Kudrive umbali mrefu

Kudrive umbali mrefu

Dar to Mwanza, zaid kidogo ya km 1000.. kama ni mara yako ya kwanza naomba fanya yafuatayo.. ukiacha usalama wa chombo.

1. Pata usingizi wa kutosha kabla ya safari

2. Vunja safari katikati... ni vizuri ukalala Singida

3. Usikubali kwa namna yeyote kushawishiwa kuendesha gari usiku ukiwa umechoka

4. Usikubali ku overtake bila tahadahari ya kutosha.

5. Nenda taratibu, max 100km/hr..

6.Beba carton ya maji makubwa na uyanywe taratibu.

7. Macho kwenye sahani ... angalia taa zote za tahadhari, usikubal hata moja iwake, na ikiwaka paki pembeni kwenye usalama tafuta fundi.

8. Fuata alama za barabarani...

9. Usiendeshe kwa hofu ya maaskari barabarani, wapo kwa usalama wako

10.Mwisho na sio kwa umuhimu, Sali kabla ya safari, Mungu akutangulie.

Hapa umesomeka
 
We andaa pesa tu ya kulipa faini au kuhonga huko barabarani. Wale jamaa hawakwepeki.

Kisha kuwa makini sana na mabasi, hao watu Wana fujo sana kwa magari madogo.
Piga hata ka-redbull kukukeep alert.
 
Mimi route yangu ndefu kusafiri na private car ni Dar - Songea - Mbinga ila nilivunja safari katikati nikalala Tunduru (nilipita njia ya Lindi). It was the best experience ever!
 
1. Hakikisha unafanya service ya engine.
2. Hakikisha unakua na spare tyre.
3. Hakikisha unakua na wheels spaner, Jeki, Pembe tatu, fire extinguisher.
4. Hakikisha gari ina bima na kadi ya ukaguzi.
5. Kutoka Dar to Morogoro jitahidi kua makini sana kwasababu kidogo lami imejisokota na kuna tochi nyingi pia kua makini na magari makubwa yanayo paki karibu na barabara hasa kuanzia Chalinze, Gairo na Dumila.
6. Ukisigea Pandambili to Kibaigwa pale tembea mwendo wa haja wala usiwe na shaka.
7. Kutoka Kibaigwa hadi Chamwino barabara ipo vizuri ila kua makini pale Mtanana karibu na Nako hua kuna Trafic wanaweka kizuizi cha kizushi nabhawaeleweki wale, lakini barabara ipo njema hadi unaingia Dodoma.
Kibaigwa hadi chamwino kuna sehemu inaitwa Manchali, kuna rasta zinazoweza kuharibu gari!!.

Mtumba mpaka Ihumwa kuna upanuzi wa barabara, ujenzi huo umefanya njia iwe nyembamba sana.
 
Back
Top Bottom