Kuelekea maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha Hayati JP Magufuli

Kuelekea maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha Hayati JP Magufuli

1.Amechangia Kwa kiasi kikubwa sanaaa kupunguza foleni jijini Dar,ule mradi wa mwendo kasi na kupanua njia za katikati ya mji kulileta ahueni kubwa sanaa.

2. Amesaidia sanaa kurahisisha huduma za afya katika mikoa yote nchini kupatikana Kwa urahisi kwa kuhakikisha hospital nyingi za mkoa zinakua na hadhi ya rufaa na wilaya kupanda kuwa mkoa. Majengo mengi yalijengwa na vifaa vingi kununuliwa.

3. Alisaidia kuimarisha mifumo mbalimbali ya ulipaji kodi nchini iliyosaidia mapato ya nchi kuongezeka zaidi.

Wengine wataongezea mengine,kikubwa tutambue kuwa ameisaidia sanaa nchi kuvuka salama katika kipindi kigumu Sana cha UVIKO,pia alijitahidi sanaa kuwa sehemu ya sauti kwa wasio na sauti(wanyonge).

Alipendwa na wengi,lakini pia alichukiwa na wengi, MUNGU ampumzishe kwa amani...
acha uzwazwa wewe mradi wa mwendokasi hakuuanzisha yeye aliukuta , jamaa ukitaka mkujua lilikua binafsi halikuanhata linataja mambo ambayo aliyakuta akayaendeleza kidogo , alijifanya yote ni juhudi zake, selfish kabisa
 
Sawa, mtu kama mimi nashukuru Mungu alifanya vizuri kumuondoa ili tulioumizwa tupone na tumepona kwa 100%.
Kifo sio adhabu.
Ila na wewe ulitaka Magufuli afanyaje? Uliacha kazi toka 2012 ukaendelea kulipwa mshahara, alivyoingia yeye akafanya uhakiki akasitisha kwa wote mlioacha kazi. Hapo kakutesaje?
Screenshot_20220218-124419_1.jpg
 
Hatatokea rais mwenye mamlaka kama JPM wengine wapo Kwa maslahi ya matumbo yao wenye akili zao wako kimya na siku zote mtu mwema huwa haishi yeyote anayesaidia watu maisha yake huwa mafupi hebu angalia uhalisia tunakoishi wale wanaotusaidia ndo Mungu anawaita WATANZANIA TUMEPOTEZA ALMASI UKWELI NDO HUO R. I. P JMP
 
Nasema moja la JPM kwa sasa kiongozi akiahidi kitu ni ngumu kupotezea atahojiwa mpaka akome sio kama zamani jambo linapita juu juu.

Midomo yake iliahidi ambayo kweli yalitokea hata kama hayajaisha au kufanywa kabisa lakini kila mtu alitumaini na kujua kweli litatokea .

Daima alikua mkweli kwa asilimia 75% hizo 25 % ni kwa sababu hawezi ishi kama malaika ila alitutia matumaini makubwa kipindi cha corona siwezi sahau kamwe.

"Tulianza na Mungu na tukamaliza na Mungu."

kwa project zake alizozianzisha angekuta zimefanyika Tanzania ingekua mbali sana kwa speed yake tathimini zilikua ifikapo 2035 tutawafikia kenya au kuwapita.
 
Ulizungumza na Mungu lini akakuambia alisikia kilio cha Watanzania?
Unadhani kama umeumizwa wewe hakuna aliyeumizwa but still ndiye nilikuwa napiga kelele nchi ipate komando, asiye cheka cheka, jasiri nk.

Hatimaye mlipolia na Mungu mkasema amesikia kilio cha Watanzania wengi, mpaka wapinzani mlilia apatikane like him, baadaye JK akawaambia mliyemtaka huyo hapo.

Leo mnakejeli, ooh kakaza, ooh hatupumui, ooh hafai, Mungu mchukue, mmh!.

Although maendeleo siyo lelemama, kuna wkt lazima uumie ili kizazi kijacho kije kiseme hakika babu waliumia, ndiyo maana babu zako walifanyiwa unyama mkubwa na kuzurumiwa vingi ikiwemo uhai ila leo unasoma kwenye history na kula bata, hujui madhira aina gani yaliwakuta.

[emoji1485] Naendelea kujifunza tabia ya binadamu.
 
Kaacha kazi mwenyewe, akaendelea kulipwa mshahara.kaingia Magufuli uhakiki ulivyofanyika mshahara ukasitishwa. Alafu anasema aliteswa. Sasa Magufuli hapo kosa lake nini?
View attachment 2122833
Hawa pamoja na wale wapiga dili na wenye vyeti fake ndo wanaomchukia kwakua maslai yao binafsi yaliguswa...
Unakuta mtu analipwa mshahara serikalini ila kaajiriwa kwenye NGo's...or Mwingine yupo Masomoni ila still analipwa mshahara...
Unalipwaje hela ambayo hukuifanyia kazi?hizi mambo zilipopigwa stop watu wakaanza chuki...wezi to the point wanaona ni haki yao kuiibia serikali...
Km hukua na connection ya upigali i bet your life na la mzee hazikuwahi ku cross,so huwezi kua na chuki.
 
Back
Top Bottom