Kabla sijaenda mbali, kwanza nikiri mimi ni Mkristo, ila Ukristo wangu sio sababu ya kutohoji hata kama mtasema imani yangu ni ndogo.
Tukirudi kwenye mada, huku kwetu ukimpinga Kristo, hutaeleweka na utachakuliwa kuwa ni mwenye dhambi na unastahiili kuombewa.
Hata hivyo, cha kushangaza, wakati sisi tunaodai Israel ni Taifa telule la Mungu, Wayahudi wenyewe hawamkubali Yesu, na wameukataa kabisa Ukristo.
Kwa kifupi, jambo hili linaweza kuwa ni ushahidi tosha kuwa katika hizi dini, kuna mambo ya kutunga katika hivi tunavyovitta vitabu vitakatifu na huenda ni maandiko/aya zote ni uongo au baadhi ya maandiko/aya ndio za uongo .
Pia, nawaza,Tulia watanzania wengi hawamkubali, lakini huko nje ya nchi wamemkubali na kumpa cheo kikubwa tu. Je, ndio yale yale ya Wayahudi kumkataa Yesu na sisi huku kumkubali kama Mwana wa Mungu?
Hakika maswali ni mengi kuliko majibu.
Unayesema na kuamini Israel ni taifa la Mungu hujui maandiko. Ndo wale bendera fuata upepo.
Hapo mwanzo hapakuwa na Israel. Kulikuwa na mataifa mengine lkn Israel haikuwepo.
Israel inaanza kunikia baada ya Ibrahim kutokewa na Mungu na kupewa ahadi ya kupewa nchi na uzao wake kuzidi sana.
Ibrahim akamzaa Isaka, Isaka akamzaa Yacob ambaye alizaa wanamme 12 ndiyo kabila kumi na mbili za Israel. Ahadi ya Ibrahim, ikafikiwa na uzao wa Yakobo ambaye ndiye aliitwa Israel na mwanzilishi wa taifa linaitwa Israel.
Yakobo/Israel alichaguliwa na Mungu mwenyewe ili kutimiza ahadi ya Mungu kwa Ibrahim babu yake.
Hata hivyo wana wa Israel yaani vitukuu, vilembwe na vizazi vilivyofuatia, vilikataa kutawaliwa na Mungu, wakataka wafalme wa kibinadamu kama yalivyokuwa mataifa jirani. Wakapewa Saul, Daud, Suleiman na ufalme wa Israel ukavunjikia kwenye uzao wa Suleiman.
Mungu alichukuzwa akawatawanya wakasambaa dunia nzima. Wakawa chini ya utumwa wa kirumi na mataifa mengine ya uajem etc.
Baadae akaja Yesu, wakamkataa, hawakumkubali, Yesu akawageukia mataifa, wakamkubli ndiyo sisi. Waisrael walimkataa ili kutimiza unabii tu, hawakuwa na namna. Yesu alikuja ili kuukomboa ulimwengu wote toka utawala wa shetan, utawala wa dhambi.
Taifa la Mungu kwa sasa siyo la hapa duniani lenye miliki ya ardhi nk, hapana, ila taifa la Mungu ni wale wote waliokubali kuishi kwa kufuata kanuni za Yesu Kristo.
Mapigano ya waisrael si ya Mungu bali ni yao wenyewe wakidai ardhi yao na miji yao. Mungu hahusiki hata kidogo. Ukiokoka, unakuwa mkristo na raia halali wa taifa teule la Mungu yaani wakristo. Ninaposema wakristo usikimbilie hayo madhehebu yenu, bali ni watu waliokataa madhehebu wakamfuata Yesu Kristo 1kor 1:10-13