omarilyas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2007
- 2,130
- 150
Hili ndio tatizo la CHADEMA , nafikiri tayali Sultani CCM ameshapandikiza watu wake na sasa wapo katika kuhitimisha kukisambaratisha Chama hiki, afu CCM kwa vyama kama hivi vidogo vidogo inakuwa haina haraka wala hawafanyizii kama kule kwenye chama cha wababe CUF ambako CCM imegonga mwamba na sasa inaendeshwa puta.
Kitu kimoja napenda mkielewe kuwa katika Chadema kuna mambo ambayo wakuu wake wanashirikiana na wafuasi wa baadhi ya wakuu wa Sultani CCM ,katika maslahi ya kibiashara hapo ndio ukaona hiki chama huwa kinalega lega na kufikia hata wakati wanaungana na wateja wenzao wa CCM katika kufuatilia baadhi ya mambo ambayo yanawagusa kimaslahi.
Mkiambiwa Chadema sio Chama kinachoweza kumkomboa Mtanzania mnapanda peresha ,na kama mnataka ushahidi mnauona hapa JF ,siku hizi makada wa Chadema wamekuwa kama kuku waliotiwa kwenye gunia lililoloweshwa maji ,wamekaa kimya na kuduwaa wakingojea hatima ya uchaguzi wa chama chao uliojaa mizengwe na migawanyiko ,tatizo ninaloliona ni kuwa ndani ya CHADEMA hakuna security inayoweza kuwang'amua mamluki ambao wamejikita ndani ya chama kwa muda mrefu unaweza kuwafanisha na wale askari maalum wa kutunga na kuwaua watu maalum ndani ya vita au kwa jina la kijeshi wanaitwa snippers ,hawa snippers wa CCM wamejikita ndani ya vyama vya siasa vya upinzani na wametulia kikweli inataka mbinu za hali ya juu katika kuona mienendo yao. Tumeona kwenye uchaguzi wa CUF ni jinsi gani snippers wa CCM waliondolewa kwa kupigwa na chini wakiachwa wakipiga makelele,hawa snippers wa CCM wanaweza ukawaona ni viongozi imara kabisa ndani ya chama chako ambao wapo mstari wa mbele kila siku ,lakini shabaha yao ni kukivuruga chama na wakati muafaka wauonao ni mzuri ni huu wa uchagusi ndani ya Chama ,hapa ndipo wanapojaribu kucheza.
Nawatakia uchaguzi wenye utulivu ambao utajenga maelelwano ya kweli na vyama vingine vya upinzani kuliko huu umoja unaowaonyesha CHADEMA kama ndumila kuwili.
Huyu naye......na dua la kuku kamwe haliwapati mwewe, wataendelea kukudonowa hadi ubaki mifupa...
omarilyas