zomba usihangaike sana ukapoteza nguvu zako iko hivi CDM ni chama kizuri sana cha upinzani lkn ukweli bado muda wa sisi kukipa madaraka makubwa. kimsingi nakuambia Lowassa ndiye mtu anayeweza kutawala chi hii ukilinganisha na cv za wengine wote ambao wanajiita wanasiasa mashuhuri
ha ha ha mzee uko kwenye payroll ya Fred Lowasa nini?
Wanabodi,
Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimekubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai yuko fit, japo he looks sick), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, them matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali, mkatae!.
Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena, endapo and only if itamsimamisha Lowassa!.
1. Uwezo wa Kupanga, Kusema, Kusimamia na Kutenda.
Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kupanga wa kusema tuu, (Mkukuta, Mkumbita, Mkurabita, Mkuza, na sasa Dira 2025), lakini hawana uwezo wa kusimamia na kutenda!, mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na vitendo sifuri!. Edward Lowassa sio msemaji, bali ni mtendaji, yeye sio mtu wa maneno mingi, ni mtu wa vitendo virefu, he is an action oriented man!.
Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Elimu, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile mising minne tulisahau capital!.
Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo la siasa safi na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Elimu ni adui, lakini we never invested because we had no capital. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana na IMF, WB etc matokeo tunayajua!.
Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, akafanya study tour ya tulioanza nao kwanini wao wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha nyuma sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!.
Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu, tumeibiwa madini kwa sababu hatuna elimu ya madini, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu elimu ya gesi, kwa kifupi, hutujui lolote na tutaishia kuibiwa tena gesi yetu kwa kukosa elimu ya gesi!. EL ameshauri, lets invest kwenye elimu kwanza ili kuwa empower watu wetu kielimu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kilimo kwanza gesi etc!.
Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.
Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayewa kusimama na Lowassa kwenye urais na bado akaambulia kura!, there is none, no one!.
Mwenye masikio na asikie!.
2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.
Najua wapinzani wa dhana ya ukweli, watakuja na hoja za dhambi kubwa ya Lowassa ni Richmond!, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipa Simbion capacity charge ile ile ya dola 152 kama Richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanyaga moto, tumeruka maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.
3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hana wa Kushindana Nae!.
Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli CCM itamsimamisha, then, 2015, ni CCM tena, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yoyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulaini kama kumsukuma mlevi!.
Mwisho.
Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali huu ukweli mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa? au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa kutegemea katiba mpya ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.
Asante.
Pasco.
NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.
Mkuu wacha kubabaika na huyo fisadi, kama amekutuma kampigia debe basi ameisha shindwa kabla mbio hazijaanza!!! Kama CCM watamweka huyo kama mgombea basi kazi ya CHADEMA itakuwa nyepesi saana, pole ndugu yangu huyo hauziki!!!
Mkuu Zomba, nilipokuwa nakusoma nilikudhania wewe ni mwelewa!. Ina maana mpaka leo bado hujaelewa sababu za kujiuzulu kwa EL?!. Hivi hujanote jinsi serikali ya JK ilivyo pwaya baada ka kujiuzulu huyu jamaa?. Hivi hujui yeye ndiye mkombozi pekee anayeweza kuunusuru CCM 2015, vinginevyo CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukua nchi kiulaini kama kumsukumiza mlevi?.Umefikishwa wapi? mwandishi wa habari huwa haongei udaku, ongea ujulikane unachokisema, una maana Lowassa asingestaafu?
Mkuu Fugwe, baeleze baelewe!.Wana JF, Sasa yupi bora kati ya Mtu mwema na mwadilifu, asiyejua kuchukua cha mtu lakini hawezi kukemea wezi wa mali ya umma wanaoiba mchana kweupe na vingine wanadodndoshea miguuni pake na wala aiyewezi kupanga wala kusimamia mkakati ya maendeleo na mtu mwingine tunayesema ni mwizi lakini anauwezo wa kupanga na kusimamia mipango ya maendeleo lkn wizi wake ana-invest humu humu nchini??? niambieni yupi bora?????? KURA YANGU NAMPA EL
Mkuu Zomba, nilipokuwa nakusoma nilikudhania wewe ni mwelewa!. Ina maana mpaka leo bado hujaelewa sababu za kujiuzulu kwa EL?!. Hivi hujanote jinsi serikali ya JK ilivyo pwaya baada ka kujiuzulu huyu jamaa?. Hivi hujui yeye ndiye mkombozi pekee anayeweza kuunusuru CCM 2015, vinginevyo CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukua nchi kiulaini kama kumsukumiza mlevi?.
Utasemaje hivyo wakati kina Kiranga wameonyesha udhaifu wa siasa za kujadili watu badala ya itikadi kitambo tu?
Utasemaje hivyo wakati watu tushaongea humu kwamba the very label "Ujamaa na Kujitegemea" carries within itself an inherent oxymoronic contradiction if at all you value the individual as the well and litmus test of ideologies?
Mkuu Ngongo, sio tuu lisingelipwa mkataba tungevunja na mitambo tungetsifisha!. Hiyo capacity charge tuu tunayowalipa, ilishatosha zamani kununua mitambo mipya, wala kusingekuwepo na hii Simbion!. Tatizo mhusika mkuu ni muzeiye na ndivyo walivyokubaliana kwenye secret code yao! "Scratch my back, I'll scratch yours!". The only thing that will stop him is his ill heathy na atahamishia majeshi yake kwa Membe.Mkuu Pasco ni kweli Laigwanani ni mchapakazi kama angekuwa bado yuko serekalini hata hili deni la RICHMOND lisingelipwa ha ha ha ha.
Mkuu Zomba, nilipokuwa nakusoma nilikudhania wewe ni mwelewa!. Ina maana mpaka leo bado hujaelewa sababu za kujiuzulu kwa EL?!. Hivi hujanote jinsi serikali ya JK ilivyo pwaya baada ka kujiuzulu huyu jamaa?. Hivi hujui yeye ndiye mkombozi pekee anayeweza kuunusuru CCM 2015, vinginevyo CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukua nchi kiulaini kama kumsukumiza mlevi?.
Mkuu Mchambuzi, with due respect,Upo sahihi Mkuu,
Nilitamka hayo kwa sababu nimeona kuna mwenendo wa wachangiaji wengi humu kukimbilia threads zinazojadili watu badala ya masuala, lakini ni dhahiri wapo wengine wengi ambao hawapo katika kundi hilo, wewe ukiwa mmoja wapo kwani nimekuwa nakusoma sana;
Unakuta mtu anakuja na thread ya mgombea kipenzi chake na kuanza kutulazimisha kwamba hawezekaniki kwa hoja za ovyo ovyo tu na zilizojaa ushabiki na ubabe kwa sababu wanayo dola kwa hivi sasa badala ya kujenga hoja za msingi kwani pengine hilo lingeweza kushawishi watu wengi waunge mkono hoja hizo au wagombea wao lakini badala yake wanazidi kuwaharibia aidha kwa kujua au kutojua; Na cha kushangaza zaidi, unakuta watu zaidi ya mia wakishiriki mijadala ya ovyo kama hiyo ambayo literally inawapa more room waleta hoja za ovyo ovyo kama kuzidi kutuambukiza siasa za WATU vis-a-vis MASUALA, siasa ambazo wao wamekuwa ni mabingwa hasa kwa kuchafua wenzao; Vinginevyo kuna mijadala mingi sana muhimu kwa taifa letu kama vile ya katiba mpya, muungano n.k, lakini unakuta ushiriki wa watu katika mijadala ya namna hii sio ya kurudisha;
Ni hayo tu mkuu lakini ujumbe wako nina hakika wengi wanauelewa;
Mimi huwa natatizwa sana na fikra za kufikiria Ukombozi wa Mtanzania kwa kufuata vitabu vya wale walonacho wanatazama nini..Huwezi kusema kosa pekee la Nyerere lilikuwa kutofuata misingi ya ukweli kwa sababu Adam Smith kasema haya wakati hailingani na mazingira wala Mantiki ya Mtanzania. Hivi kweli wewe unategemea mtu maskini, Mjinga na mwenye maradhi ataweza vipi kuzungumzia CAPITAL ikiwa hata kula yake mwenyewe ni shida.. Au nambie yule ombaomba unayemuona Mtaani unaweza vipi kumshauri ili atoke ktk Umaskini wa kutembea na kopo maana ukisema atafute Capital utakuwa unamtukana.Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Elimu, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile mising minne tulisahau capital!.
Mkuu Mchambuzi, with due respect,
kwani Watanzania huwa wanachagua nini?. Wanachagua sera, hoja au mtu?. Kwani JK alichaguliwa kwa lipi?. Ninachofanya mimi ni kuwapa mwanga wa kitakachotokea 2015, Watanzania hawachagui sera wala hawasikilizi hoja, wao wanachagua mtu tena kwa kumuangalia sura!.
Nilipokuwa mtaani nilidhani wasomaji wakuu wa magazeti pendwa ni wale std 7 na school drop outs, nilipokuwa UD sikuamini magazeti hayo ndio choice no. 1 kwa wanafunzi wa chuo sasa nimeichukulia hiyo ndio sampling ya Watanzania!.
Kwa sisi waandishi big names makes big news, EL ndie the biggest name in Tanzania politics akisimama, hakuna wa kusimama nae!.
Japo jf is ment to be the home of great thinkers ambao wana discuss ideas, ordinary mind pia wapo wanao discuss events na sisi simple mind pia tupo ambao tuna discuss people!.
Great minds, ordinary minds na simple minds all together tukubali tukatae the name EL is the determinant factor nani anakuwa the next president wa nchi yetu come 2015!.
Wenzetu ma great thinkers endeleeni kupandisha threads za ideas, huku ma ordinary wakiendelea kutuhabarisha trends of events na sisi ma simple minds tukiendelea kuwatajieni watu posible wa kuchukua nchi 2015!. Pasco.
Hakuna anayebisha kuhusu "WANATOKEA", kilicho relevant katika discussion yangu ni Wanaoishi kule kama wapiga kura; Vinginevyo KUTOKEA sehemu sio kigezo, kwani wapo watu ambao wanajua wametokea kwenye matumbo ya mama zao lakini hawana heshima kwa wanawake, wengine hata mama zao wazazi;