Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Mtu mmoja anamiliki line tatu mpaka nne na wengine mpaka sita kwa hiyo huenda hao wanaomiliki line nyingi wameamua kuzipunguza japo hii haiondoi ukweli kuwa wananchi wananyanyaswa kwa vile NIDA wameshindwa kazi yao

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja yako hujaiweka vizuri,mbona huwazi kwamba kati ya 53% ya line zilizosajiliwa kuna wengi waliosajilia ndugu na jamaa waliokosa vitambulisho ama wao wenyewe kusajili line zaidi ya moja?

Kwa hoja yako hio ni dhahiri pia hio 53% ya watu waliojisajili,sio wote waliosajili line moja kwa kila mtandao.
 
Kwa taarifa za tcra wamiliki wa simu Ni 21m line hai Ni 46m Ina maana kila mwenye simu alikuwa na line zaidi ya moja na 26m zimesha huishwa kwa vidole, kwa lugha nyingine Kuna mgomo baridi kila mtu kaamua kusajiri line moja na kutupa nyingine.
 
Watukatie tu
Nchi zingine za Afrika, zinapambana kuingiza pesa kupitia subscribers wao wanatupunguza. Wasubiri October tutawaonyesha uchungu wetu
 
Watukatie tu
Nchi zingine za Afrika, zinapambana kuingiza pesa kupitia subscribers wao wanatupunguza. Wasubiri October tutawaonyesha uchungu wetu
Utawala wa ccm ndiyo utawala unaowaumiza kasakologia Raia wake
 
Nashindwa kuelewa. Ina maana ofisi za NIDA zitafungwa? Naona ni amsha amsha watu wakasajili.


Hili zoezi nionavyo mimi linapaswa liwe endelevu ila muda uliotolewa ilikuwa watanzania wengi wajisajili.

Kuwatambua raia ina faida nyingi mno kwa nchi kiulinzi na usalama na mambo mengine ya kitakwimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa NIDA nashauri watume majina na namba za wananchi ambao wameshajaza form na hawajapata namba zao ili mitandao ya simu (MNO) wasiwafungie kwa sababu hawana hatia.
Hii naona imefanyiwakazi mapema sana ujumbe wa simu umeingia ingawa wengine tulishachukua vitambulisho vya NIDA miaka sasa.
 
Tatizo ni NIDA adhabu anapewa Mwananchi! Serikali inayo endesha mambo kwa kukurupuka utadhani Taifa hili ni changa limeanzishwa miaka ya hivi karibuni!
Kwani wameshafunga? Lawama za nini? Kama ni kuwahamasisha tu wananchi watafute hivyo vitambulisho kwa kutambua uvuvi wao na umuhimu wa kuwatambua wananchi kitaifa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
line zitafungwa na mauzo ya line mpya yataongezeka pia, hakuna mwananchi atakayekubali kuishi bila mawasiliano ya simu, itakuwa ni kawaida kuona mtu kajisajir kwa line 5 au sita lkn yeye anatumia 2 au 3 tu, nyingine kawapa ndugu zake.
 
Kwa serikali hii inavyopenda kupika data usishangae ukaambiwa mapato yameongezeka baada ya watu kusajili laini zao kwa alama za vidole...kivipi basi muulize polepole

Sent using Jamii Forums mobile app
Na ukiona mtawala anakomalia sheria flani ipite jua kuna jambo mbele,mim siamini kama ni ishu ya uharifu tu.
 
Ondoa shaka matokeo ya uchaguzi 2015, yalikuwa ya kupika, mpaka wale waliojiandikisha kupiga kura, hivyo tutapika tena, na ndio maana tunaanza kwa kupiga idadi ya mandondocha sorry idadi ya wanaccm, ili upishi wetu huko mbele uwe rahisi, nazani utakumbuko hivi karibuni msemaji wa mandondocha polepole alitoa idadi kuwa ni 15m, na bado mandondocha wapya wanaendelea kuletwa na upepo wa kisurisuri, hivyo ndondocha mwenzangu ondoa hofu, maana tiss,jwtz, police viko upande wetu tutafanya kama serikali za mitaa.

Halafu nikupe zilizo ndani ya red carpet ni kwamba viongozi wa upinzani watakuwa jela kabla ya uchaguzi mkuu ujao hivyo tutakuwa peke yetu, si unajua boss kubwa huwa hataki kushindanishwa na mtu yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona mnadanganyana hahahaha mlikuwa wapi siku zote? NIDA kuna shida lakini watanzania tuna shida zaidi,,,,, kuna namba nyingi sana zimeshatoka lakini hadi leo hazijasajiliwa ,,,,,,,,
Umeongea kama uko kijiweni. Inamaana kazi ya namba ya kitambulisho ni kusajili laini pekee? Waliochukua vitambulisho kabla ya zoezi la usajiri na kuondoka nchini, waliofariki, wasiotumia simu, hawa mtalazimisha wawe wamesajili line za simu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…