Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kwani wameshafunga? Lawama za nini? Kama ni kuwahamasisha tu wananchi watafute hivyo vitambulisho kwa kutambua uvuvi wao na umuhimu wa kuwatambua wananchi kitaifa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo unamaanisha Mkuu wa Nchi alikuwa anatuongopea pale aliposema tarehe 20/01/2020 mwisho wa kusajili line za Simu?!
 
Pongezi zetu ziwafikie viongozi wa kiserikali kwa Maamuzi ya kuwatambua watanzania wote kupitia utoaji wa vitambulisho vya Taifa.

Mbali na yote kuna tangazo lililotolewa kuwa ifikapo tarehe 20/01/2020 simu(laini) ambazo zitakuwa bado hazijasajiliwa kwa mfumo wa alama za vidole zitazimwa.

Hakika mpango wa serikali ni mzuri lakini wananchi wengi hatujapata namba zetu za NIDA hivyo tutahukumiwa kwa kosa ambalo sio letu. Baadhi ya Wananchi kila kukicha tunafuatilia namba zetu kupitia mifumo iliyotolewa hadi kwenye ofisi za NIDA lakini zinaibuka sababu mbalimbali ikiwemo kutakiwa kurudia na tunafanya Kama maelekezo yanavotolewa, Je tunastahili kuadhibiwa?

OMBI
kwakuwa serikali ni moja na taasisi zote zinazohuska ziko chini ya serikali hiyohiyo niombe taasisi hizi ziwasiliane na pale mtakapojiridhisha kuwa wote waliojiandikisha kabla ya tarehe 20/01/2020 namba zao (NIN) zimeishakamilika na kuwekwa mtandaoni hapo ndo mzime laini ambazo hazijakamilisha usajili.

"Mungu ibariki Tanzania,"



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niwaulizeni nyie mnalalamikia NIDA TCRA hivi NIDA wanamiaka ngapi toka waanze kutoa vitambulisho.TCRA nao wana muda gani toka waanze kutuhimiza tukasajili line zetu.

Wasilaumiwe makosa ni yetu wananchi kila jambo tunadharau ata mombo ya msingi tunaleta dharau mie nimejiandikisha miezi ya nyuma huko na famila yangu baada ya muda mchache tumchuka namba.au toka miaka yote mlikua amjafikisha miaka 18 sasa ndio mmefikisha hiyo miaka.

Acheni lawama kwanza TCRA wametuvumia sana Chekini mnavyopanga mafoleni mtasema mnasubiria Mwendo Kasi Kimara.WAZIME LINE MSAJILI ZINGINE MLIYATAKA WENYEWE
Wewe hujitambui na wala huwajui Viongozi wako jinsi walivyo wakurupukaji! Mfano Mkoa wa Kigoma walisajiliwa na NIDA tangu mwaka jana.Wiki iliyo pita ndo wameanza kutoa namba za NIDA na kwa baadhi ya Watu wachache! Wenye makosa hapo ni Wananchi au ni wenye Mamlaka?!
 
Kwanza maisha ni magumu, halafu wewe unaongeza ugumu kwa kufunga laini za simu.

Wapiga kura wako, wengi wapo vijijini na hawajawahi kupata namba za NIDA. Octoba wanaenda kukuchinjia baharini (au una plan B ya kushinda?)

Unaenda kuvunja mahusiano ya watu, kuzuia miamala yote ya fedha na kujenga chuki kati yako na wananchi.

Ulitakiwa kuwawajibisha viongozi wa NIDA wala si wananchi. Nyota yako inazidi kufifia. Kwanini kila unachogusa kinafeli?

Je, mbona mnakomalia namba, tutaishia kupata namba tu bila vitambulisho?

Tarehe 20 ni usiku huu, lets wait and see.
Sisi tupo huku vijijini na tumesajili line zetu kwa namba za NIDA. Poleni sana wazee wa ' HIYO PESA TUMA KWENYE NAMBA HII' Tafuteni kazi zingine za kufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wale wenye wasiwasi na vijana wanaopita mitaani kuwasajilia laini zaidi ya moja unaweza kwenda Mtandao husika ukaomba wakuonyeshe laini zako zote zilizotumia kitambulisho chako ambazo huzitambui wanazicancel nimeona Hayo ktk Mtandao WA airtel
Hili ni jambo zuri sana .
 
WhatsApp kinachotumika ni internet namba yako utambulisho tu ndio maana unaona mtu yupo Ulaya ila anatumia utambulisho wa namba yake ya voda au tigo utashindwa kuiupdate kwa sababu namba za kuverify wanakutumia kwenye namba ya utambulisho
Asante kwa ufafanuzi mzuri.
 
Wewe hujitambui na wala huwajui Viongozi wako jinsi walivyo wakurupukaji! Mfano Mkoa wa Kigoma walisajiliwa na NIDA tangu mwaka jana.Wiki iliyo pita ndo wameanza kutoa namba za NIDA na kwa baadhi ya Watu wachache! Wenye makosa hapo ni Wananchi au ni wenye Mamlaka?!
Achana nae huyo mkuu! Ni limbukeni tu,anahisi kupata kitambulisho cha NIDA ndo kuyapatia maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi tupo huku vijijini na tumesajili line zetu kwa namba za NIDA. Poleni sana wazee wa ' HIYO PESA TUMA KWENYE NAMBA HII' Tafuteni kazi zingine za kufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya ni majibu ya akili za nzi kucheza na uchafu. Angekuwa na akili angetengeneza asali. Nchi inahitaji muda zaidi kujisajili. Line zikizimwa kesho wanyonge wengi wataumia. Mm nimeshasajili ila najua kwa muda uliowekwa ni ngumu nchi zima kuwa imesajili.
 
Back
Top Bottom