Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Mpaka sasa kuna kila
dalili kuwa mgombea urais wa CCM 2015 huenda akawa Edward Lowassa
kutokana na nguvu ya kisiasa aliyonayo ndani ya CCM kwa sasa hususani
kwa wajumbe wengi wa vikao vikuu vya juu vya maamuzi ndani ya CCM(Kamati
kuu, Halmashauri kuu na Mkutano Mkuu).
Wakati huo huo kama kuna jambo wanachama wa CHADEMA wangependa kuliona
basi ni Lowassa kuwa mgombea urais wa CCM 2015.
Kwa sababu zifuatazo:

1/Moja ya hoja zilizoipa nguvu sana na Umaarufu mkubwa sana CHADEMA ni
Vita dhidi ya Ufisadi, Lowassa ni mtu anaaminiwa kama fisadi zaidi
kuwahi kutokea ndani ya CCM, hivyo kutaipa nguvu zaidi CHADEMA katika
harakati zao.

2/Kumbukumbu isiyofutika ya kitendo cha Lowassa kujiuzuru uwaziri mkuu
kutokana na kuhusika katika Ufisadi mkubwa wa mkataba tata wa kampuni ya
kufua Umeme wa dharura(Richmond).

3/Vita ya kufa na kupona kati ya Lowassa dhidi ya makundi mengine ya
wanaCCM wenzie wanaoutaka urais pia, ambao wamekuwa kila mara
wakianikana baadhi ya maovu yao hadharani. Katika hili atakosa 'Support'
muhimu kutoka kwa wanaCCM wengine 'muhimu' wanaomchukia.

mkuu,
sio kwamba EL hafai bali ukweli ni kwamba mpaka sasa wanaccm wote wanaoutaka uraisi hawafai!
Wote waliojitokeza kuwania uraisi hawafai, wanaofaa hawajajitokeza
 
mkuu,
sio kwamba EL hafai bali ukweli ni kwamba mpaka sasa wanaccm wote wanaoutaka uraisi hawafai!
Wote waliojitokeza kuwania uraisi hawafai, wanaofaa hawajajitokeza

Sio kwamba wanaofaa hawajajitokeza bali hawajazaliwa na kama wamezaliwa basi walishakufa(mf,sokoine)
 
Tumekusikia ndugu kuwa wewe humtaki Lowassa. Tueleze wewe unadhani ni nani akipitishwa na CCM itapata ushindi wa kishindo.
 
Sio kwamba wanaofaa hawajajitokeza bali hawajazaliwa na kama wamezaliwa basi walishakufa(mf,sokoine)

mnaota ndoto moja kwa pamoja... Wakuu sio wote wanaojazana kwenye mikutano ya chadema watakipigia kura, wengine wanaenda tu kushaangaa ile ndege yenu ndogo
 
lowasa1.jpg

Hawa ndiyo wanakaopokezana vijiti.

Cc; Pasco,
 
Last edited by a moderator:
mkuu,
sio kwamba EL hafai bali ukweli ni kwamba mpaka sasa wanaccm wote wanaoutaka uraisi hawafai!
Wote waliojitokeza kuwania uraisi hawafai, wanaofaa hawajajitokeza

ccm ina kawaida ya kumpata mgombea urais ambaye anakubalika na watanzania wengi. tulieni maana Rais ajaye atakubalika na watu wengi ndani na nje ya ccm
 
Tanzania wanaopiga kura ni UWT. Ndio wenye maamuzi nani awe Rais, nchi ya ajabu sana hii.
 
Tumekusikia ndugu kuwa wewe
humtaki Lowassa. Tueleze wewe unadhani ni nani akipitishwa na CCM
itapata ushindi wa kishindo.

msianze kumjadili na kumshinikiza ili ataje anayemtaka. yeye ametahadhalisha tu hatari ya ccm kumsimamisha lowasa
 
Tanzania wanaopiga kura ni UWT. Ndio wenye maamuzi nani awe Rais, nchi ya ajabu sana hii.

una maana gani mkuu? yaani Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) pekee ndo wenye mamlaka ya kumteua Rais?
 
Tumekusikia ndugu kuwa wewe humtaki Lowassa. Tueleze wewe unadhani ni nani akipitishwa na CCM itapata ushindi wa kishindo.

Tata nadhani hujanisoma vizuri na kunielewa.
Hakuna mahali nimesema namtaka au simtaki Lowassa ila nimeonyesha uwezekano wa Lowassa kuwa mgombea Urais wa CCM 2015 na uwezekano wa CHADEMA kutushinda kirahisi.

Hoja yangu sio nani anatufaa wanaCCM ili kuwashinda CHADEMA bali nimetoa tahadhari tu kuwa Mgombea wetu wa urais mtarajiwa(Lowassa) ni dhaifu sana kuweza kupambana kisiasa dhidi ya nguvu na kasi ya sasa ya CHADEMA.

Njia bora kwa chama changu kwa sasa ili kupata mgombea bora ni kuruhusu 'siasa safi' zianze kufanyakazi ndani na nje ya CCM. Kwa njia hiyo labda huenda litawaibua watu wema na wazuri kutaka kugombea urais.
Huenda hata mimi au wewe tukawa tunafaa tu!!
 
Last edited by a moderator:
Nyie fanyeni yenu bhana,muwekeni Sisco,Six au Mende lkn sisi tunachojua ni kwamba 2015 hamna chenu ni kuwazombea tuu magerezani na ningewashauri mjenge magereza mapya kabisa maana haya yaliyopo hayatatosha...
 
mnaota ndoto moja kwa
pamoja... Wakuu sio wote wanaojazana kwenye mikutano ya chadema
watakipigia kura, wengine wanaenda tu kushaangaa ile ndege yenu
ndogo

ni heri mara mia wananchi wanaokuja na kujazana kwenye mikutano kuja kushangaa 'ndege' kuliko wananchi wanaosombwa na malori na kuahidiwa posho ili wahudhurie mikutano
 
Back
Top Bottom