Kuelekea Dar Derby VPL Simba SC dhidi ya Yanga SC, One Touch Operation 3 Points

Kuelekea Dar Derby VPL Simba SC dhidi ya Yanga SC, One Touch Operation 3 Points

Hua nachugiaga simba akimfunga gongowazi goal moja naumia kwel, vyura inabdi wafe hata goal,7
Mkuu tuonee huruma sisi Vyura tufungeni angalau 5 tu zitatutosha.

Nyuma mbele daima mwiko
 
Mungu ibariki simba Sports Club mnyama mkali kabisa msituni
IMG_20200104_154621_538.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hello Hello!

Kuelekea Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL Jumamosi January 4, 2020 utapigwa mchezo wa watani wa jadi (Dar Derby), ambapo mabingwa wa nchi Simba SC mnyama mkali, wanawakaribisha Yanga SC kwenye Uwanja wa Taifa.

Mchezo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote hasa ukizingatia ni mchezo wa kwanza kwa watani wa jadi kukutana kwa msimu huu wa Vodacom Premier League VPL 2019/2020.

Simba SC, inaongoza ligi kwa alama 34, dhidi ya Yanga SC yenye alama 24 wanataka kuwahakikishia Wanasimba na Wadau wa soka kwamba hawaongozi ligi kwa bahati mbaya bali kutokana na uwezo wa kikosi chao ambacho kimesheheni nyota wengi wenye uwezo mkubwa wa kupata ushindi pamoja na kutoa burudani uwanjani.

Yanga SC, kutaka ushindi mchezo huu, wana kikosi cha kawaida sana pia wana shida nyingi ndani na nje ingawa kwa sasa wanajitahidi kupunguza shida hizo, lakini kila mmoja anajua kwamba kuna matatizo ya wachezaji kudai mishahara pamoja wengine kuvunja mikataba yao.

Watu wanaofuatilia kandanda wanajua kwamba kwa sasa ukitaja timu bora hapa nchini Tanzania ni Simba SC, yenye uwazo mkubwa wa kiuchumi hivyo basi kupelekea kuwasajili wachezaji mahiri wenye kuamua matokeo ya ushindi uwanjani.

Wanasimba jongea hiyo January 4 2020 kushuhudia kandanda safi lililothibitishwa na shirikisho la soka Afrika CAF kutoka kwa Simba SC, One Touch Operation 3 Points, Kulitaka Mwana, Kulipewa Mwana

SimbaNguvuMoja Next Level
View attachment 1310739View attachment 1310740View attachment 1310742
Hi mechi wenye maamuzi nayo ni hawa wash ezi wa sports pesa na M pesa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom