Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Jana nimetaka kumtumia pesa fundi wangu. Kabla sijaconfirm, naona jina linatokea la kike. Baada ya kusitisha zoezi na kumcheki akaniambia nitume tu bila hofu maana ametumia ID ya mkewe kusajiri line.

Cases za namna hii zipo nyingi kwa sababu watu hawakuwa na choice. Hii National ID haina maana sasa na in essence wameigeuza kuwa ID ya kusajiri line. Kuna vijiji vingi wenye IDs ni wa kutafuta kwa tochi na hawajui watazipata wapi/lini

Rais hakupaswa kuliingilia zoezi hili kisiasa namna ile. Tukiendelea namna hii ipo siku hata Banks zitaambiwa kila mtu apeleke ID yake ya NIDA otherwise account inafungwa
 
NIDA sio kuchukua namba au kujisajiri lazima watambue kama una uhalali wa kupewa namba wengine si raia
Kama NIDA wanatambua wengine sio Raia,Serikali ilipaswa kuliangalia hilo mapema kwa kutoa muda wa kutosha ili kila Mwananchi mwenye sifa awe amepata namba au kitambulisho cha NIDA tayari kwa usajili wa Line za Simu! Sio hizi kukurupapara zinazoelekea kuharibu maana nzima usajili wa Line za Simu.
 
Kama mimi kitambulisho ninacho lakini nitasajili laini 1 kati ya nne kwasababu zitakuja niletea shida siku imepotea wakaja wakaìokota watu wakaifanyia matukio itakua noma bora nibaki na hakakamoja ntakatunza kama jicho!
 
Msiwe na hofu hawana mpango wa kuzima maana waziri nditiye baada ya kwenda kigoma juzi amebadilisha mawazo maana kumbe tatizo haliko kwa wananchi bali kwao serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…