Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,717
Mpaka sasa kuna kila
dalili kuwa mgombea urais wa CCM 2015 huenda akawa Edward Lowassa
kutokana na nguvu ya kisiasa aliyonayo ndani ya CCM kwa sasa hususani
kwa wajumbe wengi wa vikao vikuu vya juu vya maamuzi ndani ya CCM(Kamati
kuu, Halmashauri kuu na Mkutano Mkuu).
Wakati huo huo kama kuna jambo wanachama wa CHADEMA wangependa kuliona
basi ni Lowassa kuwa mgombea urais wa CCM 2015.
Kwa sababu zifuatazo:
1/Moja ya hoja zilizoipa nguvu sana na Umaarufu mkubwa sana CHADEMA ni
Vita dhidi ya Ufisadi, Lowassa ni mtu anaaminiwa kama fisadi zaidi
kuwahi kutokea ndani ya CCM, hivyo kutaipa nguvu zaidi CHADEMA katika
harakati zao.
2/Kumbukumbu isiyofutika ya kitendo cha Lowassa kujiuzuru uwaziri mkuu
kutokana na kuhusika katika Ufisadi mkubwa wa mkataba tata wa kampuni ya
kufua Umeme wa dharura(Richmond).
3/Vita ya kufa na kupona kati ya Lowassa dhidi ya makundi mengine ya
wanaCCM wenzie wanaoutaka urais pia, ambao wamekuwa kila mara
wakianikana baadhi ya maovu yao hadharani. Katika hili atakosa 'Support'
muhimu kutoka kwa wanaCCM wengine 'muhimu' wanaomchukia.
mkuu,
sio kwamba EL hafai bali ukweli ni kwamba mpaka sasa wanaccm wote wanaoutaka uraisi hawafai!
Wote waliojitokeza kuwania uraisi hawafai, wanaofaa hawajajitokeza