Uchaguzi 2020 Kuelekea siku ya kupiga kura, Mzee Butiku apindua meza kibabe

Uchaguzi 2020 Kuelekea siku ya kupiga kura, Mzee Butiku apindua meza kibabe

Screenshot_20201016-161515.png
 
Mzee Butiki nae maslai yake yameguswa ndiyo maana analialia Sasa!! Apambane na hali yake!!
Hebu acheni upumbavu nyinyi. Yaani kila mtu atakayeongea tofauti dhidi ya Magufuli basi tayari maslahi yake yameuguswa au anatumika na mabeberu? Sijui akili zenu zitabadilika lini?
 
Hima hima asiye na mwana....muda mufaka umeshafika watanzania - huu ndiyo wakati mliousubirri ufike toka 1995... mabadiliko ya kweli kama mwalimu alivyotuachia wosia ndiyo haya sasa - wote kwa umoja wetu twende na Tundu Antipas Lissu. Kijana Msomi, Mzalendo, Mwerevu ... atatusaidia mengi mengi mno hasa kuuweka sawa huu muungano wetu na kuendeleza Katiba mpya alipoachia Jaji Warioba.

Naomba Mh. Rais Lissu wakati wa uzinduzi basi awepo na JK maana kwenye katiba hiyo ana JASHO lake jingi saana.

hawa wenzetu CCM wamejisahau mno, wanatawaa kwa mazoea - hawa wapumzike... watuache kwanza turudishe tunu ya taifa letu.. Tanzania si nchi ya kudharaulika kimataifa no no noo.
Naapa mabadiriko nayataka!!!! Lakini sio kwa kuongozwa na Lissu, hana kanuni na hii ya kudhani kuwapendeza Wazungu na kujitia maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya Baba wa Taifa, nasema hata kama atashinda na kuchukua dola tutakuja zungumza mengine. Sio mkweli, tunza haya!!

Naona nivute subira huku nikipiga kelele kurekebisha mzoga wangu mpaka itakapofika tukipata kiongozi wa kweli atakayetufaa. Tutampata tu..
 
Kumbeeeee uwoga husababishwa na ujinga.
Unaweza ukaona kisiki ukasema ni mchawi,asante mzee Butiku
Wakati mwingine kunguru mwoga huponyesha bawa lake. Wengi hawapendi hiyo hali. Umoja haupo. Yule jasiri aliyeupinga hadharani UDIKTETA UCHWARA, tuliona alichokipata.
Wale maarufu wa kutoa WARAKA mara kwa mara, inakaribia miaka mitano sasa wapo kimyaaaa!
Kinana, Nape, Makamba, Membe, viongozi wastaafu waliokuwa WANAWASHWA MIDOMO, ni mashahidi wa mazingira yalivyo! Hatuna umoja wa kulikabili HILI DUDE!
 
Watz sio waoga ni kwamba walikosa mtu jasiri makini Lisu, thus ccm imekuwa ikiwaburuza. Sasa wapo tayari, Lisu amewekewa damu ya Kenya ameoondolewa damu ya uoga, kupitia damu yake ukombozi umefika.
Mateso tena Basi,
Umeniudhi tu kwa hiyo "damu ya Kenya"; bila hiyo andiko lako lilikuwa zuri sana.
Hata hivyo, nadhani umejichanganya bila kujua kwani ulianza vizuri tu kwa kuandika "Watz sio waoga..."
 
Mzee anaulizwa swali juu ya chanzo cha uwoga, anatoa sababu nyepesi kweli bila kuangalia kwa kina mila, desturi, na government systems.
Kama ni ujinga mbona mpaka ma-profesa wameshikwa na woga? Au alikuwa anamaanisha 'upumbafu'?
Maprofesa wa Tz ni wanjinga tu, kama profesa analala kwenye ofisi za chama huu siujinga
 
Tatizo kubwa linalotuathiri watanzania tukiacha uoga ni UNAFIKI. Mtanzania kaumbwa na unafiki wa kusifia jambo hata kama linamkera. Endapo kungetokea watu toka siku ya kwanza ya Dkt. Magufuli kuingia madarakani na kufanya mambo ya kinyume na katiba ilipaswa walio karibu yake wazungumze.

Lakini walimpigia makofu huku wakisonya pembeni. Hii ilipelekea kuamini kuwa anachofanya ni sahihi na kuwa hakuna anaeweza kumhoji. Unafiki wetu watanzania ulihalalisha kukandamizwa kwetu kupelekea kufika tulipofika leo.

Bw. Magufuli ni muendelezo wa mfumo ambao ulishawekwa na waasisi wake, mfumo uliojengwa kwa unafiki na nidhamu ya uoga.

Hapa ndipo yalipo makazi ya Jane Lowassa Crimea Bia yetu na barafuyamoto unafiki uliopitiliza. Yani mtu anaona kabisa jambo hili sio sawa lakini atapiga makofi na kushangilia huku moyoni akijisuta mwenyewe lakini kwa sababu ya tumbo basi bora liende.
Angalau johnthebaptist kiunzi hiki kuna wakati anafanikiwa kukiruka
 
Wasio julikana Mzee. Ina maana huwajuwi... Tumechoka mbaya

Hivi unatuthibitishiaje wewe sio mmoja wao?
Tumepoteza kijana wetu humu na first suspect ulikuwa wewe kwa replies zako za humu, hivi ulishalitolea maelezo hili au ulitolea likanipita?
 
Inaonekana dhahiri sasa hata wazee wamechoshwa na Taifa la watu kuishi kwa hofu.

Msikilize Mzee Butiku hapa anavyopigilia nyundo kwa mzee Meko.

Unamfahamu Butiku Vizuri? Unafahamu nini alichokifanya akiwa kwenye nafasi zake? Tumefikia hatua ya kuunga mkono kila anayeonekana kusema chochote cha kukusaidia kupata kura moja. Jinsi hii tutajikuta tunawakariibisha watu wa jinsia moja, mashoga.
 
Huko Chadema asilimia 100 wamejaa woga juu ya mwenyekiti wao hakuna anayethubutu kugombea uwenyekiti,

Mwenyekiti ni mmoja tu. Na katiba haina kipengele cha ukomo wa mihula kwa nafasi ya uwenyekiti na wote wameufyata.
 
Fundisho kwa mjinga ni taabu,taabu ikiwa kubwa akili itawakaa,nashauri jiwe akirudi ikulu,aendelee kufanya maisha kuwa magumu na magumu ili wananchi wapate shida kubwa kubwa ili wapate fundisho.
mkiona taabu na kila kona ya nchi watu wanalalamika mjue kumekucha hapo ndo utakuwa mwisho wa ccm
 
Huko Chadema asilimia 100 wamejaa woga juu ya mwenyekiti wao hakuna anayethubutu kugombea uwenyekiti,

Mwenyekiti ni mmoja tu. Na katiba haina kipengele cha ukomo wa mihula kwa nafasi ya uwenyekiti na wote wameufyata.
Mwenyekiti wa kwanza wa Chadema ni Edwin Mtei, wa pili Bob Makani, wa tatu Mbowe.

Mpaka sasa Chadema imeongozwa na wenyeviti watatu, lakini ccm yenye miaka mingi mpaka sasa imeongozwa na wenyeviti watano tu, kama kichwani kwako kuna angalau ubongo uliobakia hebu fikiria hapo.
 
Fundisho kwa mjinga ni taabu,taabu ikiwa kubwa akili itawakaa,nashauri jiwe akirudi ikulu,aendelee kufanya maisha kuwa magumu na magumu ili wananchi wapate shida kubwa kubwa ili wapate fundisho.
mkiona taabu na kila kona ya nchi watu wanalalamika mjue kumekucha hapo ndo utakuwa mwisho wa ccm
Aisee . . . for sure we need to learn the hard way
 
Back
Top Bottom