Kuelekea Mechi ya Ngao ya Jamii August 13, 2022

Ety utabiri,, wewe umekuwa nani kwanza una uspecial gani, uliwahi tabiri jambo gani la maana.. toa hizo tongotongo.
Yanga inajishape kithamani..Kolo imejaza uwanja kwa buku 3, 3 Ila kwenye mapato tumewazidi mara dufu.. We are citizens... Hakuna kolo litajilinganisha kwetu.. Timu tunayo kama unabisha save my comment then uje ui-revive Saturday after game
 
Nyie tulieni acheni porojo nyingi za kujifurahisha yanga ameweka mtego mkali sana kwa simba baada ya kufungwa jumamosi, Simba wataingia kichwa kichwa wakidhani wanaiweza yanga sasa kitakachotokea watasimulia, kwa tathmini ya kawaida tu yanga bado ina timu bora zaidi ya simba kiufundi, hili simba aupate ubora wa yanga anatakiwa kufanya kazi ya ziada mara 2 zaidi, kuanzia muunganiko mpaka kwa mchezaji mmoja mmoja, kutengeneza muunganiko wa timu sio suala jepesi Kama mnavyofikiria na matokeo dhidi ya st george ndo yamewalevya kabisa na kuona wamemaliza kila kitu, kiufundi kuna kazi ya ziada wanatakiwa waifanye vinginevyo wataonyeshwa kwa vitendo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] unaandika huku chozi linadondoka, woiiiiiih poleeeeeeeh
 
Game ya simba na yanga haitabiriki hata kama mmoja ni mbovu.

Niliwaona yanga vs vipers sijaona kama wana ubovu kiasi hicho, kufungwa ni matokeo tu ya mchezo.

Mimi simba, napenda kuona chama langu likishinda lakini siwezi kuwakosea adabu yanga kuwa atafungwa kirahisi, yanga anaemdeleza alipoishia msimu uliopita ambao alikuwa vizuri.
 
Huwezi kuongea haya kama si shabiki wa mpira. Hongera umejitofautisha na Washangiliaji.
 
Mechi hiyo haitakua na maajabu ni kama hizi mechi mbili zilizopita...bado muunganiko na kuchangamka kwa wachezaji..tukubalini matokeo yeyote yatakayotokea
Mechi nzuri itakua oktoba 23

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
wewe mganga feki rudisha kuku wa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…