Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
KUELEKEA SIKU 365 ZA MHE SAMIA, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Na Elius Ndabila
0768239284
2: UHUSIANO WA KIMATAIFA.
Baada ya kuangazia utulivu wa kisiasa kuelekea siku 365 za Mhe Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tutaitazama Tanzania katika uhusiano wa kinataifa.
Ifahamike kuwa nchi zote duniani zinategemeana kwa namna moja au nyingine. Nchi yoyote ikiamua kuvunja mahusiano na kuamua kujifungia inakuwa sawa na binadamu kujichoma sindano ya sumu. Huyu binadamu anakuwa anasubiria kufa tu. Lakini Taifa lolote linaloimalisha mahisiano na mataifa mengine ya nje ni sawa na binadamu ambaye anagundua maradhi yake na kuamua kumuona dakitari.
Sera ya Tanzania tangu kupata uhuru ni kuendelea kushirikiana na nchi zingine duniani. Mahusiano haya ya kimataifa ndiyo yanayotengeneza dipolomasia ya Uchumi Duniani. Nchi zote duniani zinazofanya vizuri katika sekta ya maendeleo basi tafsiri yake nchi hiyo ipo vizuri katka uhusiano na nchi zingine.
Uhusiano huu wa kidplomasia ni lazima ujengwe kibiashara. Tanzania tunahitaji masoko kwa ajili ya bidhaa zetu zinazozalishwa nchini lakini pia tunahitaji bidhaa zinazozalishwa kutoka nchi washirika.
Mhe Samia baada ya kuapishwa hotuba yake ya kwanza ilikuwa ni kuwa nitaifungua nchi. Rais Samia alimini kuwa nchi imefunguliwa, lakini haijafunguliwa Kwa kiasi ambacho kinatakiwa.
Kuna wakati Tanzania iliingia kwenye migogoro na baadhi ya mataifa na wakati mwingine na EU ambao wamekuwa mdaada mkubwa katika maendeleo ya Tanzania.
Ziara za Mhe Rais nje ya nchi zimerudisha Kwa kiwango kikubwa mahusiano yaliyokuwa yameanza kufifia. Na hivi karibuni Tanzania imeweza kupata mikopo ya riba nafuu kutoka mataifa hayo.
Ukweli ni kuwa hatuwezi kutegemea fedha za wahisani kuendesha nchi. Lakini ili kujenga uchumi imara wa nchi tunazihitaji hizo fedha ili kuleta maendeleo. Jambo kubwa ni kuhakikisha hizo fedha zinatumika kama zilivyokududiwa ili miradi hiyo iweze kujizslisha na kulipa hayo madeni. Tunatakiwa kuijenga Tanzania ambayo bajeti ya nchi walau 75% iwe inategemea fedha yake kuliko ilivyo sasa.
Mhe Samia anajitahidi kufanya hivyo ili miradi ambayo tunakopea ijizalishe na kulipa. Serikali inapaswa kuwekeza zaidi kwenye Wizara ya kilimo. Wizara ya kilimo kama itapewa bajeti kubwa itasaidia kupunguza gharama za uzalishaji. Gharama za kuzalisha zikipungua nchi itazalisha sana na kuuza ziada nyingi nje.
Mafanikio makubwa kuelekea Mwaka mmoja wa Mhe Samia ni kuwa ameendelea kuiweka Tanzania katika kilele cha juu cha mahusiano na mataifa mengine. Taifa halina minyukano ya wazi na mataifa mengine.
Pamoja na mafanikio haya kuelekea Mwaka mmoja, ushauri wangu ni kuwa tunahitaji kuimalisha zaidi diplomasia ya uchumi. Uhusiano ni jambo Moja lakini faida kutoka na mahusiano hayo ni jambo lingine. Tanzania Kwa rasilimali tulizonazo bado ninaitazama kama nchi ambayo dipolomasia haijatusaidia. Bado Wizara yetu ya mambo ya nje kushirikiana na Balozi zetu hawaijaitendea haki Tanzania. Wameshindwa kuitangazia vizuri dunia juu ya vivutio tulivyonavyo. Utalii wa Tanzania ukitangazwa vizuri unaweza kuwa chanzo kizuri cha mapato.
Brazil ambayo ni ya kwanza kwa vivutio vya utalii Duniani kwenye ripoti yao ya mwezi wa pili wameingiza Dollars Million 700. Hizo fedha ni nyingi sana na uwingi huu unatokana na kuwa wamefanikiwa kuvitangaza vivutio vyao.
Ili ziara za Mhe Rais ziweze kufikia matamanio anayoyataka inatakiwa balozo zetu zifanye kazi kubwa. Wapunguze usingizi. Pamoja na kuwa Tanzania ni ya pili kuwa na vivutio lakini inazidiwa na nchi ambazo hazina vivutio Kwa kuwa na watalii wengi.
Msaidieni Rais kufungua nchi. Wenye wajibu huo wakimsaidia vizuri Kwa rasilimali tulizonazo tinaweza kujitegemea Kwa zaidi ya 75%.
Kazi kubwa aliyoifanya Mhe Rais ni kuhakikisha mahisiano yanaendelea kuwa vizuri huko nje, lakini wajibu wa wizara ya mambo ya nje ni kuhakikisha wanautumia mwanya huo kuitangaza Tanzania. Watu waje kutalii na kuwekeza.