Kuelekea Mei mosi 2022 tunaomba Rais Samia tusaidie hili kuhusu CWT

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
Raisi wa awamu ya Tano Ndugu John Magufuli alijaribu kuanzisha hili Jambo kwa kuonesha namna viongozi wa CWT (chama Cha walimu Tanzania) wanatumia michango ya wanachama na rasilimali kujinufaisha wenyewe na wakiendelea kuwanyonya walimu ,

Chama hiki hakina msaada wowote kwa walimu Tanzania Zaidi ya kukata 2% tu,

Binafsi naomba Raisi Samia atusaidie Jambo hili
Aagize Makato ya 2% kusimamishwa na viongozi wasimamishwe na watoe wazi mchanganuo wa mapato na matumizi.

Walimu watakaotaka kukatwa hiyo 2% wenyewe waandike barua kwenye halmashauri zao wajiunge kwa upya..

Walimu ambao hawatahitaji kujiunga Tena na CWT warudishiwe angalau nusu ya pesa zao Toka walipoanza kuchangia chama.

Mwisho Kupitia wizara ya Utumishi isikubali mwalimu kukatwa 2% kwenye mshahara wake bila ridhaa
 
Usitegemee msaada wowote ule kutoka Serikali ya CCM! Maana hiyo CWT ni tawi la CCM! Hivyo siku zote lao ni moja! Ufisadi na upigaji.
 
Nikiwafikiria hawa jamaa CWT hua naona vituko sana kiukweli hawana msaada wowote nasisitiza wowote kwa Mwalimu maana hivyo vijihuduma ambavyo huwa wanazuga kutoa ni upuuzi mtupu Mama kama huwa unapitia au kuna wasaidizi wako wanasoma hii comment nnaomba basi wapitishe hata form za maoni mashuleni kujiridhisha ni kwa kiasi gani waalimu hawana haja na hiki Chama kila Mwalimu analaumu yaani mtu unakatwa karibu 20elf kwa mwezi malipo yako ni tshrt yenye ubora wa kiwango cha chini sometimes bila kujali hata size ukichelewa unakutana na dela na ndio maana hiyo mitshrt unaona imezagaa kwa wachungaji wa mifugo na wakulima wa kiwango cha chini kabisa kama ni mijini basi bodaboda and other local peoples whats a Shame to Tanzanian Teachers [emoji848] Mama tunakuomba tuondolee CWT wanatuibia mno

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Cwt ni tawi la kijani kama ilivyo uvc...lao ni moja kuwakamueni walimu mpaka tone la mwisho la damu.

#MaendeleoHayanaChama
Yaani wewe jamaa naona akili yako Kama inafanana kabisa na emoj uliyoweka
 
Nikiwafikiria hawa jamaa CWT hua naona vituko sana kiukweli hawana msaada wowote nasisitiza wowote kwa Mwalimu maana hivyo vijihuduma ambavyo huwa wanazuga kutoa ni upuuzi mtupu Mama kama huwa unapitia au kuna wasaidizi wako wanasoma hii comment nnaomba basi wapitishe hata form za maoni mashuleni kujiridhisha ni kwa kiasi gani waalimu hawana haja na hiki Chama kila Mwalimu analaumu yaani mtu unakatwa karibu 20elf kwa mwezi malipo yako ni tshrt yenye ubora wa kiwango cha chini sometimes bila kujali hata size ukichelewa unakutana na dela na ndio maana hiyo mitshrt unaona imezagaa kwa wachungaji wa mifugo na wakulima wa kiwango cha chini kabisa kama ni mijini basi bodaboda and other local peoples whats a Shame to Tanzanian Teachers [emoji848] Mama tunakuomba tuondolee CWT wanatuibia mno

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Kwa taarifa za chini chini eti mwaka huu hizi dela/t-shirts zitatolewa kwa mkoa sherehe za kitaifa zitafanyika tu. Nasubiri nihakikishe, ili nijue wajanja wamesha kula 2% yangu!
 
Ni kweli kabisa,Dodoma ndio mkoa pekee walimu watapewa tisheti.
 
T shirt 👕 tulikuwa tunawapa hamvai mnagawa kwa shamba boy wenu dada wa kazi Sasa mnataka T 👕 za nini wakati huwa hamzivai
 
CWT ni chama Onevu kwa Waalimu wa Tanzania hii, haina msaada wowote kwao.

Inawachuna tu pesa.
 
Kama hukujaza form inaitwa TUF 16 kuruhusu hao wanaokukata fedha wafanye hivyo basi una kila haki ya kuwashtaki kwa kuingilia mshahara wako bila idhini yako..
 
Unajua kitu kinaitwa ADA YA UWAKALA kinachopatikana kwenye Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ya mwaka 2004?
 
hivi kwa Nini CWT isiimarishe benki ya walimu isiyo na masharti meengi,na wakawa wanatoa mikopo kwa riba nafuu zaidi kwa walimu,badala ya kuwaacha walimu wana zi vagaa benki ambazo zinakamua walimu kwa riba kubwa?
 
poleni sana watumishi[emoji26]
IMG-20220421-WA0013.jpg
 
Kwa taarifa za chini chini eti mwaka huu hizi dela/t-shirts zitatolewa kwa mkoa sherehe za kitaifa zitafanyika tu. Nasubiri nihakikishe, ili nijue wajanja wamesha kula 2% yangu!
Wanaboa kinoma hawa jamaa na wamewapanga maafisa utumishi mtu asijiengue kwenye kikaango

Back
Top Bottom