Kuelekea Champions league final Millenium Stadium

Kuelekea Champions league final Millenium Stadium

Mnyakatari

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2010
Posts
2,073
Reaction score
1,862
Ni Jumamosi ya tarehe 3 June 2017 ndiyo siku itakayopigwa fainali ya 25 ya uefa champions league na ya 62 tangu kombe hilo likiitwa Europa Cup.Ni ndani ya Millenium Stadium uliopo mji wa Cardiff nchini Wales.

Hapa tutakuwa tunapeana mambo mbalimbali juu ya ligi hii jinsi inavyoendelea mpaka fainali.Bado tupo hatua ya makundi ambapo mechi moja tu kwa kila timu imesalia kumaliza mzunguko wa makundi zitakazofanyika hapo December 6 na 7.

Ni timu 12 ndizo zimeshafuzu kuingia raundi ya 16 bora ambapo 4 zingine zitajulikana baada ya mechi za mwisho.

Group A
PSG na arsenal zimeshafuzu kundi A.Zote zina points 11 huku PSG ikiwa inaongoza kwa kuwa kwenye head to head PSG wana magoli mengi ya ugenini ingawa mechi zote mbili ilikuwa sare.Ikumbukwe kuwa arsenal ina magoli mengi ya kufunga kuliko PSG lakini H2H inaangaliwa kwanza kwenye uefa kabla ya magoli ya kufunga.Ludogorets na Basel zikiwa na points 2 kila moja zimeshaaga mashindano zimebakia tu kumalizia ratiba.

Group B
Katika group B ni Dynamo kiev pekee ndiyo haina nafasi ya kufuzu au tuseme imeshaaga mashindano hayo.Timu mbili zozote kati ya Napoli,Benfica na Besiktas zina uwezo wa kufuzu itategemea na matokeo ya mwisho ya makundi.

Kund C

Barcelona imeshafuzu hapa na Celtic imeshaaga michuano.Manchester City imeshafuzu pia kwa kuwa head to head yake na M'gladbach inaibeba.Kigezo cha kuangalia kwanza head to head kabla ya magoli ya kufunga timu zinapofungana points kinafuta kabisa uwezekano wa M'gladbach kufuzu hata kama itaifunga barcelona milioni moja na city ikapigwa na celtic bilioni.Hii ni kwakuwa zote mbili zitakuwa na points sawa lakini H2H zao kwenye michuano hii haibadiliki.

Group D

Atletico Madrid na Bayern Munich zimeshafuzu kundi D huku vijana wa El Chollo wakifanikiwa kuwa timu pekee hadi sasa ambayo imeshinda michezo yake yote.Rostov na PSV zimeshafungashwa virago hapa na wamebakiza kukamilisha ratiba tu.

Group E

Monaco imeshafuzu hapa huku CSKA Moscow wakiwa tayari wameshaaga michuano.Leverkusen pia wameshafuzu kwani point zake zinaweza kufikiwa na Spurs tu lakini Spurs imeshindwa kwenye H2H kwenye mechi baina yao kwenye michuano hii.Hivyo spurs wameshatolewa kwa kigezo hiki na hakuna uwezekano wa wao kufuzu hata iweje.

Group F

Borussia Dortmund na Real Madrid zimeshafuzu kundi hili.Sporting Lisbon na Legia Warsal hazina nafasi kabisa ya kufuzu.Dortmund wanaongoza wakifuatiwa na Madrid.

Group G

Leicester City wameshafuzu hapa na Club Brugge imeshaaga huku ikiwa haina point.FC copenhagen na FC porto yoyote ina uwezo wa kufuzu na kuungana Leicester.

Group H

Juventus inatimiza idadi ya timu 12 ambazo zimeshafuzu raundi ya mtoano.Sevilla ina nafasi kubwa ya kupenya ukilinganisha na Lyon.Lyon inaweza kufuzu kama itaifunga sevilla mechi ya mwisho kwa ushindi mzuri zaidi ya ule wa moja bila iliopata sevilla nyumbani kwao mechi ya kwanza.Ushindi wowote wa goal difference ya kuanzia mbili unatosha kuivusha Lyon raundi ya 16 bora.

Karibuni tujadili.
 
Kwa upande wa ufungaji wa magoli Lionel Messi anaongoza mpaka sasa kwa mabao 9 huku Edson Cavani akifuata kwa mbali na magoli yake matano.Messi amebakiza goli tatu tu aifikie rekodi ya Christian Ronaldo ya ufungaji bora wa wakati wote kwenye michuano hii.Ronaldo ana goli 95 huku Messi akiwa na 92.
 
Borrusia Dortmund inaongoza kwa kufunga mabao mengi mpaka sasa.Wamefunga goli 16 ambayo ni mengi zaidi ukilinganisha na timu zingine.

Waluofungwa goli nyingi zaidi hadi sasa ni Legia Warsaw ambayo imefungwa goli 24 hadi sasa.Wastani wa goli 5 kila mechi.

Pia timu ya Dynamo Zagreb haijafunga goli hata moja kwenye michezo yake mitano iliyocheza hadi sasa.
 
Leo kuna mechi za kumaliza mzunguko wa makundi.

Kundi A PSG na Arsenal yeyote akiteleza anajikuta nafasi ya pili pale wanapokutana na timu zisizo na nafasi.Basel wanawakaribisha arsenal na Ludogorets ni wageni wa PSG.
 
Kundi B Besiktas inahitaji ushindi wa lazima pale itakapokaribishwa na timu inayokamilisha ratiba Dynamo Kiev.Ushindi wowote kwa Besiktas utaihakikishia nafasi mbili za juu kwenye kundi.

Benfica inaikaribisha Napoli na kila timu itasaka ushindi hapa hasa Napoli ambayo inajua droo yoyote itaihakikishia nafasi Benfica huku yenyewe ikiombea Besiktas isipate ushindi.Ili kujiweka mbali na utegemezi wa matokeo ya mechi ya besiktas napoli wanahitaji ushindi.
 
Kwa ujumla kundi C mshindi wa kwanza ni Barca na wa pili ni Man City.Hii ni hata baada ya mechi zao za leo kwani hakuna matokeo yanayoweza badilisha huu msimamo.Hivyo leo inategemewa mechi za kundi hili ziwe rahisi huku wachezaji muhimu wakipumzishwa kwani hakuna kinachotafutwa cha maana zaidi ya kuweka rekodi tu kwa timu na wachezaji hasa Messi
 
Kundi D pia leo ni mechi za kuweka heshima zaidi kwani hakuna matokeo yatakayofanya mshindi wa kwanza asiwe Atletico na wa pili asiwe Bayern Munich.
Bayern inaikaribisha Atletico na inategemewa wachezaji muhimu watapumzishwa kwenye mechi hii.
 
Kwa ujumla kwenye mechi zote 8 za leo timu sita zinazofuzu zimeshafahamika kabla ya mechi.
PSG
Arsenal
Barcelona
Man City
Atletico Madrid
Bayern Munich

Timu zingine mbili ni zozote kati ya Napoli,Benfica na Besiktas.
 
Leo kuna mechi za kumaliza mzunguko wa makundi.

Kundi A PSG na Arsenal yeyote akiteleza anajikuta nafasi ya pili pale wanapokutana na timu zisizo na nafasi.Basel wanawakaribisha arsenal na Ludogorets ni wageni wa PSG.
PSG imeteleza baada ya kulazimishwa sare jana huku arsenal wakipanda juu kwa ushindi wake mnono dhidi ya Basel jana.

Kwa hiyo namba moja kundi A ni Arsenal na wa pili ni PSG.
 
Kundi B Besiktas inahitaji ushindi wa lazima pale itakapokaribishwa na timu inayokamilisha ratiba Dynamo Kiev.Ushindi wowote kwa Besiktas utaihakikishia nafasi mbili za juu kwenye kundi.

Benfica inaikaribisha Napoli na kila timu itasaka ushindi hapa hasa Napoli ambayo inajua droo yoyote itaihakikishia nafasi Benfica huku yenyewe ikiombea Besiktas isipate ushindi.Ili kujiweka mbali na utegemezi wa matokeo ya mechi ya besiktas napoli wanahitaji ushindi.
Besiktas imegalagazwa na Dynamo kiev goli 6 bila.Kwa hiyo zote zimeaga huku Napoli na Benfica(ingawa walifungwa jana na napoli) zikifuzu raundi inayofuata.

Kundi hili napoli wanaongoza wakifuatiwa na benfica.
 
Kundi C Barca ni ya kwanza man city ni ya pili wakati kundi D Atletico madrid ingawa imefungwa jana na Bayern inaendelea kuwa juu ya kundi.
 
Atletico madrid baada ya kipigo cha jana imeshindwa kuweka rekodi ya kuwa timu ya sita kushinda mechi zote za group stage.Timu tano zilizowahi kufanya hivyo ni Real Madrid(mara 2),AC Milan,Sparta Moscow,Barcelona na PSG.
 
Mechi za leo kundi E
Bayern leverkusen v Monaco

Spurs v CSKA Moscow

Monaco na Leverkusen wameshafuzu hapa na hakuna namna yoyote itakayobadilisha timu ya kwanza na ya pili.Vyovyote iwavyo monaco ni ya kwanza na Leverkusen ya pili.
 
Kundi F leo

Legia warsal v Sporting Lisbon

Real Madrid v Borussia Dortmund

Real madrid na Dortmund zimeshafuzu hapa na mechi yao leo itakuwa ni kugombania nafasi ya kwanza.
 
Kundi G leo

Club Brugge v FC Copenhagen

FC porto v Leicester city
Leicester City wameshafuzu hapa na Club Brugge imeshaaga huku ikiwa haina point.FC copenhagen na FC porto yoyote ina uwezo wa kufuzu na kuungana Leicester.
 
Kundi H

Juventus v Dynamo Zagreb

Lyon v Sevilla

Juventus imeshafuzu hapa.Sevilla ina nafasi kubwa ya kupenya ukilinganisha na Lyon.Lyon inaweza kufuzu kama itaifunga sevilla mechi ya mwisho kwa ushindi mzuri zaidi ya ule wa moja bila iliopata sevilla nyumbani kwao mechi ya kwanza.Ushindi wowote wa goal difference ya kuanzia mbili unatosha kuivusha Lyon raundi ya 16 bora.
 
Timu ambazo zimeshafuzu kwa mechi za leo ni
monaco
leverkusen
Real madrid
Dortmund
Leicester
Juventus
 
Kwa match za jana Barcelona walipiga pass 993 huku Ineista pekeee akipiga pass 108!!!
Istand to be corrected
 
So far timu 16 zilizofuzu ni zifuatazo
Group winners
Group A
Arsenal
Group B
Napoli

Group C
Barcelona

Group D
Atletico madrid

Group E
Monaco

Group F
Dortmund

Group G
Leicester

Group H
Juventus
 
Group runners up

Group A
PSG

Group B
Benfica

Group C
Man city

Group D
Bayern munich

Group E
Leverkusen

Group F
Real madrid

Group G
Porto

Group H
Sevilla
 
Back
Top Bottom