Elections 2010 Kuelekea uchaguzi: Jeshi lawatisha wananchi

Elections 2010 Kuelekea uchaguzi: Jeshi lawatisha wananchi

shimbo asileta mambo yake ya ushoga hapa pumbavu zake..ujinga wake huko huko na bosi wake mwamunyange mrembua macho...Rais wanayemtaka hapiti na ni mgonjwa wasitulazimishe kuchagua maiti iliyo hai...Dr.Slaaa goo gooo goo!!!

Hakuna sababu ya kumtukana Shimbo. Amekosea kusema maneno hayo lakini tusifikie hatua ya kumtukana hadi mwili wake. Wala hakuna sababu ya kumtukana Gen. Mwamunyange juu ya alivyoumbwa. Hawa ni binadamu tu. Kumbuka ni dhambi kusema, "Shetani ni mseng*" Akina Mwamunyange waelewe hatukubali msimamo wao kwa hoja tutakazotoa.
 
Naiona habari ya Slaa ITV, acha tu!!!!!!!!!!
 
Hakuna sababu ya kumtukana Shimbo. Amekosea kusema maneno hayo lakini tusifikie hatua ya kumtukana hadi mwili wake. Wala hakuna sababu ya kumtukana Gen. Mwamunyange juu ya alivyoumbwa. Hawa ni binadamu tu. Kumbuka ni dhambi kusema, "Shetani ni mseng*" Akina Mwamunyange waelewe hatukubali msimamo wao kwa hoja tutakazotoa.
Sikio la kufa halisikii Dawa,. Hoja pekee Haziwatoshi Wahafidhina wakubwa hao
 
Watu wote Tunajua Kikwete, Lowassa, Rostam na Chenge ndiyo wanaoongoza nchi hii, watahakikisha CCM inarudi madarakani kwa gharama zozote.

Hawa wote wanaoandika andika hoja za kutetea utendaji kazi wa JK ni njaa zinawasumbua, mtu yupo radhi kumsaliti mtanzania mwenzake kwa kupokea vipande vitatu vya sarafu. kwa syle hii hatufiki popote as na nation.
 
Only in Tanzania mtu anaingilia kazi za watu na wala hawajibishwi au komba radhi.
 
Only in Tanzania mtu anaingilia kazi za watu na wala hawajibishwi au komba radhi.
Siyo "Kuingilia kazi" rather ni kulinda maslahi yao kifisadi...Wao kwa wao....Sasa vipi kuhusu Amiri jeshi mkuu anapoingilia mhimili wa mahakama na kusema watuhumiwa wa ufisadi wanasingiziwa?Mnadhimu mkuu na amiri jeshi mkuu wote lao moja.
 
headline_bullet.jpg
Wasema wamejiandaa kukabili vurugu
headline_bullet.jpg
Waonya vyama vya siasa, taasisi binafsi

onyo%281%29.jpg

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, akitoa tamko la ulinzi na usalama mbele ya waandishi wa habari Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Naibu Kamishna wa Polisi, Peter Kivuyo, na kulia ni Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna, Venance Tossi.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likishirikiana na Jeshi la Polisi nchini wamevitaka vyama vya siasa kukubali matokeo baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba na kuonya kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kikamilifu kupambana na yeyote atakayejaribu kuyakataa matokeo.

Tamko la vyombo hivyo vya usalama lilisomwa mbele ya waandishi wa habari jana na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, Makao Makuu ya JWTZ, Upanga, jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo, Luteni Jenerali Shimbo aliambatana na maofisa kadhaa wa JWTZ, Kamanda wa Kikosi cha Operesheni Maalumu cha Jeshi la Polisi nchini, Venance Tossi, na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa

Makosa ya jinai, Peter Kivuyo.
Alisema wamelazimika kuweka msimamo huo bayana baada ya kuona dalili za baadhi ya taasisi na vyama vya siasa kutaka kuvunja sheria wakati huu wa kampeni.

"Vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kikamilifu kupambana na mtu, watu, kikundi, chama au taasisi yoyote itakayokwenda kinyume na (cha) sheria, kuchochea au kufanya fujo, kuvunja amani kwa mujibu wa sheria. Aidha, kuchochea kuyakataa matokeo," alisema Luteni Jenerali Shimbo.

Aliongeza kuwa: "Vyama vya siasa vifanye kampeni kwa ustaarabu na kufuata sheria na kanuni za uchaguzi, visitukane vyombo vya dola wala kuvichokoza kwa vile havihusiki na siasa zaidi ya kulinda amani na utulivu."
Alisema vyombo vya ulinzi vimejipanga kuhakikisha kwamba damu haimwagiki wakati wa kampeni na baada ya uchaguzi na kuwaomba wananchi kushirikiana navyo katika kutunza amani na usalama wa nchi.

"Dalili zimeanza kuonekana za kutaka kuvunja sheria katika kampeni, kuchochea fujo na uvunjifu wa amani ... dalili hizi sio nzuri na zinaweza kuharibu utulivu na amani iliyopo kwa miaka mingi. Aidha, baadhi ya mashirika yameanza kutoa matamko yanayolenga kushabikia vyama vya siasa na wagombea," alisema.
Luteni Jenerali Shimbo alisema vyombo vya ulinzi na usalama vimebaini pia kwamba baadhi ya taarifa

zinazotolewa kwenye vyombo vya habari hazichujwi ipasavyo.
Aliwataka waandishi wa habari kuchuja taarifa zao. "Ninyi pia mnayo dhamana kubwa ya kulinda amani na utulivu, wananchi wanafuatilia sana vyombo vya habari mkiruhusu haya mtatupa kazi kubwa sana, hamtakuwa mmelitendea haki taifa hili," alisema Shimbo.
Bila kutaja chama chochote, alisema baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikivihusisha vyombo vya ulinzi

kwa kuvihusisha na vyama vingine vya siasa.
Alisisitiza kuwa maofisa wa vyombo hivyo hawafungamani na chama chochote na kwamba hawaruhusiwi kushabikia upande wowote zaidi ya kuhakikisha taifa lipo salama.

"Vyombo vya ulinzi na usalama vinapenda kueleza kuwa wajibu wake ni kuhakikisha amani, usalama na utulivu wa nchi yetu wakati wowote usiku na mchana, havifungamani na chama chochote cha siasa bali vinatii viongozi na serikali iliyoko madarakani," alisema.
Alisema vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kulinda amani wakati huu wa kampeni, siku ya kupiga kura na wakati wa kuapishwa.
Tamko hili la vyombo vya ulinzi na usalama limekuja zikiwa zimesalia siku 29 tu kabla ya siku ya kupiga kura, Oktoba 31, mwaka huu.

Mnyika: Uchaguzi ni kazi ya Polisi
Akizungumzia tamko hilo, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, alisema chama hicho kinaamini kwamba JWTZ ni jeshi la wananchi ambalo lina jukumu kubwa la kulinda mipaka ya nchi ili kuhakikisha ni salama wakati wote.

Alisema jukumu la uchaguzi linalihusu Jeshi la Polisi ambalo linasimamia amani kwenye vituo vya kupigia kura pamoja na NEC ambacho ni chombo cha serikali kinachohusika na uchaguzi.
"Tunajua JWTZ halina chama, lakini maofisa wake wanaweza kushiriki kwenye zoezi la upigaji kura kwa kiongozi wanayemtaka sio vizuri kwa jeshi letu kujiingiza kwenye siasa hasa kipindi hiki, tunadhani JWTZ lingeliachia jeshi la polisi jukumu la kulinda amani wakati wa uchaguzi," alisema.

Mnyika alifafanua kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kukishauri chama tawala kikubali matokeo kwa kuwa mara nyingi vyama tawala vimekuwa na kasumba ya kutokubali kushindwa.
Alisema amani na utulivu wakati wa uchaguzi unategemea usimamizi mzuri wa NEC kwa kuweka uwanja sawa wa kampeni na upigaji kura.

Makamba: Sijui yanayoendelea Dar

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hakuwa amepata taarifa kwa kina.
"Mimi nipo Tunduru sijui mambo yanayoendelea huko...niulize ya Tunduru siwezi kuzungumzia kitu ambacho sijakisikia," alisema.

Kinana: Tutafuata sheria

Meneja Kampeni wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipotakiwa kutoa maoni naye alisema CCM itazingatia sheria, kanuni na taratibu zote zinazotawala uchaguzi na kwamba chama hicho kitaheshimu matokeo ya uchaguzi yatakayotangazwa na NEC.
"Lakini kama kutakuwa na malalamiko yoyote tutafuata taratibu zilizowekwa kuyawasilisha kwa vyombo husika," alisema.
Alisema chama hicho kinategemea pia kwamba vyama vingine vya siasa vitazingatia sheria na kanuni ili kudumisha amani wakati huu wa kampeni na baada ya uchaguzi mkuu.

CHANZO: NIPASHE
 
magazeti ya rostam na ushabiki wa kidini kimya, na yale mengine kimya, na kupitiliza saa za kampeni kimya, na kagoda kimya, na meremeta licha jina la jueshi kutumika kimya, haya generali simbo, mamlaka na uwezo ni wako.
 
Siyo "Kuingilia kazi" rather ni kulinda maslahi yao kifisadi...Wao kwa wao....Sasa vipi kuhusu Amiri jeshi mkuu anapoingilia mhimili wa mahakama na kusema watuhumiwa wa ufisadi wanasingiziwa?Mnadhimu mkuu na amiri jeshi mkuu wote lao moja.

Hili tamko limeniacha hoi jeshi kutangaza hivi linamaanisha polisi kazi hawawezi au? Serikali ya Tanzania kila kitu kiko shaghalabaghala tu kila mwenye cheo akijisikia anaropoka analotaka rais ndio hivyo anawakampenia watuhumiwa wa ufisadi. Ila hili tamko la Shimbo alitakiwa alitoe mkuu wa polisi sio mnadhimu wa jeshi.
 
Shimbo aende tuu kulinda mipaka ya nchi yetu kama inavyobid na si vinginevyo
 
Source: Tanzania Daima

amka2.gif
JESHI la Wananchi (JWTZ) limetoa onyo kali kwa watu na taasisi ambazo zimeanza kutoa kauli zenye mwelekeo wa kuchochea vurugu na kuvunja amani wakati huu taifa linapojiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu. JWTZ lilitangaza onyo hilo la kwanza la aina yake mbele ya waandishi wa habari kupitia tamko lililotolewa na Mnadimu Mkuu wa jeshi hilo, Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo.
Akizungumza kwa kujiamini na pasipo kutoa mfano wowote wa kuwapo kwa hali inayotishia amani, Jenerali Shimbo alisema vikosi vya ulinzi na usalama vimejipanga kukabiliana na mtu, taasisi, shirika ama kikundi chochote kitakachoashiria uvunjifu wa amani wakati huu wa kampeni, uchaguzi na kabla na baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
Jenerali Shimbo, aliyekuwa akizungumza yalipo makao makuu ya JWTZ (Ngome) jijini Dar es Salaam alisema tayari kumeanza kuwapo kwa dalili zinazotoa ishara mbaya kuhusu tishio la amani nchini.
Mnadhimu huyo aliwaomba wananchi na wanasiasa, kuendeleza amani iliyopo hasa kipindi cha uchaguzi licha ya ukweli kwamba majeshi yake yamejiandaa kikamilifu kukabiliana na uovu wowote hasa wakati wa kutangazwa kwa matokeo.
"Dalili zimeanza kuonekana za kutaka kuvunja sheria katika kampeni, kuchochea fujo na uvunjifu wa amani… dalili hizo sio nzuri. Pia kuna baadhi ya taasisi na mashirika yameanza kujiingiza kwenye kampeni kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuhusu upigaji kura au kutoa matamko yanayolenga kushabikia vyama vya siasa na wagombea.
"Tuko tayari kupambana na yeyote yule atakayetaka kuvuruga amani, nawahakikishia wananchi wote, hakuna damu itakayomwagika. Tumejipanga kulikabili hilo. Tutashirikiana na Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa ratiba, kanuni, sheria na taratibu zao kuilinda amani yetu.
"Napenda kulisisitiza hili, vyombo vya ulinzi na usalama havifungamani na upande wowote katika siasa. Kuvihusisha huko ni kutuchokoza, msituchochee wala kutuchokoza tuko kwa ajili ya kuwalinda," alisema.
Mnadhimu Shimbo alivionya pia vyombo vya habari nchini kuchuja habari ili kuepuka uchochezi wa vurugu na kuviagiza kuwa wadau wakubwa wa amani kutokana na imani ya wananchi kwa vyombo vya habari.
Katika hilo, Luteni Jenerali huyo alisema zipo nchi zilizoingizwa kwenye machafuko kutokana na waandishi wa habari hususan wakati wa chaguzi kama ilivyo sasa hapa nchini.
"Waandishi msikubali kuwa wachochezi wa vurugu, tunawaomba mzichuje habari zenu kabla ya kuzitoa maana zitaweza kuhatarisha amani, jambo ambalo sisi hatuko tayari kuona likitokea… tunajua kwamba wananchi wanawaamini sana, hivyo tushirikiane kuilinda na kuitunza amani; kuutunza utulivu na usalama uliopo," alisisitiza.
Tamko la vyombo vya ulinzi na usalama, limekuja siku 30 kabla ya kupiga kura huku kukiwa na taarifa za vurugu na fujo za hapa na pale kwenye mikutambo ya wagombea mbalimbali hasa wa vyama vya CCM, CUF na CHADEMA.
Aidha, tamko hilo pia linazihusu taasisi mbalimbali za dini, asasi za kiraia zinazotoa elimu kwa wapiga kura kuzitaka kuimarisha hali ya utulivu na amani ya taifa iliyodumu kwa miaka 48 sasa.
Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba alilaani taarifa iliyotolewa na Luteni Jenerali Shimbo kuwa ni kitendo cha kutaka vyama vya siasa kukubaliana na matokeo ya uchaguzi.
Alisema hatua iliyochukuliwa na Mnadhimu wa JWTZ, Luteni Jenerali Shimbo, ni kulidhalilisha jeshi na kumtaka kuomba radhi kwa wananchi kwa kulidhalilisha jeshi hilo.
"Hatua waliyofikia jeshi la Wananachi ni kutaka kuibeba CCM waziwazi na yaelekea hawajui mamlaka yao ya kulinda mipaka ya nchi. Kauli hii ilitakiwa kutolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi na si JWTZ," alisema Lipumba.
Alisema, umefika wakati kwa kamati ya dini ya kitaifa kukemea hatua hiyo kwani inaweza kusababisha machafuko nchini kwa vyama vya siasa kupikiwa matokeo ya lazima na vyombo vya ulinzi na usalama.

My Take:
Guys lets us discuss this matter in detail,huo usalama unaotishiwa mimi sion hayo matishio kabisa,viongozi wa dini kutoa elimu ya uraia kuwaasa Wananchi juu ya kumchagua Kiongozi safi,kunahusiana nini na uvunjaji wa aman,hiv anaposema kuna hatari ya umwagaji damu ana maana gan?
Kauli yake inashabihiana na kauli ya Rais Kikwete reffer pale alipokuwa anamnadi Rostam,allmost alichokuwa anakisema ndo hicho amabacho Shimbo amekizungumza.reffer gazeti la mwananchi la leo..
""Wenye vyama hivi hawana sera, wao ni wadandiaji sera na wanung'unikaji tu, hawana kipya wakati mwingine wanahubiri kumwaga damu. Sasa hakuna damu itakayomwagika kwa mtu wa kawaida na hata hao wanaohubiri," alisema.
.
Fikiria,chukua hatua
 
Ukiona Jeshi linawageukia raia wake ambao wanaliwezesha kuwepo kwake, basi lazima ufahamu kwamba jeshi hilo liko mikononi mwa Mafisadi. Limevunjikavunjika kama kipande cha kioo.

Tumeyaona na kudhuhudia yaliyotokea Zimbabwe waliwapiga wananchi bila huruma na mwisho wakakubali yaishe ili waendelee kula japo kidogo. Lakini kwa Tanzania kuwa na jeshi ambalo linawekwa mfukoni na Mafisadi, hili haliwezi kuwa JWTZ pengine itabidi jeshi hili kuundwa upya kwa mantiki ya 21st century maana mabadiliko yale ya 1964 inavyoonekana yamepitwa na wakati kwa sababu yule failure ambaye alipita kule na hivi sasa ameshika mpini anafikiri anaweza kuwatisha watanzania.

Hivi wanafahamu kwamba wengi wetu pia tumepita jeshini? Kipi hasa kitakuwa kipya? Uzoefu wa jeshini wengi tunao kwa hiyo basi hii mikwara mbuzi haiwezi kuwababaisha wapiga kura na huu mwaka ndio mwaka wa uamuzi. Tukumbuke mwalimu alisema Wakati ni huu wakati wa kisomo cha ngumbaru, usemi huo sasa unaweza kabisa kutumiwa kuwahamasisha wapiga kura, wasikubali kutetemeshwa na wale ambao wamepewa dhamana kuwalinda.
 
Hawa ccm walizoea kuwatisha wazenji kwa vifaru wakati wa uchaguzi sasa mwamko upo nji nzima sasa tuone na huku bara watatembeza vifaru mtaaaniiii??????????????wazenji wameshazoea hizi kashkash zao na vitisho vyao
 
headline_bullet.jpg
Wasema wamejiandaa kukabili vurugu
headline_bullet.jpg
Waonya vyama vya siasa, taasisi binafsi

onyo%281%29.jpg

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, akitoa tamko la ulinzi na usalama mbele ya waandishi wa habari Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Naibu Kamishna wa Polisi, Peter Kivuyo, na kulia ni Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna, Venance Tossi.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likishirikiana na Jeshi la Polisi nchini wamevitaka vyama vya siasa kukubali matokeo baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba na kuonya kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kikamilifu kupambana na yeyote atakayejaribu kuyakataa matokeo.

Tamko la vyombo hivyo vya usalama lilisomwa mbele ya waandishi wa habari jana na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, Makao Makuu ya JWTZ, Upanga, jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo, Luteni Jenerali Shimbo aliambatana na maofisa kadhaa wa JWTZ, Kamanda wa Kikosi cha Operesheni Maalumu cha Jeshi la Polisi nchini, Venance Tossi, na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa

Makosa ya jinai, Peter Kivuyo.
Alisema wamelazimika kuweka msimamo huo bayana baada ya kuona dalili za baadhi ya taasisi na vyama vya siasa kutaka kuvunja sheria wakati huu wa kampeni.

“Vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kikamilifu kupambana na mtu, watu, kikundi, chama au taasisi yoyote itakayokwenda kinyume na (cha) sheria, kuchochea au kufanya fujo, kuvunja amani kwa mujibu wa sheria. Aidha, kuchochea kuyakataa matokeo,” alisema Luteni Jenerali Shimbo.

Aliongeza kuwa: “Vyama vya siasa vifanye kampeni kwa ustaarabu na kufuata sheria na kanuni za uchaguzi, visitukane vyombo vya dola wala kuvichokoza kwa vile havihusiki na siasa zaidi ya kulinda amani na utulivu.”
Alisema vyombo vya ulinzi vimejipanga kuhakikisha kwamba damu haimwagiki wakati wa kampeni na baada ya uchaguzi na kuwaomba wananchi kushirikiana navyo katika kutunza amani na usalama wa nchi.

“Dalili zimeanza kuonekana za kutaka kuvunja sheria katika kampeni, kuchochea fujo na uvunjifu wa amani ... dalili hizi sio nzuri na zinaweza kuharibu utulivu na amani iliyopo kwa miaka mingi. Aidha, baadhi ya mashirika yameanza kutoa matamko yanayolenga kushabikia vyama vya siasa na wagombea,” alisema.
Luteni Jenerali Shimbo alisema vyombo vya ulinzi na usalama vimebaini pia kwamba baadhi ya taarifa

zinazotolewa kwenye vyombo vya habari hazichujwi ipasavyo.
Aliwataka waandishi wa habari kuchuja taarifa zao. “Ninyi pia mnayo dhamana kubwa ya kulinda amani na utulivu, wananchi wanafuatilia sana vyombo vya habari mkiruhusu haya mtatupa kazi kubwa sana, hamtakuwa mmelitendea haki taifa hili,” alisema Shimbo.
Bila kutaja chama chochote, alisema baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikivihusisha vyombo vya ulinzi

kwa kuvihusisha na vyama vingine vya siasa.
Alisisitiza kuwa maofisa wa vyombo hivyo hawafungamani na chama chochote na kwamba hawaruhusiwi kushabikia upande wowote zaidi ya kuhakikisha taifa lipo salama.

“Vyombo vya ulinzi na usalama vinapenda kueleza kuwa wajibu wake ni kuhakikisha amani, usalama na utulivu wa nchi yetu wakati wowote usiku na mchana, havifungamani na chama chochote cha siasa bali vinatii viongozi na serikali iliyoko madarakani,” alisema.
Alisema vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kulinda amani wakati huu wa kampeni, siku ya kupiga kura na wakati wa kuapishwa.
Tamko hili la vyombo vya ulinzi na usalama limekuja zikiwa zimesalia siku 29 tu kabla ya siku ya kupiga kura, Oktoba 31, mwaka huu.

Mnyika: Uchaguzi ni kazi ya Polisi
Akizungumzia tamko hilo, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, alisema chama hicho kinaamini kwamba JWTZ ni jeshi la wananchi ambalo lina jukumu kubwa la kulinda mipaka ya nchi ili kuhakikisha ni salama wakati wote.

Alisema jukumu la uchaguzi linalihusu Jeshi la Polisi ambalo linasimamia amani kwenye vituo vya kupigia kura pamoja na NEC ambacho ni chombo cha serikali kinachohusika na uchaguzi.
“Tunajua JWTZ halina chama, lakini maofisa wake wanaweza kushiriki kwenye zoezi la upigaji kura kwa kiongozi wanayemtaka sio vizuri kwa jeshi letu kujiingiza kwenye siasa hasa kipindi hiki, tunadhani JWTZ lingeliachia jeshi la polisi jukumu la kulinda amani wakati wa uchaguzi,” alisema.

Mnyika alifafanua kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kukishauri chama tawala kikubali matokeo kwa kuwa mara nyingi vyama tawala vimekuwa na kasumba ya kutokubali kushindwa.
Alisema amani na utulivu wakati wa uchaguzi unategemea usimamizi mzuri wa NEC kwa kuweka uwanja sawa wa kampeni na upigaji kura.

Makamba: Sijui yanayoendelea Dar
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hakuwa amepata taarifa kwa kina.
“Mimi nipo Tunduru sijui mambo yanayoendelea huko...niulize ya Tunduru siwezi kuzungumzia kitu ambacho sijakisikia,” alisema.

Kinana: Tutafuata sheria
Meneja Kampeni wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipotakiwa kutoa maoni naye alisema CCM itazingatia sheria, kanuni na taratibu zote zinazotawala uchaguzi na kwamba chama hicho kitaheshimu matokeo ya uchaguzi yatakayotangazwa na NEC.
“Lakini kama kutakuwa na malalamiko yoyote tutafuata taratibu zilizowekwa kuyawasilisha kwa vyombo husika,” alisema.
Alisema chama hicho kinategemea pia kwamba vyama vingine vya siasa vitazingatia sheria na kanuni ili kudumisha amani wakati huu wa kampeni na baada ya uchaguzi mkuu.

CHANZO: NIPASHE

Hizi ni dalili za Serikali ya Mseto ya kulazimisha kama ilivyotokea Kenya.
 
Kauli ya Mnadhimu wa JWTZ inamuondolea sifa ya kuendelea kuwa Mnadhimu wa Jeshi hilo.Rais wa Jamhuri ya Muungano ilipaswa amstaafishe Luteni Jenerali Abdulrahmani Shimbo kwa kauli yake ya Uchochezi,na kutokujua mipaka yake ya kazi.Si kazi ya Jeshi la Ulinzi na Usalama kusimamia Uchaguzi,Masuala yote ya amani ya ndani ya Nchi ni suala la Jeshi la Polisi.Inaweza kuwa ni kwa makusudi au Luteni Jenerali Shimbo hafahamu mipaka yake ya kazi.Kwa kosa hilo ilibidi awajibike!
 
JWTZ Lilianzishwa tarehe 01 Septemba, 1964 likiwa na lengo la kulinda uhuru, na mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. JWTZ lina majukumu yafuatayo:
  1. Ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya adui.
  2. Kutoa mafunzo ya kivita kwa maafisa na askari ili kumshinda adui.
  3. Kutoa msaada unaohitajika kwa mamlaka za Serikali katika hali ya hatari na maafa yatokanayo na nguvu za asili.
  4. Kusaidia uwezo wa mamlaka ya Serikali katika kudhibiti ghasia au vurugu ndani ya nchi.
  5. Kuendesha na kusimamia mafunzo ya mgambo.
  6. Kushiriki katika shughuli za kulinda amani duniani.
 
[*]Kusaidia uwezo wa mamlaka ya Serikali katika kudhibiti ghasia au vurugu ndani ya nchi.

Nadhani hii yenye red ni baada ya Polisi kushindwa si eti? Isijekuwa pale kirumba mashabiki wa Simba na Toto wanatwangana hafu JWTZ wanaingilia, au Mgambo wa jiji wanakimbizana na Machinga, JWTZ wanaingilia!
 
Unaweza kuta hayo majukumu yalitungwa toka 1964 bse item 4 inagongana na polisi
 
Back
Top Bottom