Kuelekea 29 Oktoba 2026: Mbona serikali inaogopa TEC kuwaombea wauaji?

Kuelekea 29 Oktoba 2026: Mbona serikali inaogopa TEC kuwaombea wauaji?

Deus Jovin

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2013
Posts
250
Reaction score
201
1792968937771.png

Mapadre wawili, Stanslaus Muyebe na Alex Muyebe (2001), katika kitabu chao kiitwacho “The African Bishops on Human Rights: A REsource Book,” wanafafanua misimamo thabiti ya Maaskofu Kuhusu wajibu wetu wa kukuza na kuhami haki za binadamu, zikiwemo haki za kidini.

Kuhusu haki za kidini, Muyebe na Muyebe (2001:30-80) wameorodhesha haki saba za taasisi za kidini, bila kujali jina la dini inayowakilishwa na taasisi wala madhehebu husika. Kuna:
  1. Haki ya Kutafuta na Kujua Ukweli (The Right to Seek and Know the Truth );
  2. Haki ya Uhuru wa Kutoa Maoni na Kujieleza (The Right to freedom of Opinion and Expression);
  3. Haki ya Elimu na Fikra Tunduizi (The Right to Education and Critical Thinking);
  4. Haki ya Uhuru wa Kiakademia na Kiitikadi (The Right to Academic and Ideological Freedom );
  5. Haki ya Uhuru wa Dhamiri na Imani ya Ndani (The Right to Freedom of Conscience and Internal Belief);
  6. Haki ya Kuabudu na Kutekeleza Imani (The Right to Worship and Manifest One's Faith); na
  7. Haki ya Uhuru wa Kitaasisi Katika Kujitawala Watakavyo Bila Kusumbuliwa na Mtu Yeyote (The Right to Institutional Autonomy), yaani Uhuru wa Taasisi za kidini kusimamia shule zao, vyombo vyao vya upashani habari, miundo yao ya uongozi, na kazi zao zinazohusu utoaji wa huduma za kijamii bila kuingiliwa na wanasiasa, wanaharakati, mapolisi auwanajeshi.
Kwa sababu hizi saba, tarehe 23 Oktoba 2026, Askofu Wolfgang Pisa, ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), alitoa wito wa kichungaji, ambao unaonekana kuitishia serikali kwa kusababisha hofu inayotetemesha vyombo vya ulinzi na usalama. Hakuna sababu ya kuogopa ukweli.

TEC wanasema kuwa, kwa kutambua haki na wajibu wa taasisi za kidini katika kulitakatifuza Taifa la Wana wa Mungu, Kanisa Katoliki la Tanzania linawaalika Wakatoliki walioko katika jumuiya Kanisa la Mahujaji (Pilgrim Church community) kushiriki katika adhimisho la Misa maalum tarehe 29 Oktoba 2026.

Ni Misa kwa ajili ya kuliombea Taifa kwa kutimiza mwaka moja salama tangu misukosuko ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ambapo baadhi ya watu waliumizwa, kupotea na wengine kuuawa kwa risasi za moto, baadhi wakiwa ndani ya nyumba zao wakiangalia luninga.

Kwa mujibu wa Imani Katoliki, watu wote waliouwawa kwa sasa ni sehemu ya jumuiya ya Kanisa la Toharani (Repentant Church community).

Wako safarini kuelekea mbinguni kwenye jumuiya ya Kanisa la Washindi (Triumphant Church community).

Wakatoliki wote ambao ni sehemu ya jumuiya ya Kanisa la Mahujaji wanatamani kufika huko ili wamwone Mungu, Eliya, Yakobo, na Yesu uso kwa uso.

Huko mbinguni kuna mziwa, asali, shibe na furaha tele. Hakuna njaa, kiu, hasira, chuki, wivu, magonjwa wala kifo.

Kwa mujibu wa Biblia, katika Toleo lemye vitabu 73, wakati jumuiya ya Kanisa la Washindi wanao wajibu wa kuliombea Kanisa la Mahujaji (Warumi 8:34), jumuiya ya Kanisa la Mahujaji wanao wajibu wa kuliombea Kanisa la Toharani (2 Wamakabayo 12:43-46).

Hivyo, Wakatoliki watakusanyika sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya kuomba “umoja, upendo, ukweli, na mshikamano,” ambavyo ni “matunda ya haki na amani.”

Pia, Wakatoliki wataomba “faraja kwa wanaolia, tumaini kwa waliokata tamaa, imani kwa wenye mahangaiko, haki na ukweli kwa waliopotea, busara kwa wasioelewa, uponyaji kwa wenye majeraha na upendo kwa wenye chuki.”

Misa Takatifu zote nchi nzima zitaadhimishwa kwa ajili ya kufanikisha nia nne: faraja kwa walioumizwa, kurejea kwa waliopotea, haki ya waliouawa, na “kuliombea Taifa letu” liondokane na wauaji wa Oktoba 2025 na washirika wao.

Misa hiyo itafanyika kwenye Parokia zote, kwenye vituo vya sala na Taasisi za Kanisa kadiri iwezekanavyo, muda wa asubuhi au muda mwingine wowote unaofaa.

Kwa ujumla, yafaa tukumbuke kuwa, Kanisa Katoliki, kama zilivyo taasisi baki za kidini, wanazo haki zao kikatiba na kisheria.

Haki mojawapo ni kuwapokea wauaji wa OKtoba 2025 ambao ni waumini wao, kusikiliza dhambi walizotenda wakati wa vurugu zile, na hatimaye kuwapatia ondoleo la dhambi, ili wawe na amani ya moyo.

Na haki nyingine ni kutoa elimu ya uraia kuhusu haki za binadamu. Kulingana na Muyebe na Muyebe (2001), katika kitabu chao nilichokitaja hapo juu, Maaskofu wa Afrika, na Maaskofu wa Tanzania wakiwemo, wanapigania haki za binadamu zifuatazo:
  • Haki za Kibayolojia (Biological Rights)
    • Haki ya kuishi, ikiwa inajumuisha mimba, vikongwe, na vifo vya kiholela.
    • Haki ya usalama wa mwili na kuendelea kuishi hapa duniani
    • Haki ya kupata huduma za msingi za afya na matibabu
    • Haki ya kupata chakula cha kutosha, maji safi, na malazi
  • Haki za Kisaikolojia na Kimwili (Psycho-Somatic Rights)
    • Haki ya kuteswa, kunyanyaswa kimwili, na ukatili
    • Haki ya kulindwa dhidi ya kiwewe cha kisaikolojia (trauma), unyanyasaji, na vitisho
    • Haki ya kutendewa kwa utu wakati wa kuzuiliwa au kufungwa gerezani
    • Haki ya ustawi wa akili na usalama wa kihisia
  • Haki za Kiakili na Kiroho (Intellectual-Spiritual Rights)
    • Haki ya uhuru wa dhamiri, mawazo, na mtazamo
    • Haki ya uhuru wa dini, kuabudu, na mazoea ya kiroho
    • Haki ya kupata elimu, kujua kusoma na kuandika, na maendeleo ya kiakili
    • Haki ya utambulisho wa kitamaduni, kujieleza, na kuhifadhi mila
  • Haki za Kisiasa (Political Rights)
    • Haki ya ushiriki wa kiraia na kupiga kura kidemokrasia
    • Haki ya uhuru wa kujieleza, kusema, na uhuru wa vyombo vya habari
    • Haki ya ulinzi sawa chini ya sheria na kupata kesi ya haki
    • Haki ya kukusanyika kwa amani na kushirikiana
    • Haki ya utawala bora, wa haki, na unaowajibika
  • Haki za Kiuchumi (Economic Rights)
    • Haki ya kufanya kazi na kupata fursa sawa za ajira
    • Haki ya kupata mshahara wa kukidhi mahitaji na mazingira ya haki ya kazi
    • Haki ya kumiliki mali binafsi
    • Haki ya maendeleo ya kiuchumi yenye usawa na ugawaji mzuri wa rasilimali
    • Haki ya kulindwa dhidi ya umaskini wa kimfumo na unyonyaji wa kiuchumi
  • Haki za Kijamii (Social Rights)
    • Haki ya kuoa/kuolewa na kuanzisha familia
    • Haki ya usalama wa familia na ulinzi kutoka kwa serikali
    • Haki ya kushiriki katika maisha ya jamii na ushirikiano wa kijamii
    • Haki ya hifadhi ya jamii, ustawi, na mitandao ya usalama wa jamii
  • Haki za Kijinsia (Sexual Rights)
    • Haki ya utu na maadili katika mahusiano ya kijinsia na kingono
    • Haki ya kulindwa dhidi ya unyonyaji wa kingono, unyanyasaji, na biashara ya binadamu
    • Haki ya kuheshimiana na usawa kati ya wanandoa ndani ya mfumo wa ndoa
    • Haki ya kupata mwongozo wa kichungaji na ulinzi kuhusu uzazi wa mpango na maadili ya ngono
Kama ukweli ndio huu, kina Clement Mwandambo, na watu waliowatuma, wanapata wapi ujasiri wa kupayuka na kudai kuwa TEC wanaendesha misa ya wafu kwa sababu Rais SSH ni Mwislamu, na kwamba hawakuendesha misa ya wafu kwa ajii ya wafu wa Zanzibar mwaka 2001 kwa kuwa wakati huo Rais MKapa alikuwa Mkristo?

Nani aliwambia kwamba vifo vya Wazanzibari 2001 vilihusisha waumini Wakristo, hadi Kanisa lipate sababu ya kuendesha misa ya wafy Wakristo?

Na je, nani kawadanganya kwamba Rais SSH ni Muislamu kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo tena kwa 100?

Bila utafiti hauna haki ya kuongea, na akili za kuambiwa changanya na zako!

Nawasilisha.

Tafakari, shirikisha, chukua hatua.

tec02.png
 
Kwakweli atakaye hamasisha uchochezi safari hii naomba asiachwe hai. auwawe, Amani ya nchi ni muhimu kuliko mtu yeyote yule.
 
Kwakweli atakaye hamasisha uchochezi safari hii naomba asiachwe hai. auwawe, Amani ya nchi ni muhimu kuliko mtu yeyote yule.
Wa kwanza awe wewe. Tena upigwe mawe hadharani. Maana ndio mchochezi nambari Moja hapa JF.
 
Back
Top Bottom