Bora mara kumi elfu zitto kuliko Mbowe
Na bora Mbowe kuliko Mwakalinga au sio?!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bora mara kumi elfu zitto kuliko Mbowe
Hawa ndio wameshakigawa chama. Upande mmoja kuna kundi linalomuunga mkono Zitto likiongozwa na Msafiri Mtemelwa lenye makada kama Kafulila, Danda na wenyeviti wa zamani wa mikoa. Upande mwingine kuna wanaompinga asiwe mwenyekiti, kundi hili yuko Dr Slaa, Profesa Baregu, Mnyika, Tundu Lissu, Benson Kigaila na viongozi wa wilaya
Serayamajimbo
hapo kuna kazi kubwa. hawa wasiomtaka wanamtaka nani? Mbowe?😕
no we need a new chairman.
Mbowe akiondoka mie nitachukua kadi ya chadema
Slaa angefaa sana kuwa canditate wa CHADEMA ktk Uraisi wa nchi!
Slaa akiwa raisi wa nchi hii..Tanzania ingebadilika kuwa nchi nzuri zaidi kwa haraka!!
Vipi Mbowe hapendi tena uenyekiti??
Wakiwa makini huu utakuwa msingi mzuri wa Demokrasia, lakini wakichemsha yatakuwa yale yale ya NCCR_mageuzi ya Kina, Mrema, Marando, Maguto etc.
Hawa hawana itifaki na inaonyesha wanamatatizo makubwa sana ,yaani kuwepo kote kwa muda mrefu wakiwa viongozi wakuu ,wanaonyesha dalili za kuwa na matatizo ya ndani kabisa ,ninavyoamini ikiwa nyote ni wananchama wa chama kimoja na mmetoka mbali katika kukiendeleza chama chenu basi lazima mtakuwa na mashirikiano (strategy) za karibu kabisa na kuweza kumpanga Mwenyekiti ,ikiwa tu aliekuwepo atakumbwa na mauti au atasema basi, kupeleka watu wazito wawili katika kugombea nafasi ya juu ya Chama ni kuonyesha kuwa au ni kukigawa chama ,inaonyesha waChadema hawana maelewano ,nilivyotaraji labda angetokea mtu mwengine kabisa zaidi ya wale heads kutaka kugombea nafasi hiyo na sio vinara walio juu ,huko ni kukosa muelekeo na hapa Chadema watakuwa wamechemsha au labda iwe ni mbinu ya kutaka kuwadanganya waTz kuwa ndani ya Chama chao kuna demo na sio demokrasi.
Ilikuwa ni lazima awepo kiongozi katika top 10 wa Chadema ambae angeweza kuchukua nafasi ya kugombea pindipo Mwenyekiti aliekuwepo ameamua kubwaga manyanga ,na itakuwa wenyewe wawe wanalijua hilo na wawe wanamjua kwani ni jambo la kuridhiana kabisa katika harakati za kuendesha Chama kikuu na sio mnatokea kama mnaonekana mnanyang'anyia ,ni kukigawa Chama ,na hapo ikitokea kufikia kupigiwa kura na kuibuka mmoja kumshinda mwenziwe kwa kura kidogo basi mambo hayatakuwa mazuri & they will never be the same again ,ingawa watataka ionekane machoni mwa WaTz kuwa mambo ni kawaida na ndio demokrasia ilivyo ,ni sawa lakini not in that way at all and spesho in Tz.
Mungu wangu ibakishe salama walau Chadema, najuwa CCM wamekaa mkao wakula kuotea "machafuko" ndani ya Chadema. Tuwaombeeni Chadema wafanye mkutano wa kupanga safu zao kwa amani na utulivu na kukiimarisha chama chao. Kama habari hizo ni za kweli nawatakia chadema uchaguzi mwema na wapite salama katika jaribio hili la kimageuzi.