Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Mtu mmoja anamiliki line tatu mpaka nne na wengine mpaka sita kwa hiyo huenda hao wanaomiliki line nyingi wameamua kuzipunguza japo hii haiondoi ukweli kuwa wananchi wananyanyaswa kwa vile NIDA wameshindwa kazi yao

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja yako hujaiweka vizuri,mbona huwazi kwamba kati ya 53% ya line zilizosajiliwa kuna wengi waliosajilia ndugu na jamaa waliokosa vitambulisho ama wao wenyewe kusajili line zaidi ya moja?

Kwa hoja yako hio ni dhahiri pia hio 53% ya watu waliojisajili,sio wote waliosajili line moja kwa kila mtandao.
 
Huu ni mtizamo wangu ambao nauleta kama tahadhari kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) juu tukio la kionevu ambalo Watanzania wanalipigia kelele lakini mamlaka zinatumia ubabe kulitekeleza.

Kwa mujibu wa TCRA, kesho kutwa ndio hatma ya line takribani milioni 20 za Watanzania kuwa hewani kwa kile kinachodaiwa kutokuwa na usajili wa alama za vidole.

Kwa mujibu wa TCRA mpaka juzi ni 53% tu ya line za simu kati ya line zote ndizo zilizosajiliwa kwa alama za vidole hivyo kitakwimu ni kama nusu ya watumiaji wa simu line zao zitafungwa mpaka watakapokamilisha taratibu.

Ningependa niwakumbushe chama changu pendwa CCM kwamba idadi ya watu ambao haijasajili line za simu kama wataamua kulipiza kisasi kwenye uchaguzi ujao kwa uonevu wakuzifunga line zao ni dhahiri uchaguzi utakuwa mgumu.

Nawakumbusha uchaguzi mkuu 2015 idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura ni 23,253,982 na idadi ya waliojitokeza kupiga kura kote bara na visiwani ni watu milioni 15.6.

Watu watakaofungiwa line za simu kwa makadirio ni takribani watu milioni 20, hivi hamuoni kwamba hili ni hatari hasa kwa mwaka wa uchaguzi kama huu?

CCM tambueni hili zoezi Watanzania mnaowatetea (wanyonge) ambao ndio wapiga kura ndio wahanga wakubwa kwani wengi wapo vijijini ambapo hizi huduma hazipo.

Watu wamepoteza muda wao tangu awali zoezi hili lilipoasisiwa mwaka 2014 wamehangaika na vitambulisho hivi pasipo mafanikio, wapo ambao wamediriki hata kuuza mifugo kama kuku ili kupata nauli za kwenda wilayani (NIDA) ili tu walau kupata hizo namba za NIDA lakini mpaka leo hawajazipata.

Hii dhana kwamba wananchi walipuuza hili zoezi mwanzoni sio kweli kwani sisi ndio wananchi, wapo wengi wamejitokeza mwanzoni kabisa 2014 lakini hawajapata vitambulisho, watu wamerudia tena na tena lakini hawa NIDA ni tatizo.

Tusijiamini eti tu kwasababu ya miradi kama Stiglers, ununuzi wa ndege. Hii idadi ya watu wanaoenda kuonewa tarehe 20 kwa uzembe wa NIDA inaweza kabisa ikawa tatizo uchaguzi ujao.

Watanzania hawakatai kujisajili ila ni vema wakawekewa mazingira wezeshi ili wajisajili.

SMS sent & delivered
Kwa taarifa za tcra wamiliki wa simu Ni 21m line hai Ni 46m Ina maana kila mwenye simu alikuwa na line zaidi ya moja na 26m zimesha huishwa kwa vidole, kwa lugha nyingine Kuna mgomo baridi kila mtu kaamua kusajiri line moja na kutupa nyingine.
 
Watukatie tu
Nchi zingine za Afrika, zinapambana kuingiza pesa kupitia subscribers wao wanatupunguza. Wasubiri October tutawaonyesha uchungu wetu
 
Adjustments.JPG
 
Watukatie tu
Nchi zingine za Afrika, zinapambana kuingiza pesa kupitia subscribers wao wanatupunguza. Wasubiri October tutawaonyesha uchungu wetu
Utawala wa ccm ndiyo utawala unaowaumiza kasakologia Raia wake
 
Nashindwa kuelewa. Ina maana ofisi za NIDA zitafungwa? Naona ni amsha amsha watu wakasajili.


Hili zoezi nionavyo mimi linapaswa liwe endelevu ila muda uliotolewa ilikuwa watanzania wengi wajisajili.

Kuwatambua raia ina faida nyingi mno kwa nchi kiulinzi na usalama na mambo mengine ya kitakwimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa NIDA nashauri watume majina na namba za wananchi ambao wameshajaza form na hawajapata namba zao ili mitandao ya simu (MNO) wasiwafungie kwa sababu hawana hatia.
Hii naona imefanyiwakazi mapema sana ujumbe wa simu umeingia ingawa wengine tulishachukua vitambulisho vya NIDA miaka sasa.
 
Tatizo ni NIDA adhabu anapewa Mwananchi! Serikali inayo endesha mambo kwa kukurupuka utadhani Taifa hili ni changa limeanzishwa miaka ya hivi karibuni!
Kwani wameshafunga? Lawama za nini? Kama ni kuwahamasisha tu wananchi watafute hivyo vitambulisho kwa kutambua uvuvi wao na umuhimu wa kuwatambua wananchi kitaifa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
line zitafungwa na mauzo ya line mpya yataongezeka pia, hakuna mwananchi atakayekubali kuishi bila mawasiliano ya simu, itakuwa ni kawaida kuona mtu kajisajir kwa line 5 au sita lkn yeye anatumia 2 au 3 tu, nyingine kawapa ndugu zake.
 
Kwa serikali hii inavyopenda kupika data usishangae ukaambiwa mapato yameongezeka baada ya watu kusajili laini zao kwa alama za vidole...kivipi basi muulize polepole

Sent using Jamii Forums mobile app
Na ukiona mtawala anakomalia sheria flani ipite jua kuna jambo mbele,mim siamini kama ni ishu ya uharifu tu.
 
Ondoa shaka matokeo ya uchaguzi 2015, yalikuwa ya kupika, mpaka wale waliojiandikisha kupiga kura, hivyo tutapika tena, na ndio maana tunaanza kwa kupiga idadi ya mandondocha sorry idadi ya wanaccm, ili upishi wetu huko mbele uwe rahisi, nazani utakumbuko hivi karibuni msemaji wa mandondocha polepole alitoa idadi kuwa ni 15m, na bado mandondocha wapya wanaendelea kuletwa na upepo wa kisurisuri, hivyo ndondocha mwenzangu ondoa hofu, maana tiss,jwtz, police viko upande wetu tutafanya kama serikali za mitaa.

Halafu nikupe zilizo ndani ya red carpet ni kwamba viongozi wa upinzani watakuwa jela kabla ya uchaguzi mkuu ujao hivyo tutakuwa peke yetu, si unajua boss kubwa huwa hataki kushindanishwa na mtu yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona mnadanganyana hahahaha mlikuwa wapi siku zote? NIDA kuna shida lakini watanzania tuna shida zaidi,,,,, kuna namba nyingi sana zimeshatoka lakini hadi leo hazijasajiliwa ,,,,,,,,
Umeongea kama uko kijiweni. Inamaana kazi ya namba ya kitambulisho ni kusajili laini pekee? Waliochukua vitambulisho kabla ya zoezi la usajiri na kuondoka nchini, waliofariki, wasiotumia simu, hawa mtalazimisha wawe wamesajili line za simu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom