/aya ndio za uongo .

Pia, nawaza,Tulia watanzania wengi hawamkubali, lakini huko nje ya nchi wamemkubali na kumpa cheo kikubwa tu. Je, ndio yale yale ya Wayahudi kumkataa Yesu na sisi huku kumkubali kama Mwana wa Mungu?

Hakika maswali ni mengi kuliko majibu.
Evangelical Christians wa Marekani ndio wapo mstari wa mbele kuiunga mkono Israel kwa hiyo hoja kuwa ni taifa teule la Mungu, na mafundisho yao yameenea mpaka huku Africa na wengi kuamini hivyo.

Ila kiuhalisia waliompokea Kristo na kuongozwa na Roho wa Mungu ndio taifa teule la Mungu hivyo 'uteule' ni mambo ya rohoni.
 
Jews believe the Messiah will be a direct (blood) descendant of King David through Solomon on his father's side and will be born naturally to a husband and wife (Genesis 49:10, Isaiah 11:1, Jeremiah 23:5, 33:17; Ezekiel 34:23–24).

"The point is this: that the whole Christology of the Church - the whole complex of doctrines about the Son of God who died on the Cross to save humanity from sin and death - is incompatible with Judaism, and indeed in discontinuity with the Hebraism that preceded it."[18]
Nimesoma hiyo Mwanzo 49:10 sijaelewa kabisa hoja yako, sijaona pale walipomkana Yesu na Yesu kwenye Agano la kale hakuwepo.
 
Ipo siku hata hao waarabu watamkataa mudi hapo ndipo akili zitawakaa sawa haya mambo ya kuletewa tena ili tutawaliwe hayawezi kutuacha salama kamwe. Fikiri mzungu angeleta dini kwa upendo upi alio nao kama asingekuja kukomba mali ghafi
 
yaani na sisi wamakonde wa Ntwara leo tuandike kitabu sisi ni Taifa teule na tuhubiri hivyo mpaka 4520 huko, bila shaka kuna watakaotuamini tu na kukubaliana na sound zetu..

Yaani mwenyezi aumbe ulimwengu na wanadamu halafu miongoni wa hao binadamu abariki kizazi fulani fulani tu, eti na wengine ili mbarikiwe lazima muwabariki hao aliowabariki, hakujawahi kuwa na Mwenyezi Mungu atayeweza kubagua wanadamu aliowaumba wenyewe waishi kwa misingi aliyoiweka.
 
Mleta hoja kuna kitu unatakiwa ujue wayahudi ni kabila kama unavosema wasukuma na kinachofanya wayahudi waonekane ndo Israel yenyewe nikwasababu wao ndo wengi na wenye nguvu pale,,,,sasa wasukuma wakiukataa ukristo huwezi kusema Tanzania imeukataa ukirsto,,,,afu kuna kitu unapaswa ujue kama wewe ni muumini wa dini yoyote,,,mngu anaweza kuyaacha mabaya yakukute kwasababu za unabii wake utimie,,,,,,wauwaji,wezi,waongo,wazinifu,,,wote tunaishi nao unafikiri mngu hawaoni??anasabbu zakuwaacha hai;;;;mngu alilichagua lile taifa pawe mahali pakumiliza unabii wake,,,,we fikiria ugomvi uliopo kati ya Palestinian na Israel kinachogombewa kikubwa ni masuala ya imani hapo kwa akili yakawaida tu unaelewa haijalishi mkristo yuko sawa myahudi yuko sawa ama muislamu yuko sawa lakini pana mgongano mkubwa wa kiimani mahala pale
 
Mimi ni mkristo ila nawaambia kupitia bibilia yesu hakusema wafuasi wangu muitwe wakristo. Yesu anamajina mengi sana kwenye bibilia hadi mengne anayakataa mfano jina mwema. Kristo,mwana wa adamu,kweli,mwana wa mungu n.k ni majina tu yalyotumika kumtambulisha yesu. Kwa hyo kristo ni jina na sio dini
Kiasili, 'kristo', siyo jina la Yesu. Ni neno lililotoholewa kutoka kwenye neno christos, kwenye lugha ya Kigiriki. Neno hilo Christos kwa Kiebrania lilitafsiriwa kama meshiah (messiah), linalomaanisha, 'mpakwa mafuta'.

Waliofuata mafundisho ya Yesu, walianza kuitwa wakristo wakati wa mitume. Na kwa mara ya kwanza kwenye biblia lilianza kutumika kwa waumini wa Yesu huko Antokia. Kuna wakati, wanaofuata mafundisho ya Yesu waliitwa 'wanazarete'. Msingi wa kuitwa wakristo au wanazareti ni kwa sababu watendo yao yalifanana na masiha mpakwa mafuta.
 
Zote hizi ni imani ambazo hakuna mwenye uhakika kama ziko sahihi au ni mambo ya kufikirika tu kwa malengo fulani.
Kwani imani ni nini?.Ata mada uliyoileta inatokana na imani pia.kwasababu wote hatukuwepo na hatujui nikwanini iko hivyo zaidi yakusoma tu vitabu ambavyo sio lazima uviamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida watu wakipata pesa kidogo au wakiwa na afya njema huwa hawaoni uwepo wa Yesu wala Mungu subiri awe kwenye shida, hata Babu Oseya(mwanamziki) wakati yupo gerezani alituma ujumbe kuwa siku akitoka gerezani atamtukuza MUNGU na kumtumikia lakini baada ya kutoka akarudi kule kule. Lisu alipigwa risasi 38 lakini hakufa hapo hapo kuna watu wakipigwa hata na manati wanakufa.
Umeongea pointi mkuu
 
Hao wana uhasama wa kudumu, tulizaliwa wanapigana na tutakufa tukiwaacha wanapigana.
Labda niiweke sawa hoja yako.....Ni ugomvi wa Imani kuliko watu wanavyofikiri.......Kila upande hiyo ardhi ni sacred ...Halafu interests nyingine zinakuja juu yake.....Myahudi na Mapelestine wote wana historical attachment na hiyo ardhi.....! HAKUNA ANAWEZA KUWEKA SAWA HILO TATIZO....NI KULIPOOZA TU!
 
Back
Top Bottom