PreGE2025 Kudukuliwa kwetu imekuwa kituko Kenya, wanasema polisi wameweza kuzuia akina Martha udukuzi umewashindaje?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
hata marekani walidukuliwa sembuse tanzania!?
Polisi wetu ni miguvu tu akili haina, wengi ni form 4 failure haishangazi wao kudukuliwa!
SA100 mwenyewe naye form 4 alilamba zero, we msikilize kwenye speech zake akiwa hasomi vikaratasi utaona jinsi alivyo 'white' kuchwani!
 
Hahahaaaa mkuu ndiyo watu wajue tuna tatizo kubwa. Mtu anasema bila aibu mbona USA kadukuliwa yaani alivyo ZEZETA anaona kwa sababu USA kadukuliwa Basi ni sahihi na sisi kudukuliwa. Tanzania yetu tuna changamoto sana.
Tatizo la exposure na mfumo duni wa Elimu, ndiyo matokeoyake haya.
 
Polisi wetu ni miguvu tu akili haina, wengi ni form 4 failure haishangazi wao kudukuliwa!
SA100 mwenyewe naye form 4 alilamba zero, we msikilize kwenye speech zake akiwa hasomi vikaratasi utaona jinsi alivyo 'white' kuchwani!
tatizo ni kubwa sana, kuja kurudi kwenye mstari itachukuwa muda mrefu sana. ku catch up na majirani zetu wenda ikachukua kitambo kidodogo.
 
Hii ni ile vita ya uchumi aliyokuwa anaongelea Magufuli. Tanzania ikivurugika, Kenya itafaidika sana kiuchumi. Ndiyo maana Wakenya wako mstari wa mbele kuchochea moto wa siasa Tanzania. Maana Tanzania ikivurugika, watalii wetu watahamia Kenya, wawekezaji wetu watakimbilia Kenya, mizigo inayopitia bandari ya Dar kwenda nchi jirani itahamia Mombasa, na mengine mengi.
 
PoliCCM have now turned a laughing stock.
 
hata marekani walidukuliwa sembuse tanzania!?
Duuu! Achana na mawazo ya hivi. Maana yake huwezi kujishughulisha kabisa Kwasababu na fulani ni masikini. Ama utasema Fulani ameibiwa hela kwenye mfuko wake hivyo na wewe ukiibiwa sawa tu. Ama waweza sema mzazi wa Fulani akivunjiwa heshima basi na mzazi wako akivunjiwa heshima mbela ya kadamnasi ni sawa tu. Badilika! Badilika! Badilika kifikra.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…