Kuelekea maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha Hayati JP Magufuli

Kuelekea maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha Hayati JP Magufuli

1.Amechangia Kwa kiasi kikubwa sanaaa kupunguza foleni jijini Dar,ule mradi wa mwendo kasi na kupanua njia za katikati ya mji kulileta ahueni kubwa sanaa.

2. Amesaidia sanaa kurahisisha huduma za afya katika mikoa yote nchini kupatikana Kwa urahisi kwa kuhakikisha hospital nyingi za mkoa zinakua na hadhi ya rufaa na wilaya kupanda kuwa mkoa. Majengo mengi yalijengwa na vifaa vingi kununuliwa.

3. Alisaidia kuimarisha mifumo mbalimbali ya ulipaji kodi nchini iliyosaidia mapato ya nchi kuongezeka zaidi.

Wengine wataongezea mengine,kikubwa tutambue kuwa ameisaidia sanaa nchi kuvuka salama katika kipindi kigumu Sana cha UVIKO,pia alijitahidi sanaa kuwa sehemu ya sauti kwa wasio na sauti(wanyonge).

Alipendwa na wengi,lakini pia alichukiwa na wengi, MUNGU ampumzishe kwa amani...
 
Unadhani kama umeumizwa wewe hakuna aliyeumizwa but still ndiye nilikuwa napiga kelele nchi ipate komando, asiye cheka cheka, jasiri nk.

Hatimaye mlipolia na Mungu mkasema amesikia kilio cha Watanzania wengi, mpaka wapinzani mlilia apatikane like him, baadaye JK akawaambia mliyemtaka huyo hapo.

Leo mnakejeli, ooh kakaza, ooh hatupumui, ooh hafai, Mungu mchukue, mmh!.

Although maendeleo siyo lelemama, kuna wkt lazima uumie ili kizazi kijacho kije kiseme hakika babu waliumia, ndiyo maana babu zako walifanyiwa unyama mkubwa na kuzurumiwa vingi ikiwemo uhai ila leo unasoma kwenye history na kula bata, hujui madhira aina gani yaliwakuta.

👉🏾 Naendelea kujifunza tabia ya binadamu.
 
Back
Top Bottom