Mkuu BAK, kusema ukweli, nimecheka baada ya kuisoma posti yako hii, maana ndio kwanza nimemaliza kuisoma post ya Nico, amepiga nyundo za kufa mtu, kufumba kufumbua, nimecheka kwa sababu kumbe kuna ma great thinkers humu wanadhani
namfagilia EL ili nipate chochote?.
- Kwa taarifa tuu, baada ya Mwl. Nyerere kustaafu, nimemfanyia kazi pale MNF na ni mimi ndie niliyefanya recording yake ya ziara yake ya mwisho nchini kwenye kambi za wakimbizi.Ni mimi ndie niliesafiri nae ule mkutano wake wa mwisho nchini Uswis na hizo footage ndizo the last akiwa on duty, tuliporudi ndipo alianza kuugua!Kwenye familiy level, nimesoma na mwanae mmoja na nilikuwa MC wa harusi ya bintie, hivyo closeness hiyo ingeni guarantee nimuombe anipigie chapuo lolote popote, nipate kijiposti chochote ili nisife njaa.
- Kipindi cha Mwinyi nilikuwa on-off on- off ila kama ni kutaka ulaji, ningelobby nisingekosa chochote!.
- Ben, kijana wake shule moja darasa moja na alipokuja NY nilipelekwa rasmi Presidential Suite kuwa introduced, hivyo kama ni lobbying, ningelobby niwe anybody!.
- Kijana wa JK is a friend tangu pale UD, kabla hata hajaukwaa up presidaa, mahali JK alipotangazia nia kwa mara ya kwanza ni UD, master mind yule yule kijana ambaye sasa ndie master mind wa Membe. Hivi kweli kama nia yangu ni hii njaa ya kupitiliza inayonikabili, kweli ningeshindwa kwenda kwa kijana kumlilia shida angalau na mimi nitoke!.
- Kama nilikuwa na connections tangu Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na sasa JK, nili lobby chochote, why should i fight for EL ili kuja kuwa anybody?!.
Kuna watu hawaamini kuwa kuna kundi fulani la watu, sisi ni masikini jeuri, yaani tumeuzoea umasikini mpaka kufikia point, tumejiridhisha kuwa umasikini wetu ndicho tulichopangiwa na Mungu ana unaupokea kwa moyo mkunjufu huku ukiwafurahia matajiri kwa utajiri wao Mungu aliowajalia na ndio maana siku zote, huwa nawapiga vita sana hawa hate preachers wetu humu jf kwa kuumwa na roho za chuki, vivu na husda, kwa kila mwenye kautajiri hata kadogo tuu!.
Kwa ufano, usafiri wangu wa siku zote kwenye carrear yangu as a journalist ni boda boda!, usafiri huo ndio nimekuwa nikiutumia siku zote na kwenda nao popote!. Nilishaonywa sana kuhusu hatari za usafiri wa kimasikini hivyo kwa mizunguko yangu sikusikia, siku ya siku, yalinikuta, japo kwa sasa siwezi kuendelea kuendesha boda boda, lakini boda boda yangu nimeipark pale mbele ya kibanda nilichopanga na marafiki zangu wengi wanatamani niwauzie, nimegoma kuiza smply because usafiri wa kimasikini wa boda boda, sio tuu ndio ninaoupenda for convenience, bali ndio most affordable mode of transport kwa sisi watu wa hali ya chini!.
Kwenye CCM nampigania EL kwa nguvu zangu zote kwa sababu naamini ni kwa kupitia yeye, Tanzania itapata ule ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania na pia ili litimie lile neno kuwa "rais wa 2015" lazima atatoke Kaskazini.
Pasco.