Uchaguzi 2020 Kuelekea siku ya kupiga kura, Mzee Butiku apindua meza kibabe

Uchaguzi 2020 Kuelekea siku ya kupiga kura, Mzee Butiku apindua meza kibabe

Ndugu yake Nyerere ndie chanzo cha uoga,kwa kuwanyima watz exposure ya kuwazuia kutoka nje na alifanikiwa Sana kwenye mind control sababu hakukuwepo kwa mitandao.
Baba yake, sahihi zaidi ukisema ni baba yake ' kama hukuwahi kufahamu huyu Butiku ni mtoto wa kwanza wa mwalimu
 
Tatizo kubwa linalotuathiri watanzania tukiacha uoga ni UNAFIKI. Mtanzania kaumbwa na unafiki wa kusifia jambo hata kama linamkera. Endapo kungetokea watu toka siku ya kwanza ya Dkt. Magufuli kuingia madarakani na kufanya mambo ya kinyume na katiba ilipaswa walio karibu yake wazungumze.

Lakini walimpigia makofu huku wakisonya pembeni. Hii ilipelekea kuamini kuwa anachofanya ni sahihi na kuwa hakuna anaeweza kumhoji. Unafiki wetu watanzania ulihalalisha kukandamizwa kwetu kupelekea kufika tulipofika leo.

Bw. Magufuli ni muendelezo wa mfumo ambao ulishawekwa na waasisi wake, mfumo uliojengwa kwa unafiki na nidhamu ya uoga.
Hata hao kinana waliishia kwenda kusuka mipango yao huko nje na kina rostam kisha kurejea mikono nyuma kana kwamba wamemwagiwa maji
 
Ukiona hivyo ujuwe Magu kamkatia Umeme,maana hao Wazee wengi ndiyo wamejimilikisha Mali zetu! Magu kaza ili wote watoke mafichoni!!
Hukuwahi kumjuwa Butiku na hutokaa umjuwe labda usubiri akitangulia mbele ya haki kabla yako ndio Tbc watakushushia wasifu wake.

Huyu ni PS wa Nyerere, pata picha kwanza.
 
Alichokisema Mzee Butuku nilisema kitambi tu.

Watanzania tuna "self censorship". The worst kind of censorship.

Naona hata mitandaoni, hususqn migandqo inayotumia majina halisi kama Whatsapp, watu wanakaa kimya si kwa sababu wanapenda yanayoendelea au hawaoni.

Watu wengi wanakaa kimya kwa sababu wanaogopa.

Mzee Butiku kasema kweli.

Na woga huu ni alama kwamba watu hawana imani nanserikali yao. Wangekuwa na imani wasingekuwa na woga.
 
Mzee anaulizwa swali juu ya chanzo cha uwoga, anatoa sababu nyepesi kweli bila kuangalia kwa kina mila, desturi, na government systems.
Kama ni ujinga mbona mpaka ma-profesa wameshikwa na woga? Au alikuwa anamaanisha 'upumbafu'?
Hakuna jibu sahihi zaidi ya alilolitia Mzee Butiku.

Sababu ya msingi ya woga ni ujinga.

Huko kwenye mila, desturi, government systems, ma profesa kote woga unasababishwa na ujinga.

Mtu kuwa orofesa hakunq maqna hawezi kuwa mjinga.

Magufuli ana Ph.D lakini mpaka leo anaongea maneno ya kijinga
 
Mzee anaulizwa swali juu ya chanzo cha uwoga, anatoa sababu nyepesi kweli bila kuangalia kwa kina mila, desturi, na government systems.
Kama ni ujinga mbona mpaka ma-profesa wameshikwa na woga? Au alikuwa anamaanisha 'upumbafu'?
Unaweza ukawa professor ukawa hujaelimika!.
 
Mwenge ndio ulikuwa unawafanya watz kuwa wajinga na waoga, this time sababu haupo we uoni akili za watz zilivofunguka.
Siyo mwenge ni kuminywa kwa upatikanaji habari na kushughulikiwa walikoshuhudia tangu nchi ingali changa
 
Mzee anatulaumu wa Tz kwa kuwa waoga. Ameshindwa kukubali kuwa jasiri na wasema kweli siku hizi wanaishia kupotezwa, kufunguliwa kesi za ovyo, kupigwa risasi, n.k. Awe wazi.

Asipidishe maneno. Amtizame shetani machoni na amwambie: Wewe ni Shetani. Hapo ndipo tutaamini kuwa yeye ni jasiri kama alivyo TAL.
We hukumbuki Kaka yake alipigwa vibao na bwana yuleee! bashite!!
 
Back
Top Bottom