Wenzangu wengi wameshachangia kuhusu kilichotokea jana cha mwanajeshi anayetwa Shimbo kuwatisha wananchi. Nimejaribu kufikiri kwa undani kwa nini iwe sasa? Ninavyojua mimi jeshi la wananchi linatakiwa liingilie mambo ya ndani pale ambapo situation itakuwa desperate kwamba hata polisi wameshindwa kufanya kazi. Hali kama hii hatujaifikia, kwa maana ya kwanza wamedharilisha jeshi la polisi kwamba limeshindwa kazi. Pili wamekiuka maadili ya kazi yao ambao kubwa ni kulinda mipaka ya nchi. Kikubwa zaidi nilichogundua ni kwamba kuna mpango ambao ni coordinated na baadhi ya vyombovya habari. Kwa mfano wakati ITV inatangaza habari hiyo liweka picha za wanajeshi wakiwakamata raia wakiwa wameinua miono juu!. Kwa hiyo huu ni mpango zaidi ya wanajeshi.Cha msingi hawa wanajeshi watambue kwamba raia w sasa hivi hawatishwi hovyo tunataka haki mambo ya kuleta amani kwa mtutu hatutaki na kwa hiyo tamko lao halikuwa na ulazima zadi ya wao kutumika kama papet wa CCM jambo linaloshusha heshima ya jeshi.Navishauri vyama vya ushindani kuufahamisha umoja wa Africa (AU), Umoja wa mataifa (UN) NA nchi wafadhili wafahamu mambo yanayoendelea behind the scene as a preemptive move.Namalizi kusema kwamba wanajeshi wamerukia yasiyoahusu kwa sasa.