Kuelekea kuadhimisha miaka 10 ya ndoa

Hongera mkuu, inaonekana mda wa uchumba uliutumia vizuri katika kuchunguzana.
Asikudanganye mtu hakuna cha kuchunguzana wala nini, ukimchunguza sana binadamu utakuta madhaifu kama 100 na ushee, na kila ukichunguza utabaini mengi zaidi, na kila achunguzae sana haoi, mwisho wake huishia kula tunda kimasihara na kutokomea. Kama huamini fuatilia hili kwenye jamii zetu utabaini ukweli.
 
Unasherekea miaka 10 ya kugongewa bila kujua?😂

Hakuna mke wa mtu aliewahi nikataa otherwise wako Ni mbovu
 
Unasherekea miaka 10 ya kugongewa bila kujua?😂

Hakuna mke wa mtu aliewahi nikataa otherwise wako Ni mbovu
Hata akiwa mbovu ni sawa tu ilimradi maisha yanakwenda. Then unagonga wa wenzio basi nakutahadharisha tu jiunge na team kataa ndoa. Maana uchungu wa kugongewa hauwezi kukukwepa endapo utaoa. Malipo ni hapa hapa duniani.
 
Hatukatai kuishi kinyumba baina ya mwanamke na mwanaume, hatukai watoto kulelewa kimaadili wakiwa chini ya uangalizi wa wazazi wote wawili, hatukatai mahusiano yana kupanda na kushuka ivyo kuvumiliana na kusameheana ni muhimu. Tunachokataa ni ule mkataba mnaotakiwa kuusaini kwa sababu vifungu vyake vinamkandamiza mwanaume pale ndoa inapovunjika.
 
Wewe kwani hutaki ukilala unamkumbatia mtu badala ya mto!
Nataka,

Ila isiwe tukio, mara harusi mara sendoff nini....

Naamini watu wawili kukubaliana kushare maisha kuna nguvu kuliko kufanya matukio ya kufurahisha watu

Labda kusaini cheti tu ndo muhimu
 
Inamaana huelewi kuwa wewe mwenyewe ni athari ya kizazi cha mababu zako, au hujui kama mababu zako walizaliwa na hata wao pia walikuwa na mababu zao hadi kufikia wewe!
Sasa mimi inanisaidia nini hiyo ya mababu zangu kuwa na mababu zao
 
Umesomeka na kueleweka barabara.
 
Mwaka ujao,natimiza miaka 10 ya ndoa,ndoa ni nzuri,familia ni nzuri,kila napoamka asubuhi nawaona watoto wangu wanavyonifurahia,naporudi nyumbani wanavyonikimbilia na kunikumbatia,nahisi faraja,Upendo,amani najawa na tumaini katika maisha🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…