Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...


No, wait a minute Pasco, Ina maana mpo mnaojua au mliokwisha iona draft ya Katiba mpya?
Suppose wabara wakadai nchi yao? Watu tusipokuwa makini hapa hili litasababisha pata shika. Hivi Pasco, unavyosema hivyo una maanisha kuwa kwako wewe uwiano uliopo wa idadi ya wananchi Tanzania bara na Zanzibar ni haki kwa watu wa bara kuwa wanaamuliwa uongozi wa nchi na wachache Zanzibar milele bila ukomo?. Sasa nimeamini 100% kuwa jinsi muungano ulivyoundwa upo kwa ajili ya kudhoofisha na kuua upinzani kutoka pande zote na kwamba hapatatokea upinzani kuchukua uongozi wa nchi. Na hapa ndiyo inathibitika wazi sababu zinazopelekea CCM kutamka kila mara kuwa watatawala milele. Na bila shaka sasa ni wakati kabisa wa kuuweka huu muungano uwe wa sayari hii, au serikali moja nchi nzima au serikali tatu. Hakuna kitakachokuwa sahihi nje ya hapo.
 
Once a dreamer, always a dreamer!, Pasco wa jf is a dreamer and his dreams will come true!. Mark my words, my my dreams!. Please keep records of these dates na tutakumbushana humu humu!. Uchaguzi ni Jumapili October 25, 2015!. Matokeo ya urais ni Ijumaa 30 October 2015!. Rais mpya ataapishwa Saa 6 kamili mchana, Jumamosi October 31, 2015!, Subiria ni nani, wa chama gani na kwanini!.
 
Mkuu MpendaTz, hakuna aliyeona draft ya katiba mpya bali nakufunulia tuu kama Ufunuo wa Yohana!. Muungano wetu ni wa nchi mbili zenye haki sawa. Usawa huu hauko based in idadi ya watu, hata kama Bara wako 99 na Zanzibar yuko mmoja tuu, rais ajaye wa Tanzania atakuwa rais tuu baada ya kupata kura 51% majority ya pande zote za muungano, chini ya hapo ni re-run au serikali ya mseto!.
 
Nimeupenda ujasiri wako wa Ufunuo wa Yohana. Ni jambo zuri tunaonyeshana tunakoelekea. Asante sana.
 
Mkuu Mpenda TZ, muungano wetu ni wa ndoa kamili na sio wa uwiano. Kama ilivyo ndoa, mkiingia kwenye ndoa, mali zote za baba alizochuma kabla ya kuoa zinageuka family joint properties. Hata kama baba ndie bread winner na mke ni goli kipa tuu akisubiri kudaka mipira, siku ndoa ikivunjika, mnagawana kila kitu pasu kwa pasu!, haijalishi mama amecontribute nini!. Hivi ndivyo itakavyokuwa katiba mpya, itafanya restoration ya Zanzibar as equal partner kwenye ubia wa muungano na chama kitakachopata sifa ya kutawala, ni kile tuu kitakachopata kura angalau theluthi moja toka kila upande!. Mpaka sasa sijaziona juhudi zozote za Chadema kutafuta kura za Wazanzibari, or I might be too blind to see!.
P.
 
Well said
 
Ni kama kweli lkn 2subis 2one
 
Ni kama kweli lkn 2subis 2one
Sisi wengine hatuna subira, ni tunaendelea kutembeza bakora mtindo mmoja!, hatutaki na 2015 tuje kuliliwa tena kama 2010!. Tunawapitisha Chadema kwenye tanuru la moto!.
P.
 
Mkuu Pasco, point yako inaweza kueleweka na wenye elimu kuanzia dr. na kuendelea. kwa kuwa ni kweli kabisa kuwa watu hao wapo wachache sana hapa tanzania, ukweli huu ulioufafanua kwa kirefu sana unakuwa si msaada kwenye ukombozi wa taifa letu ADHIMU.

Takwimu ulizoweka kwa sisi tulioko kijijini ni kama unatutisha, akili yetu haina uwezo wa kupambana kikamilifu na milinganyo, ingawa takwimu zako zinaungana nami kimantiki kuwa "ADUI YETU NI CCM" na ombi langu bado lipo pale pale "unikubalie japo mara hii tafadhali"

naamini makubaliano yaliyofikiwa na cuf na ccm haikuwa dhidi ya chadema, bali ni mbinu ya kuidhoofisha cuf, chadema, kwa kuzingatia uelewa wa wananchi, inaweza kufanya kosa kubwa kuingia makubaliano na cuf, chama ambacho kwa sasa kimeonekana kuwasaliti wananchi kutokana na MOU yao na ccm, na wananchi wameishi kuiona methali "ukitembea na mwizi nawe utakuwa mwizi" ikiiishi.

busara hielekezi kufungwa na uelewa kuwa wapiga kura milioni nane na ushee ndio pekee watatakiwa kutupatia rais 2012, badala yake wale 12,000,000 ambao kwa sababu ulizoziainisha ndiyo haswaa walengwa wakihamasishwa, ccm itakuwa chama kikuu cha upinzani.

ahadi (hongo) waliyopewa cuf na ccm si ya kupambana nayo, chadema isifuate njia ya mpinzani wake, kwani unaweza kukuta umetegewa mabomu ya kujitoa muhanga. kwa mbaaaaali picha ya zitto ni kielelezo hapa.

kwa wale wote walio na hamu ya ndoto kuwa kweli niwashauri watafakari sana, mfano ukiota umeokota gunia la hela kwa mazingira ya sasa, ukiondoa muujiza wa mungu, nani anaweza kutupa gunia la hela wewe uokote?

HII SIOTI BALI CCM WATAGARAGAZWA VIBAYA NA CHADEMA COME 2015 NA MAFISADI WATALIA NA KUSAGA MENO, MANAKE WATATAKIWA KUTOA HESABU YA MALI ZAO SAWA SAWA NA KAZI WALIZOZIFANYA.
 
Last edited by a moderator:
Nimekuwa nikifuatilia matokeo ya udiwani ambapo Chadema imeshinda viti 5 kati ya 29. Japo ushindi ni ushindi, kwa pace hii na time factor iliyobakia kabla ya 2015!, tukubali, tukatae, safari bado ni ndefu!. Chadema, yatumieni Matokea haya kama MTR yenu ya M4C!.
P.
 
S i rahisi chama cha upinzani kuingia madarakani kwa sababu inategemea sana pepo za msimu. mizizi yake bado haijakomaa kiasi cha kuhimili kimbunga cha cha CCM 2015 bado ndani yao wanalumbana wenyewe na hata kufikia hatua waandamizi wao kuwafagilia hadharani viongozi wa CCM, udini umeitesa sana M4C kwa mtaji wa Dr WS ambaye aliungwa mkono sana na Maaskofu japo alikuwa hasimu wao wakati akiwa na wao, walimuunga mkono tu kwa sababu walikosa mwelekeo pamoja na ubovu wake wakaona ana unafuu kuliko wengine. Udini wa M4C ukaunda udini mwingine wa CUF kuiunga mkono CCM ili kuiua M4C imeungwa mkono na wakristo bila kujari kiongozi anafaa au hafai. Chadema hawana mbadala kwa sasa mbali na Dr Ws ambaye anaweza kuungwa mkono na Wakristo na akaungwa mkono na Waislamu. Hapa lazima Maaskofu wataandaa Mtu aliye Mkristo lakini anakubalika na Waislamu walioko ndani ya CCM na anayekubalika kwa Watanzania Wengi kwa misimamo yake kwa saabu ndani ya CCM wamo wanaokubalika kwa wananchi Ili CCM isife kwa maana kufa kwake kutakuwa kiama kwa mafisadi wote, CCM itapata mashiko makubwa ya kuungwa mkono na mafisadi hayo kwa hali na mali ili kumnadi huyo anayekubalika wakiamini zimwi likujialo halikuli likakumaliza kwa mtaji huo M4C watabaki kama watoto yatima na hapa naweza kutabili kwamba hata viti vyao ndani ya Bunge vitapungua badala ya ilivyo sasa. hivyo adui upinzani utaitegemea sana katiba ijayo na misimano inayoshika kasi ya udini na ukabila.
 
mm wanachonikera chadema ni udini na ukabila, asilimia nyingi ya sisi vijana tulipoona CUF imeshindwa kuing'oa CCM kwa muda hapa bara tulihisi CHADEMA imekuja na nguvu ya ziada na baada ya wengi wetu kuifatilia tumegundua ina ukiristo uliopitiliza na uchaga mnooo, njia pekee ya kung'oa hawa wahuni ni kwa CUF, NCCR na CHADEMA kuungana bara na zanzibar na kukubaliana kuwa either lipumba au slaa mmoja atakuwa raisi na mwingine makamu wa raisi na yule wa NCCR kuwa waziri mkuu, nd kule Znz aende Seif sharif na Mbowe, mm naamini kwa hilo kufanyika udini na ukabila utapungua, na itarudisha upendo baina yetu na bila shaka CCM wataanguka
 
Mtu mmoja anasema hivi :'UCHAGUZI WA MAREKANI DARASA KWA WATANZANIA' umefika wakati wa watanzania kukataa kabisa kuchagua chama chochote kinacho hubiri ukanda au udini,navyo viko wazi CUF,uislam kwanza, CHDM,usisi,umimi
mbunge1 amedai uhuru wa eneo fulani ndani ya TZ! Sisiem nayo Tumbo langu kwanza. kumbe chama si swala la kuzingatia sana,ila yule anayekuomba kura jiulize anataka kura yako kwa udi kwenda hapo kwaninî? then utafanya uamuzi mzuri.not chdm,cuf,uddp,tlp,nor ccm.Godbless Africa,Godbless T
 
Wanabodi,
Ushauri huu niliutoa 2012, UKAWA imezaliwa kwa convenience ya katiba tuu, baada ya hapo its dead!, ushauri wangu huu bado ni very valid, naanza kuukumbushia kidogo kidogo kadri 2015 inavyokaribia, ili baada ya 2015, nifanye stock taking, walishauriwa nini, walifanya nini, walipuuza nini na matokeo ni nini!.

Pasco.
 
Kwa takwimu hizo hatupaswi kuwalaumu watanzania ati wanawaweka ccm madarakani hii naikataa kwa sababu 2 kwanza ni watanzania chini ya 50% ambao wamepiga kura 2. Wizi wa kura mkubwa uliokithiri tena wa kibabe, labda tulaumiane kwa nini tukubali wizi huu na matokeo haya???? sasa tufanyeje...........????????
 
Wanabodi, naendelea kufanya tafakuri rejea ndogo ndogo kwenye baadhi ya threads zangu nilisema nini kuhusu safari ya kuelekea 2015, hiyo 2015 sasa ndio hii, nafanya MTR ni kipi kimefanyika hadi sasa, ili ikitokea Chadema ikashindwa tena kuchukua nchi hapo October, 2015, itakuwa imeshindwa kwa mambo ya kijinga jinga, kuendekeza ujinga ujinga na udikiteta wa hapa na pake kwa kudhani itasaidia kumbe inawabomoa!.

Pasco
 
Kuna mtu aliwahi kupata au kusikia mrejesho wowote wa hii M4C?.

Pasco
 
Baadhi ya hoja hizi ziko take care of ndani ya UKAWA.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…