Kuelekea kuapishwa Biden kuwa Rais wa Marekani raia na askari hawatambuliki wote wamebeba silaha

Kuelekea kuapishwa Biden kuwa Rais wa Marekani raia na askari hawatambuliki wote wamebeba silaha

Hii habari ingekuwa imeletwa inahusu nchi za Africa yangemwagwa matusi ya kiswahili na ya kizungu hapa,lakini kwasababu ni U.S akuna tusi hata moja.
Unamlalamikia nani sasa? Wewe si umwage matusi kama unaona ni mahala pake?
 
Kuna andiko flani kwenye msaafu ikizungumzia Marekani na utawala wake huku matukio makubwa kama haya yakiongelewa kwa undani japo ni kwa kificho.

Maandiko hayo yameandikwa kwa kificho ili wajuzi waweze kuyafumbua.
 
watu wanaandamana na siraha, polisi wanasindikiza maandamano bila kuwadhuru hao raia, huu ni mfano bora kabisa wa majeshi kuheshimu uhuru wa mawazo na kuandamana bila kusababisha madhara kwa raia, au unadhani majeshi ya marekani hayana uwezo wa kuwaua hao raia? na kuwabambikia kesi za uhaini? swali la kujiuliza ingekuwa hapa kwetu Afrika nini kingetokea unampinga rais mweusi alie chaguliwa? hiiii utanyonyolewa hata kama huna manyoya.
Ndugu, siyo kwamba hao wanajeshi wanawaheshimu hao waandamanji ila wanaogopa wakiwagusa silaha zaidi ya hizo zinakuja road!

Alafu kwa mujibu wa bbc hao wenye silaha ni makundi ya wanamgambo, mfano hilo la waliovaa vikaragosi wana kiongozi wao kabisa.

[emoji23][emoji23][emoji23]Yani USA inabidi viongozi wao waishi na hao raia kwa adabu yani hata wakitiwa vidole machoni wakae kimya tu maana wakifurukuta kwa jinsi raia wa huko walivyo na siraha watamalizana.
 
1610988308429.png

Jamani hapa ni juzi tarehe 6 Jan huyo mnayemwona katikati kama hapa kwetu ni waziri kukuu Kasim Mjaliwa bungeni Dodoma, wanausalama wakijaribu kuokoa maisha yake mbele ya waandamanaji wenye democrasiya ya kutosha duniani.

1610988603854.png

Hawa si FBI au US Army, hawa ni raia wema ambao wanatimiza haki yao ya kidemocrasia wakiwa wamebeba siraha za kivita fulu magazini ktk maandamano, wakati huku kwetu kwa Magu hata gusa tu barabara ugusi.

1610988639139.png

Waandamanaji wakiwa nje ya jengo la serikali huku wakiwa na siraha za kijeshi na nzito tayari kwa lolote lile kutimiza haki ya ya kidemocrasia.



1610988692335.png

Hapa muandamanaji akichukuwa selfii kwa ajiri ya kuwatumia jamaa zake huku yeye na mwenzake wakiwa na siranzito kuliko zile tulizotumia mwaka 1978 kule Mutukula Uganda kumwondoa Idi amini.

Jamani zimebaki siku tatu 2 kufutika kwa taifa ambalo lilikuwa linapigiwa mfano kila kuitwapo leo kuwa mababa wa democrasia duniani Marekani. Tangia mwaka 1992 milango ilipofunguliwa tume kuwa tukiubiliwa na sisi tuwe na democrasia kama ya Marekani mpaka tumechoka.
Sijui kama nyakati za mwisho zimefika, wakati mimi ukusanyaji wa sadaka bado haujanitosha. Naelekeza swali kwa wanaharakati wa Tanzania ambao wamekuwa wakisisitiza kwa miongo kadha sasa kuwa tufuate siasa na democrasia za Marekani leo wanahoja gani kwani siwaoni wala kuwa sikia kanakwamba hawapo au awaoni chochote.

Maduka ya siraha yanafanya biashara kuliko wakati wowote tangia kuruhusiwa kununua sira nchini humu, kila raia anajaribu kununu mkwasa wake hili kunukishiana kama ilivyotokea kwa Wahutu na Watusi na sasa leo ngoma imeamia kwao.


Bwana mmoja ambaye yeye alikuwa anataka kununua lile la kuweka begani lakini ilishindikana hivyo wameamua kwenda wekshopu kutengeneza wenyewe, taarifa sisizo rasmi lakini zenye ukweli kuwa siku hiyo ya kuapishwa Biden ndiyo huo mchezo wa kuchezea moto juu ya tanki la petroli utaanza kuchezwa nchini Marekani
1610991910713.png


Macho ya dunia nzima yatakuwa yakishuhudia mwisho wa kitu kinanachitwa democrasia duniani.


Taarifa tulizopata ni kuwa kilakitu kitalipwa hapa hapa duniani kwani sitaki kusema mengi ila wafuasi wa Trump na Biden wanapishana katika maduka ya siraha kuhakikisha wanapata bunduki nzuri na risasi za kutosha kwa kazi ya siku hiyo.

Taasisi za kidini pia nazo zimemiminika katika viwanda na maduka hili kuweza kujipatia siraha kwaajili ya kuwa tayari kwa chochote siku hiyo kwani hawana hakika na maombi tupu.
Tayari watu 5 akiwemo polisi mmoja wamekwisha fariki dunia wakati wa maandamano ya kuvamia bunge wakitimiza haki yao ya kidemocrasia ya kuandamana kama Lisu na Mbowe walivyokuwa wakisisitiza ndiyo maana leo nimeelewa kauli ya Mtu huru aliyekuwa anasherehekea sikukuu zote Segerea aliwai kusema Tanzania lazima ibebe majeneza wakifa watu 100 au 200 tutapata haki. Kumbe alijifunza huko na leo Mungu kaweka wazi Wamerekani wanatafuta haki na bundiki.

Vijana wa Tanzania na wana harakati Mungu wa baba zetu Afrika na atusaidi tujikwamue kutoka katika utumwa wa kiakili.

Na aimidiwe Mungu wa baba zetu Afrika kwani majibu yameanza kupatika.

Mtoto wa mchungaji nawasilisha.
 

Attachments

  • 1610991851481.png
    1610991851481.png
    26.4 KB · Views: 1
uhuru wa kumiliki silaha sasa utatumikake

AMSTERDAM NA LISU KWENYE HILO WAKO KIMYA
 
Hali mbaya marekani askari wametanda mitaani inayoelekea ikulu

 
hali tete askari wengi mno ona wanalala hadi sakafuni kwa kulala hamna

 
Kwangu ni kukomaa kwa demokrasi ya hali ya juu sana.

yaani watu wanaruhusiwa kuandamana hata na siraha bila bughudha yoyote hali mradi hawafanyi fujo.

Kwa nchi za kiafrica na za kikomonist dhubutu hata kupeperusha jani angani ni shida kubwa sana.
"yaani watu wanaruhusiwa kuandamana hata na siraha bila bughudha yoyote hali mradi hawafanyi fujo."

Vitu vingine mnavyo sifia, yani kuandamana na Silaha ndio demokrasia,vip hao askari nao watakuwa na hali gani endapo vurugu zikitokea.

Kama hujui zaidi ya 80% ya wamarekani wanamiliki silaha na maandamano haya lazima yatakuwa na vurugu,sasa pata picha silaha hizi zikitumika.
 
Kila nchi lazima ichague kipi bora, uhuru au amani? Wamarekani wamechagua uhuru ni bora kuliko amani, Watanzania tumechagua amani ni bora kuliko uhuru. Wamarekani wako tayari kuvuruga amani ili watete haki zao, Watanzania tuko tayari kusalimisha au kunyang'anywa haki zetu ili tuishi kwa amani.

Kwa hiyo yanayotokea Marekani sasa hivi ni mambo ya kawaida kwao. Wameshapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe (civil war), wameshapiga risasi na kuuwa maraisi wao wengi tuu (Abraham Lincoln, James Garfield, William McKinley, John Kennedy) na machafuko mengine mengi tuu lakini Marekani bado ipo.
 
"yaani watu wanaruhusiwa kuandamana hata na siraha bila bughudha yoyote hali mradi hawafanyi fujo."

Vitu vingine mnavyo sifia, yani kuandamana na Silaha ndio demokrasia,vip hao askari nao watakuwa na hali gani endapo vurugu zikitokea.

Kama hujui zaidi ya 80% ya wamarekani wanamiliki silaha na maandamano haya lazima yatakuwa na vurugu,sasa pata picha silaha hizi zikitumika.
Kumiliki silaha ipo kikatiba ajabu ni nin
 
Kwao kweli zipo kikatiba,ila kumbuka watu wanaozishika walikuwa na ujasiri mpaka kuvunja jengo la bunge manake wanaweza kufanya chochote.
Marekani kabla hata ya kupata Uhuru watu walikua wanamiliki silaha kiholehola holela hawajaanza leo
 
Mwingine kakamatwa ana kitambulisho kama mlinzi wa Capitol Hill na gwanda na bunduki nzito
 
Back
Top Bottom