Ndugu zangu Watanzania, nimeona nitoe maoni yangu machache tunapoelekea kutafuta Katiba mpya na Sheria bora za Uchaguzi. Mimi nilidhani tufanye yafuatayo:-
1. Kiundwe chombo cha kitaifa kitakachoongoza na kuratibu hii movement.
- Chombo hiki kitokane na angalau Watanzania wa makundi mbalimbali( Viongozi wa Dini, Viongozi wa kisiasa, Watanzania wasio na itikadi yoyote nk.)
2. Chombo hiki kianzishe movement ya kutafuta Katiba mpya na Sheria bora za Uchaguzi Tanzania na kuipa jina, mfano, Tanzanian Movement for Constitutional Reform(TAMOCORE)
3. Hiki chombo cha kitaifa kiunde chombo kama hiki kila Mkoa, Wilaya, Kata, Kitongoji, Kijiji/Mtaa nk.
4. Chombo hiki kitengeneze T-shirt na vipeperushi mbalimbali vinavyoelezea umuhimu wa Katiba mpya na Sheria bora za Uchaguzi.
5. Itolewe Elimu kwa Watanzania wote juu ya umuhimu wa Katiba mpya na Sheria bora za Uchaguzi.
- Elimu hii itolewe popote pale penye mikusanyiko ya watu, katika familia, katika nyumba za Ibada na hata kwa mtu mmoja mmoja.
6. Ifunguliwe Account maalum kwa ajili ya Watanzania na watu wote wenye mapenzi mema na Nchi hii ili waweze kuchangia gharama za uendeshaji wa movement hii.
Pamoja na yote, Watanzania wafundishwe kuwa mioyo ya uzalendo na ujasiri zaidi.
7. Ipangwe ratiba ya utekelezaji wa jambo hili na ifuatwe.
8. Kabla ya yote, chombo hiki kiende kwanza kukaa meza moja na watawala na kujadili kwa kina juu ya upatikanaji wa Katiba mpya na Sheria bora za Uchaguzi. Ikiwa watafikia mwafaka, kwa pamoja wapange ratiba ya utekelezaji wake na ifuatwe.
Lakini, bila kuwa tayari kujisacrifice kwa ajili ya jambo hili, kupata Katiba mpya na Sheria bora za Uchaguzi inaweza kuchukua miongo kadhaa mbeleni.
Kama nilivyosema, haya ni maoni yangu tu, kwa hiyo si lazima yachukuliwe yote. Yanaweza kuboreshwa, kuongezeka au hata kuachana nayo na kutafuta yaliyo bora zaidi.
Nawasilisha.