Kuelekea kupanga mishahara upya; Mishahara ilingane kwa kada zote

Kuelekea kupanga mishahara upya; Mishahara ilingane kwa kada zote

Huu ni uzi wa kutambiana. Angalieni msije mkapigana.Napita tu[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji126] [emoji125]
 
Kuna vitu vingine vinachekesha kweli dunia mzima haupo huo utaratibu mtu na MMED yake ya neurology anachambua ubongo kama mchele amekaa darasani miaka 9 eti alipwe sawa na mwalimu wa civics form one, NONSENSE.
Ukiona sehemu wanalipa vizuri hamia huko.
kwa taarifa yako kuna watumishi wanaolipwa zaidi ya huyo daktari aliyekaa miaka tisa darasani
 
Alaf walimu wengi haswa wa secondary ni washirikina
 
Taja nchi yoyote nyingine iliyowahi kufanya hivyo hata kama ni enzi za ujamaa.

Mwalimu wa History alipwe sawa na daktari!!

Kwangu naona hata walimu wa sayansi wanatakiwa walipwe zaidi ya wale wa Sanaa.
 
Ndio nimemjibu huyo mtoa mada kuwa haiwezekani mtu anayeunga mifupa ya binadamu eti alipwe sawa na mtu anayekalilisha "videfiniton"

Mbona watu wanakwenda India kutibiwa?na kwa nn hawaendi kufundishwa "civics"?inawezekana madakitari wengi hawana mchango mkubwa kwa jamii,huenda pia wamekaririshwa tu
 
Huu utakuwa ni uwendawazimu na bangi. Ni ujinga wa hali ya juu na hayo ni mawazo ya kimaskini.
Kila kada inatoa mchango tofauti kwa taifa na ina changamoto zake, hivyo sio sawa kutaka kutafuta usawa katika kuwalipa.
Anayelipwa Vizuri aendelee kulipwa vizuri na anayelipwa kidogo anapaswa aanze kulipwa vizuri.
Kila ajira na ujira wake.

Kumshusha chini anayelipwa vizuri ili alingane na wa chini ni sawa sawa na kumzuia wa chini asilipwe vizuri kama yule wa juu anayelipwa vizuri.
 
habari wanandugu!

Nianze kwa kusema kuwa niipongeze serikali kwa nia nzuri iliyonayo ya kupitia na kupanga upya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi wa kada zote.

kwa muda mwingi tumeshuhudia kutofautiana kwa viwango vya mishahara kutoka fani Moja kwenda fani nyingine, mfano ualimu, afya, sheria, uhandisi n.k ambapo baadhi ya Kada wamekuwa wakilipwa mishahara mikubwa kuliko wengine ingawa ukiangalia majukumu na mazingira yao ya kufanyia kazi hayatofauti sana.

kutofautiana huku kwa mishahara kunapelekea baadhi ya wafanya Wa Kada Fulani kuwadharau wafanyakazi Wa kada nyingine, lakini pia no uharibifu Wa pesa kwani kama MTU yule yule (mwalimu) analipwa 20000 na naweza kuishi basi hata huyu mwingine (daktari) akilipwa 20000 ataweza kuishi na kutimiza mahitaji yake. sula hili siyo zuri

katika kuelekea kupanga mishahara upya serikali ifanye utaratibu Wa kulinganisha mishahara kwa wafanyakazi wote kwa kutegemeana na viwango vyao vya elimu. yaani wenye elimu ngazi ya shahada mshshahara wao ulingane, hali kadhalika ngazi ya diploma na cheti

by mkulima Wa nyanya

Lakini Mkuu kada nyingine wanatumika sana kwenye Kazi, muda mwingine wanafanya Kazi mpaka saa nne usiku. Naona pia wangeangalia majukumu ya kazi katika kada husika
 
Kuna vitu vingine vinachekesha kweli dunia mzima haupo huo utaratibu mtu na MMED yake ya neurology anachambua ubongo kama mchele amekaa darasani miaka 9 eti alipwe sawa na mwalimu wa civics form one, NONSENSE.
Ukiona sehemu wanalipa vizuri hamia huko.

ukubwa Wa mshahara hautegemei idadi ya miaka ya kukaa darasani, punguza ujinga. ingekuwa hivyo wanasheria mbona wanakaa miaka mitatu/minne darasani (ngazi ya degree) lakini wanapata mshahara mkubwa kuliko Wa hao madakatari wanaokaa miaka mingi darasani
 
angalia mwalimu anafanya kazi masaa mangapi kwa wiki linganisha na daktari af urudi utuambie vizuri

hoja yako haina mashiko! hebu niambie kati ya askari jeshi na hakimu nani anafanya kazi kwa Masaa mengi harafu nani analipwa mshahara mkubwa
 
mwalimu aliyepata div 3 au 4 akaungaunga na kupata degree alingane na pharmacist au ddaktari aliyepata div 1 six..kisa tu wote eti wana degree! ridiculous!

hahahahaha! kweli kati ya wale watu 4 wewe ndiye kichaa. yaani unataka mishahara ilipwe kwa kuangalia div aliyoipata MTU. hivi MTU aliyepata div 1 anazuiliwa kusma ualimu. lkn pia mbona hata upande Wa madaktari wapo wenye div. 3 au umekaririshwa
 
Haina haja ya kuweka debate kuhusu mshahara wa mwalimu
Ipo wazi kwamba walimu wanalipwa pungufu ukilinganisha na sekta nyingne

Au tunataka had TWAWEZA waje ku confirm

sina uhakika na hizi taarifa zako
 
Watu bwana. Mishahara haiwezi ikafanana hata siku moja. Engineer atazidi kulipwa mshahara mkubwa zaidi ya askari. Daktari atalipwa mshahara mkubwa zaidi ya mwalimu. Hivi nani anataka akasome miaka 5 na zaidi ili aje alipwe sawa na mtu aliyesoma miaka 3. Mwisho wa siku wale wanaotumia miaka mingi kusoma hawatakuwepo maana kunakuwa hakuna mantiki ya kupoteza miaka yote hiyo. Nani atataka akasomee udaktari kama kuna shortcut itakayokulipa sawa na daktari.

Daktari ambaye anahitimu masomo yake, atamkuta mwenzake aliyeenda kusomea kozi nyingine ameshamaliza Masters wanapoingia Mtaani.

Msiombe vitu visivyowezekana.
 
Mbona watu wanakwenda India kutibiwa?na kwa nn hawaendi kufundishwa "civics"?inawezekana madakitari wengi hawana mchango mkubwa kwa jamii,huenda pia wamekaririshwa tu
Tatizo la walimu hamujui munachokifanya, munatumikishwa sana njaa tu imewajaa,halafu mtu kupewa rufaa inategemea na utaalaamu na vifaa
 
Back
Top Bottom