Inaniwia vigumu kila nikitazama safu ya Chadema kumpata wa kumliganisha uzito na huyu bingwa wa uzito wa juu katika medani za siasa ya Tanzania.
Nashindwa kupata jibu ni mwana siasa yupi ndani ya chadema ambae atasimama haswa na kuwakinaisha Watanzania wamchaguwe badala ya Lowassa iwapo ataamuwa kugombea kiti cha Urais Tanzania?
Maana najuwa Mbowe hana hamu tena baada ya kugaragazwa vibaya sana na Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2005.
Slaa nae choka mbaya, hana jipya zaidi ya majungu na siasa zisizo na mpango, hata ujumbe kwa Mwema ni ushahidi tosha kuwa kaishiwa kisiasa.
Nilidhani Zitto ataweza kwa kuwa ni damu changa lakini napata mashaka kuwa siasa za ukanda za chadema zitampa fursa ya kugombea, dalili zote zinaonesha chadema wa kanda ya kaskazini hawamtaki kabisa. Kwa hiyo huyu nnamtoa kwenye kinyan'ganyiro.
Shibuda hata akipitishwa kugombea akiambiwa Lowassa anagombea atakataa kuchuana nae.
Ka Mnyika, haka bado sana, hata ubungo inamshinda na sijui kama atashinda tena hata akigombea Ubunge huko. Kwishnei.
Halima Mdee, huyu hana ubavu, huyu akisikia Lowassa anagombea labda ajitafutie umaarufu tu - kwa hiyo huyu nje.
Nani mwingine?
Natamani Lowassa atangaze mapema kugombea 2015 angalau chadema waanze kujitayarisha mapema na mgombea ambae uchaguzi hautokuwa boring, maana hao wote juu Lowassa atawaonea tu.
CCM inatisha.