Kuelekea kupanga mishahara upya; Mishahara ilingane kwa kada zote

Kuelekea kupanga mishahara upya; Mishahara ilingane kwa kada zote

Nani kasema haunitoshi na hata usiponitosha kuna overtime, night, calls, procedures, bima, part time hapo sijazungumzia clinic, unajua MMED anakula ngapi serikalini?.... ni mishahara ya miezi 5 ya mwalimu mwenye degree, intern doctor tu wanakula 1. 2M yaani katoka tu MD 5 hata leseni hana, halafu ninyi muliofeli na kushindwa kusoma udaktari na pharmacy wengi wenu ndio walimu, munakuja kutusumbua na visredi vyenu vya kipuuzi, nani alikukataza kugonga one six ukachue jiwe lako la MD pale MUHAS pengine ungekuwa una superspeciality in hepatogastroentelogy sasa unakula zaidi ya 5M/months.
Hivi ww bwana mdogo ni dokta kweli??

Mbona mwaka 2015 ulikuwa kidato cha nne na baba yako mkubwa alikudhulumu mali za urithi??

Unayocomment mengine hata huyajui bali umesikia tu story za vijiweni!!

https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/837729/
 
Umelipokea andiko langu kwa mtizamo hasi.. hakuna niliposema waliosoma arts ni villaza. na hakuna niiposema waliosoma uhasibu au ualimu hawakusoma sayansi.

kada zote zinategemeana, hakuna engineer bila mwalimu, nahakuna shule bila engineer. lakin ni jambo la busara kuzipa kipaumbele baadhi ya kada kwa sababu njia yake ni ngumu kuliko kada nyingine, lengo likiwa kuwatia moyo watoto kupenda kada husika japo wanajua ni ngumu.

kutokana na ugumu uliopo wa kuwa engineer kamili, engineer akilipwa sawa na mwalimu watoto watachagua kuwa walimu na tutakosa kada hiyo.

achana na mambo ya passion mkuu.. sijui mambo ya wito.... hayo ilikuwa zamani. siku hizi mafanikio ya kimaendeleo ndo suala la msingi.

Pengine urekebishe namna yako ya kuwasilisha mitazamo yako kwani waweza kuwa waongea kitu chenye ukweli pasipo matumizi ya kejeli kama "degree za kwenye vimbweta "...... lazma ukijiweka hasi,hakuna wa kukuchukulia chanya na pia sintokulazimisha kubadilisha mitazamo yako katika maisha kwa kuwa ninaamini umepevuka vya kutosha katika kujiamulia njia gani ni sahihi kwako kuifuata

Turudi katika mada husika....

Haitotokea kamwe kada zote kuwa na mshahara sawa hata siku moja kwa kuwa ni mambo mengi huchangia katika kuamua kiasi cha mshahara na wala haiepukiki kwa mfano : uhaba wa wataalamu hupelekea thamani yao kupanda kuliko wale ambao hupatikana ki rahisi, umuhimu wa kada husika kutokana na mahitaji na sera ya nchi husika n.k
 
ok, tushafunga mjadala. tunatofautiana namna ya kuwasilisha jambo lakin mtizamo wetu upo sawa katika mada hii ya kulinganisha mishahara.
 
hoja yako ya kipuuzi, kwani kwenye afya hakuna wanaoungaunga mpaka ngazi ya degree au masters?
vp na we umeungaunga nini mbona maneno makali? haya say wote wameunga unga we usome miaka yako mitano ya kuunga unga huo ualimu wako ulinganishe na afya aliyesoma miaka 9? mwalim mwenyewe wa civics au history?
 
Huwezi ukalipa mshahara kwa sababu tu wote wa degree au diploma au Cheti

degree ya miaka 03 mfano sociology , IPO degree ya miaka 04 Mfano Law ya SAUT, IPO degree ya miaka 05 MF medicine

Diploma IPO ya miaka 02 mfno uhasibu,
Ipo diploma ya miaka 03 mf n pharmacy nk

Kuwalipa watu wote sawa ni ndoto za mchana haiwezekani na hajawai kutokea Duniani kote,

Duniani kote watu wanalipwa kulingana na muda waliotumia shule pamoja na ugumu wote course husika ASANTE NAOMBA NIWASILISHE MH.
 
habari wanandugu!

Nianze kwa kusema kuwa niipongeze serikali kwa nia nzuri iliyonayo ya kupitia na kupanga upya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi wa kada zote.

kwa muda mwingi tumeshuhudia kutofautiana kwa viwango vya mishahara kutoka fani Moja kwenda fani nyingine, mfano ualimu, afya, sheria, uhandisi n.k ambapo baadhi ya Kada wamekuwa wakilipwa mishahara mikubwa kuliko wengine ingawa ukiangalia majukumu na mazingira yao ya kufanyia kazi hayatofauti sana.

kutofautiana huku kwa mishahara kunapelekea baadhi ya wafanya Wa Kada Fulani kuwadharau wafanyakazi Wa kada nyingine, lakini pia no uharibifu Wa pesa kwani kama MTU yule yule (mwalimu) analipwa 20000 na naweza kuishi basi hata huyu mwingine (daktari) akilipwa 20000 ataweza kuishi na kutimiza mahitaji yake. sula hili siyo zuri

katika kuelekea kupanga mishahara upya serikali ifanye utaratibu Wa kulinganisha mishahara kwa wafanyakazi wote kwa kutegemeana na viwango vyao vya elimu. yaani wenye elimu ngazi ya shahada mshshahara wao ulingane, hali kadhalika ngazi ya diploma na cheti

by mkulima Wa nyanya
Vipi, hii itahusu na sekta binafsi?
 
Mkuu, wakati wenzio wanachagua kitu cha kwenda kusomea chuo wewe ulichagua ualimu kwa kuamini utapata mkopo 100%. Sasa mkopo wa miaka mitatu unaharibu maisha yako yote labda uwe mpambanaji.

Wakati wenzako wanasoma PCB wew uko busy na HKL yako ya kuunga unga ili upate tiketi ya chuo.....

Later unaanza kuota ndoto za watu wote kulipwa sawa? Crazy huh!
 
Unadhani inawezekana hivi changamoto za idara ya afya unaifananisha na idara ya elimu?

Ufananisho huu unatumia hoja ipi Mkuuu
changamoto gani kuzidi walimu?.Unadhani utapata watumishi wa afya wazuri bila walimu wazuri?Ni Tanzania tu,unapokumbana na mawazo mafupi kama haya.
 
Tatizo sio muda wa masomo tatizo n risk nitamshaanga na itakua nchi ya ajabu et mishahara ikiwa sawa.wauguzi na madaktari wengi wanakufa Kwa hepatitis,HIV,Tb ndo kabisaaa wanaugua ad sio vizuri ifike time tudai haki mishahara ipandishwe ila tusijtoe fahamu eti iwe sawa. Walimu mnafanyakazi sawa ila mmezidi kulalamika.

Sent from mTalk
 
Wewe mawazo yako ni finyu sana, yaani mimi nilieyekaa darasani miaka 5 ya udaktari, mwaka mmoja intern, nilingane na wewe wa miaka 3, si itakuwa maajabu haya, Hilo halitakaa litokee, unajua strength ya shule ya medicine wewe?
Waalimu ni wengi mno. Ukipandisha sana mishahara ya kada hii nchi itafilisika.
 
kuna watumishi wanakaa maporini wakilinda tembo, wapo idara ya wanyamapori (now TAWA).. mishahara yao ni sawa au kuzidiwa kdg na walimu! mazingira ya kazi ni magumu, majangili wenye silaha za vita hupambana nao. nyoka jamii ya koboko, wamejaa huko maporini, akikugonga ni instant death!! changamoto kama uhaba wa nyumba, maji, umeme, nk ni sawa na walimu wa remote arrears,, kwa maoni yangu hawa ndo wanaostahili mishahara minono
 
habari wanandugu!

Nianze kwa kusema kuwa niipongeze serikali kwa nia nzuri iliyonayo ya kupitia na kupanga upya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi wa kada zote.

kwa muda mwingi tumeshuhudia kutofautiana kwa viwango vya mishahara kutoka fani Moja kwenda fani nyingine, mfano ualimu, afya, sheria, uhandisi n.k ambapo baadhi ya Kada wamekuwa wakilipwa mishahara mikubwa kuliko wengine ingawa ukiangalia majukumu na mazingira yao ya kufanyia kazi hayatofauti sana.

kutofautiana huku kwa mishahara kunapelekea baadhi ya wafanya Wa Kada Fulani kuwadharau wafanyakazi Wa kada nyingine, lakini pia no uharibifu Wa pesa kwani kama MTU yule yule (mwalimu) analipwa 20000 na naweza kuishi basi hata huyu mwingine (daktari) akilipwa 20000 ataweza kuishi na kutimiza mahitaji yake. sula hili siyo zuri

katika kuelekea kupanga mishahara upya serikali ifanye utaratibu Wa kulinganisha mishahara kwa wafanyakazi wote kwa kutegemeana na viwango vyao vya elimu. yaani wenye elimu ngazi ya shahada mshshahara wao ulingane, hali kadhalika ngazi ya diploma na cheti

by mkulima Wa nyanya

Mmoja kati ya wale wanne.
 
Nimejaribu kusikiliza kiini cha hoja ya mabadiliko ya mishahara nadhani tatizo ni uelewa
Usawa unaozungumziwa siyo wa mwalimu, mhandisi ama mhasibu n.k walingane mshahar ila watu haswa watumishi wa umma wenye taaluma sawa kwenye fani sawa walingane mishahara kuanzia serikali kuu TAMISEMI na taasisi za serikali tofauti na ilivyo sasa hv. Mfano sasa hv Daktari anayefanya kazi serikalini analipwa tofauti na kwenye taasisi za serikali na hospitali za serikali jambo ambalo kimantiki si zuri maana utakuta wote wana ujuzi na elimu sawa. (Mfano Daktari bingwa wa akinamama na watoto anayefanya Hospitali ya BOMBO analipwa tofauti na mwenzake aliyepo Bugando ama MNH Muhimbili regardless ya elimu sawa. Mabadiliko ya namna hii nafikiri ni mazuri ili kuleta ufanisi sawa sehemu za kazi. Si vyema Daktari aliyeajiriwa na wizara ya afya kwa mfano akawa stationed Muhimbili kupokea mshahara mdogo kuliko aliyeajiriwa na MNH muhimbili direct na wanafanya kazi sehemu moja pia. Huo ni mfano wa kero za sasa za utofauti wa mshahara.
Nadhani utafiti wa kina unahitajika katika kuleta hayo marekebisho yawe na tija haswa yakizingatia Hali halisi ya maisha yakiwa yanalenga kuongeza kuliko kupunguza mishahara ili kuboresha maisha ya wafanyakazi wa Tanzania

Maledhi
 
ni vizuri mishahara ikalipwa kwa kuzingatia elimu ya mtu, na marginal productivity of labour
 
Back
Top Bottom