Mnyakatari
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 2,073
- 1,862
Ni Jumamosi ya tarehe 3 June 2017 ndiyo siku itakayopigwa fainali ya 25 ya uefa champions league na ya 62 tangu kombe hilo likiitwa Europa Cup.Ni ndani ya Millenium Stadium uliopo mji wa Cardiff nchini Wales.
Hapa tutakuwa tunapeana mambo mbalimbali juu ya ligi hii jinsi inavyoendelea mpaka fainali.Bado tupo hatua ya makundi ambapo mechi moja tu kwa kila timu imesalia kumaliza mzunguko wa makundi zitakazofanyika hapo December 6 na 7.
Ni timu 12 ndizo zimeshafuzu kuingia raundi ya 16 bora ambapo 4 zingine zitajulikana baada ya mechi za mwisho.
Group A
PSG na arsenal zimeshafuzu kundi A.Zote zina points 11 huku PSG ikiwa inaongoza kwa kuwa kwenye head to head PSG wana magoli mengi ya ugenini ingawa mechi zote mbili ilikuwa sare.Ikumbukwe kuwa arsenal ina magoli mengi ya kufunga kuliko PSG lakini H2H inaangaliwa kwanza kwenye uefa kabla ya magoli ya kufunga.Ludogorets na Basel zikiwa na points 2 kila moja zimeshaaga mashindano zimebakia tu kumalizia ratiba.
Group B
Katika group B ni Dynamo kiev pekee ndiyo haina nafasi ya kufuzu au tuseme imeshaaga mashindano hayo.Timu mbili zozote kati ya Napoli,Benfica na Besiktas zina uwezo wa kufuzu itategemea na matokeo ya mwisho ya makundi.
Kund C
Barcelona imeshafuzu hapa na Celtic imeshaaga michuano.Manchester City imeshafuzu pia kwa kuwa head to head yake na M'gladbach inaibeba.Kigezo cha kuangalia kwanza head to head kabla ya magoli ya kufunga timu zinapofungana points kinafuta kabisa uwezekano wa M'gladbach kufuzu hata kama itaifunga barcelona milioni moja na city ikapigwa na celtic bilioni.Hii ni kwakuwa zote mbili zitakuwa na points sawa lakini H2H zao kwenye michuano hii haibadiliki.
Group D
Atletico Madrid na Bayern Munich zimeshafuzu kundi D huku vijana wa El Chollo wakifanikiwa kuwa timu pekee hadi sasa ambayo imeshinda michezo yake yote.Rostov na PSV zimeshafungashwa virago hapa na wamebakiza kukamilisha ratiba tu.
Group E
Monaco imeshafuzu hapa huku CSKA Moscow wakiwa tayari wameshaaga michuano.Leverkusen pia wameshafuzu kwani point zake zinaweza kufikiwa na Spurs tu lakini Spurs imeshindwa kwenye H2H kwenye mechi baina yao kwenye michuano hii.Hivyo spurs wameshatolewa kwa kigezo hiki na hakuna uwezekano wa wao kufuzu hata iweje.
Group F
Borussia Dortmund na Real Madrid zimeshafuzu kundi hili.Sporting Lisbon na Legia Warsal hazina nafasi kabisa ya kufuzu.Dortmund wanaongoza wakifuatiwa na Madrid.
Group G
Leicester City wameshafuzu hapa na Club Brugge imeshaaga huku ikiwa haina point.FC copenhagen na FC porto yoyote ina uwezo wa kufuzu na kuungana Leicester.
Group H
Juventus inatimiza idadi ya timu 12 ambazo zimeshafuzu raundi ya mtoano.Sevilla ina nafasi kubwa ya kupenya ukilinganisha na Lyon.Lyon inaweza kufuzu kama itaifunga sevilla mechi ya mwisho kwa ushindi mzuri zaidi ya ule wa moja bila iliopata sevilla nyumbani kwao mechi ya kwanza.Ushindi wowote wa goal difference ya kuanzia mbili unatosha kuivusha Lyon raundi ya 16 bora.
Karibuni tujadili.