Kuelekea mkutano mkuu wa CCM Taifa, natamani kuona uongozi mpya wenye ushawishi

Kuelekea mkutano mkuu wa CCM Taifa, natamani kuona uongozi mpya wenye ushawishi

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Amani iwe nanyi,

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema, amani, upendo, umoja na mshikamano kwa taifa letu. Ni mengi makuu Mungu ametenda maishani mwetu kustahili shukrani kuu. Pia, nakipongeza CCM kwa kudumisha utamaduni wa kuandaa chaguzi za kidemokrasia. Demokrasia ndio sifa kuu ya uwepo, ueneaji na ukuaji wa siasa za CCM.

Zikiwa zimebaki siku mbili kufanyika mkutano mkuu wa 10 wa CCM ,natumaini viongozi imara na wenye ushawishi watapatika. Nakipongeza chama kwa kufanikisha uchaguzi wa jumuiya ngazi ya taifa. Kilichonifurahisha jumuiya zote wamepatikana watu licha ya waliokuwepo kugombea kutetea nafasi zao lakini hawakufanikiwa.Hii ni ishara kwamba watu wenye ushawishi ndio wanahitajika.

Katika Uzi wangu wenye'title' CCM ni chama kikubwa lakini kimekosa viongozi wenye ushawishi nimejaribu kuonesha ni faida zipi watu hao wataweza kusaidia kuimarisha chama.

Tunapoelekea mkutano huo mkuu kama ilivyo mikutano mikuu ya jumuiya lengo lake ni uchaguzi na kutoa malengo ya chama. Ni matumaini yangu uchaguzi mkuu utatuletea watu safi na wenye ushawishi kwa nafasi zisizokuwa na kugombea.

Kama chuma cha mabadilko ya uongozi ndani ya jumuiya na chama na kuangusha baadhi ya miamba ,natamani kuona mabadiliko hayo yakifanyika pia ndani ya uongozi wa chama taifa .

Kwa nini natamani kuona mabadiliko?

Natamani kuona mabadilko ya uongozi ndani ya Chama kwa sababu ni kipindi ambacho zitaibuka na kuibuliwa hoja nyingi na wapinzani bila watu wenye uwezo wa kujenga hoja na ushawishi Chama kinaweza kupitia kipindi kigumu uchaguzi mkuu wa 2025.

Natamani kuona watu wapya ili kurekebisha makosa na kuziba mashimo yaliachwa na watangulizi wao.

Watu wenye ushawishi wa hoja watakisaidia chama kuvuka hususani kipindi hiki cha maridhiano.

Siku za nyuma niliwahi kuandika juu ya mtu anayeitwa Thobias Mwilapwa kupitia Uzi huu Thobias Mwilapwa apewe Ukatibu Mkuu wa CCM kwa uwezo wa ziada alionao ,mpaka sasa bado nina imani na uwezo alionao kwa nafasi hiyo

Nakitakia CCM mkutano mkuu mwema
 
Mkuu

Hata kinana awe mwenyekiti rasmi ni ngumu sana CHAMA kuwa na ushawishi zaidi ya polisi pekee!!

Mwendazake alijitahidi kubadili jina na kujiita yeye pia akaleta watu wapya kina Bashiru ili Angalau CHAMA kiwe na mvuto LAKINI UBADHIRIFU ulikita mizizi mno kiasi Kwamba hata jina lake halikufua dafu!!

Namna pekee ni kuzaliwa kwa CHAMA KIPYA ili kuleta sura mpya na mwelekeo mpya sio HUU wa sasa!!

CHAMA chetu kimekuwa kama zimwi hata umuingize mtu muadilifu kiasi gani atachafuka tu hata kwa zengwe na hatoweza kusafisha uchafu uliomo zaidi Sana mishipa yake ya Moyo itapasuka na tutampoteza!!

Tunataka CHAMA KIPYA kizaliwe tuwe na muelekeo mpya na maono mapya na kukizika kilichopo coz hakisafishiki hata kwa dawa!!

Naamini wenye Mamlaka wameona na watalifanyia kazi!

Mungu IBARIKI nchi yangu Tanzania
 
Mimi natamani kuona hiki chama kinatoweka kwenye utawala. Ni mzigo mzito sana kwa wananchi wa Tz
 
Nakipongeza sana Chama Cha Mapinduzi kwa usikivu wake kwa wanaotoa ushauri na mapendekezo ,ni matumaini yangu uongozi ulioteuliwa leo utaleta matokeo chanya kwenye uongozi wa Chama, serikali na Taifa.
 
Back
Top Bottom