Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Katika uchaguzi huo, Basil Lema, alichaguliwa kuwa Katibu wa chama hicho huku Deogratius Munishi, akichaguliwa kuongoza Baraza la Vijana wa chama hicho na Seranus Mushi alichaguliwa kuongoza Baraza la Wazee wa chama hicho.

Ndesamburo kachaguliwa kiti gani na mtoto kachaguliwa kiti gani?
 
hapa nilisema kuwa hawa ni mamluki tu copy & paste ya ccm ,ila kitu kimoja ambacho niliwashauri ,hawa akina zitto wasiwe na papara ya kutaka uenyekiti waridhike na nafasi waliyokuwepo mpaka pale mwenyekiti mwenyewe atakapoamua kuachia ngazi au kujiuzulu,na iwe mnapishana kiaina ,yaani katika safu kuu asitokeze mtu pua kutaka nafasi ya juu na hata akitokeza asiwemo katika ile safu kuu ya uongozi.

Maana chama lazima kiwe na msimamo na viongozi wake walio katika nafasi kuu za juu kabisa ili kusitokee migongano kama tunavyoona ,kwa mfano mwenyekiti agombee palepale makamu halikadhalika na katibu nae awanie nafasi yake ileile ,kama ni kupangwa au kupanguliwa, kilichojitokeza kwa chadema nasema sio jambo zuri kabisa kwa zitto kutaka kugombea nafasi hiyo ,kwani umri wake unamuwezesha kusubiri pale wakuu wenzake watakapofika wakati wa kuachia ngazi na kumkabidhi chama.

Hizo ni hisia nzuri kabisa kwa chama chenye viongozi wanaothaminiana na walio amua kukijenga chama chao , demokrasia itumike kwa walio nje ya uongozi na sio waliomo ndani ya uongozi wa ndani tena wa juu,hawa inawabidi watulize akili zao vilivyo kama tuonavyo katika uongozi wa cuf, nafasi za juu zinakuwa protected kwa wale waliomo ndani na zinakuwa open kwa walioko nje, natumai nimeeleweka.

sijakuelewa kwa hiyo professor safari mmemzuia kwa kanuni hii?
Hujui mchango wa professor safari kwa cuf? Unajua kuwa alifukuzwa kazi na kupoteza zaidi ya milion mia moja kwa sababu ya cuf?

Zitto kabwe kama ni kijana hana uwezo kwanini mlimtuma busanda akawafanyia kazi kubwa. Kuomba uenyekiti mnasema umri haukutosha.kweli hii ni miujiza.
 
matatizo ya chadema yapo kwenye vyanzo vya fedha. Hapo ndipo tatizo lilipo. Nani atachaguliwa kuwa mwenyekiti kwenye uchaguzi huu, ndiye atakaye peleka chama kwenye uchaguzi 2010.

chadema inategemea kushinda majimbo zaidi ya haya ya sasa, hivyo mapato yao yataongezeka maradufu…usimamizi wa mapato hayo ndio chanzo cha haya yote.

natumaini watamaliza hizi tofauti zao kwenye uchaguzi huu. Taifa linawahitaji watu kama dr slaa wame behind strong institutions.

come on chadema….

wewe mzima kweli? Aliyechangia pesa nyingi uchaguzi uliopita ni ndesamburo na mengi jee hawa walikuwa na wadhifa wa uenyekiti taifa?
Kwanini wazee hawa wasimpe mbowe umakamu mwenyekiti? Kwani mtu anachagia chama hadi awe mwenyekiti?

Cuf wanaochangia sana na kutafuta funds sio lipumba,mtafute mchukia ufisadi ambaye kwa bahati ni member hapa atakwambia nani anatafuta michango ya cuf.
 
kipofu haambiwi tazama,haihitaji uwe umekwenda univesiti kugundua kuwa chadema ni sacos ya baadhi ya wachaga

waliochaguliwa kuongoza chadema kilimanjaro ni wachagga watupu.wakiongozwa na ndesamburo na mtoto wake lucy ambao wamepita bila kupibngwa.
 
Naomba tuwe waangalifu tusitumiwe na yule mwovu (CCM). Habari hii ililetwa vibaya. Lengo lilikuwa lipi?

Hapo ndipo ambapo nyie wakereketwa wa CHADEMA-Family-Operation (au Origino) mnatukatishaga tamaa sisi wa CHADEMA-National-Party(ambayo tungependa iongozwe na Dr Slaa). Hebu tueleze, CCM inahusika vipi na mapambano kati ya Zitto na Mbowe mpaka kuwatupia lawama? Yaani Zitto hawezi kutaka kugombeya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA akijiona ana uwezo mpaka apate msukumo na CCM? Acheni hayo...

Ndio maana wasomaji waliotanguria walisemaga CHADEMA imekuwa kama CCM. Sasa namimi nakubalina nawo. Mkifurunda kwenye kambi yenu mnakimbilia kuwalaumu CCM. Mnakuwa kama CCM wanavyofanya kulaumu upinzani! Tena afadhali CCM walisuhusu demokrasia kwa kuwaruhusu Kikwete, Mondosha, Salim, Kigoda, na Sumaye kugombea na kuwapigia kura badala ya kuwaengue kabla ya kura.
 
Mkuu ungekuwa Fair kama ungekuja na Matokeo ya Viongozi wa Mikoa yote against Makabila yao, No Wonder ungekuta kwa Mbeya Mwenyekiti na katibu wote ni Wanyakyusa, so do mikoa mingine

haiwezekani wajumbe na viongozi wote wawe kabila moja.

mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dsm ni John Guninita sio mzaramo au mtu wa Dsm.anatoka Musoma.
Mwenyekiti wa Uwt mkoa wa Dsm ni Z.madabida ni mtu wa Rufiji.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Dsm ni Said kijana wa Tabora.
 
Naomba tuwe waangalifu tusitumiwe na yule mwovu (CCM). Habari hii ililetwa vibaya. Lengo lilikuwa lipi?

Hapo ndipo ambapo nyie wakereketwa wa CHADEMA-Family-Operation (au Origino) mnatukatishaga tamaa sisi wa CHADEMA-National-Party(ambayo tungependa iongozwe na Dr Slaa). Hebu tueleze, CCM inahusika vipi na mapambano kati ya Zitto na Mbowe mpaka kuwatupia lawama? Yaani Zitto hawezi kutaka kugombeya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA akijiona ana uwezo mpaka apate msukumo na CCM? Acheni hayo...

Ndio maana wasomaji waliotanguria walisemaga CHADEMA imekuwa kama CCM. Sasa namimi nakubalina nawo. Mkifurunda kwenye kambi yenu mnakimbilia kuwalaumu CCM. Mnakuwa kama CCM wanavyofanya kulaumu upinzani! Tena afadhali CCM walisuhusu demokrasia kwa kuwaruhusu Kikwete, Mondosha, Salim, Kigoda, na Sumaye kugombea na kuwapigia kura badala ya kuwaengue kabla ya kura.

Salamu kwenu wana JF. Natumaini nyote mu beheri waa afya, na leo tunaanza tena wiki ya mikiki mikiki kusaka riziki.

Ninatambua uchangiaji wa wana JF kuhusu ChaDEMA Taifa na Kilimanjaro.

Wasiwasi wangu hapa ni kuwa wachangiaji wengi ni wana CCM and so, wanajaribu kujifanya wachambuzi na viongozi wa kudhani lipi lafaa na bora kuliko lingine. Lakini wangepewa nafasi, holaaaaa!

1. Kwa taarifa yenu, Zitto alichukua form ili kuonyesha kuwa kuna makundi chadema lakini sivyo,.......it was a strategy kuwafungisha midomo wasioipenda chadema. Makubaliano yalikuwa CHUKUA FORM afu UJITOE. This is politics.

2. Uongozi wa Chadema kilimanjaro mbona unawaumizeni vichwa sana...wakati watu waligombea na kupewa kura....nyie mlitaka mwana mbilimbi aende na kupewa chama? Hivi political thinking za wengine zikoje? Ungepewa uongozi wewe na babayako ao another family member, ungekataa,,provided uliomba? Najua hamuwapendi wachaga, lakini ukweli haufichiki kuwa they are eligible and capable!

3. Chadema ni chama cha Demokrasia ya maendeleo, na Zitto amedhihirisha hilo,,,,,"najitoa chama kisigawanyike" hakuwa presurised. Kwa taarifa zenu, nilikuwa kwenye kikao cha wazee na najua kilichojiri. Mliotaka Ya lipumba na Safari yajiri chadema, poleni.
 
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=282
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kabwe Zitto, amesema hana mpango wa kuondoa fomu yake ya kugombea uenyekiti wa chama hicho, kwa kuwa ni haki yake na ana sifa za kuwa Mwenyekiti.

Pia Zitto amekanusha taarifa kuwa fomu zake zilirejeshwa na watu wanaoshinikiza awanie nafasi hiyo kwa lengo la kukibomoa chama hicho na kusema kama ni shinikizo basi ameshinikizwa na wana Chadema na si mtu wa pembeni. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Zitto alikiri kuchukua fomu na kufuata taratibu zinazotakiwa na kama kuna tofauti ni mbinu za kisiasa.

"Hii ni staili tu, nisingeweza kuchukua mdundiko, kwanza nilikuwa jimboni kisha nilikuwa na safari ya Ujerumani hata fomu zenyewe nilijazia Uwanjani (wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere)," alisema.

Aliongeza kuwa yamesemwa maneno mengi kumhusu pamoja na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ambayo aliyaita ya siasa za kampeni na kuwa anatarajia yatakwisha baada ya uchaguzi, kwa kuwa wote lengo lao ni kuimarisha chama hicho.

"Chama hiki si changu, wala si cha Mbowe, sisi tutaondoka chama kitabaki hapahapa na uamuzi wangu kugombea, ni jambo la kawaida wala sihitaji mpasuko au mgawanyiko, mwaka 1998 Bob Makani na Philemon Ndesamburo waligombea nafasi hii wakatofautiana, lakini baada ya uchaguzi, waliungana na kuendeleza chama," alisema Zitto.

Alisema alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa na uwezo wa kukipeleka mbali chama hicho na hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi, ambapo inatarajiwa kuwapo vijana wapya wapiga kura wapatao milioni 6.3 hivyo ni vyema chama kijipambanue kwa kuongozwa na kijana.

Alitamba kuwa anajiamini kuwa na uwezo katika kukiongoza chama hicho hasa ikizingatiwa kuwa katika nafasi yake ya ubunge wa Kigoma Kaskazini, ameongoza kamati muhimu ya Bunge, ya Hesabu za Mashirika ya Umma, iliyo na mashirika yenye thamani ya zaidi ya Sh trilioni tano.

"Nikiwa kijana kama wanavyodai, kwa nini niweze kuongoza kamati hiyo ila nishindwe chama chenye mapato ya Sh bilioni 72 kwa mwezi? Hata hivyo binafsi sikupenda kugombea uenyekiti, lakini nimeombwa sana na wanachama na kujikuta najaza fomu hizi," alisema.

Alisema amekuwa kwenye chama hicho tangu akiwa na umri wa miaka 16 na kupitia ngazi mbalimbali za uongozi ndani na nje ya chama hicho, hivyo anaamini sifa za kushika wadhifa huo anazo kwa kuwa anakifahamu vyema.

"Na itakuwa ni ajabu kutumiwa kukiharibu chama hiki, haya ni maneno ya siasa na yatakwisha kampeni zikimalizika," aliongeza.

Aliwataka waliozusha na kutunga uongo dhidi yake, watambue kuwa yeye si mtu wa visasi, lakini pia uchaguzi unapita na maisha baada ya hapo yataendelea, lakini pia akasema haamini kama chama hicho kimetawaliwa na ukabila kama inavyodaiwa.

Hata hivyo, alionyesha masikitiko yake kwa gazeti linalotoka kila siku lililoandika habari dhidi yake ikionesha wazi kuwa linatumiwa, na hivyo kuleta dhana kwamba ukabila ndani ya chama hicho upo, kwa kuwa gazeti hilo mmiliki na mhariri wake ni Wachaga.

"Hata hivyo, nikichaguliwa kuwa Mwenyekiti dhana hiyo ya ukabila itaacha kuwa na nguvu," alisema. Alisema leo wazee wa chama hicho wanatarajia kukutana na wagombea hao wawili kujadili na kuangalia tofauti zilizojitokeza. Wanaotarajiwa kukutana ni Profesa Mwesiga Baregu, Bob Makani, Anthony Ngaiza na Edwin Mtei.

Amankatoshi haya ni maneno ya Zitto, kama ilikuwa mpango achukue fomu halafu ajitoe kwanini Kibanda alijisajiri hapa JF na kuwatukana matusi ya nguoni kina KITILA na vijana wengi wa Chadema? mpasuko na heshima ya Chadema imekwisha potea.
 
blank.gif
• Zitto asema anamheshimu, hana kinyongo

na Mwandishi Wetu


amka2.gif

HATIMAYE, washindani wakuu wawili katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Zitto Kabwe, jana walimaliza upinzani kwa kushikana mikono, kuashiria mshikamano na umoja katika chama hicho.

Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa anayemaliza muda wake, na Zitto ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, walifikia hatua hiyo, ikiwa ni siku moja tu tangu Zitto awasilishe barua mbele ya Baraza la Wazee, kuondoa jina lake katika kinyang'anyiro hicho.

Viongozi hao walifikia hatua hiyo katika kikao cha Kamati Kuu (CC), kilichofanyika katika Hoteli ya Keys iliyoko Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Habari ambazo Tanzania Daima ilizipata kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kuwa, Zitto ambaye uamuzi wake wa kuchukua fomu uliibua mjadala mzito ndani na nje ya nchi, alitoa kauli iliyoashiria wazi kumaliza upinzani uliojitokeza tangu alipochukua fomu.

Kwa hatua hiyo ni dhahiri kuwa Mbowe ana nafasi kubwa ya kupitishwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na wale wa Baraza Kuu, kabla ya kupigiwa kura na Mkutano Mkuu, unaotarajiwa kufanyika Septemba 4.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms), Zitto alisema amekubali kujitoa ili kuweka mbele umoja wa chama.

"Namheshimu sana Mbowe na wewe unajua. Wala siwezi kumvunjia heshima. Nimekubali kujitoa ili kuweka mbele umoja wa chama. Kama nimeyumba ni kwa ajili ya kukienzi chama, suala la uenyekiti limepita na sasa naangalia mbele kujenga chama. Mimi sina kinyongo," alisema Zitto.

Katika hatua nyingine, CC imepitisha jina la Mbowe kuwa mgombea pekee wa nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho taifa.

Mbali ya kupitisha jina la Mbowe, CC pia imeridhia uamuzi wa Zitto kujitoa kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa chama hicho.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya kikao zilisema kuwa, CC imefikia uamuzi huo ili kumpa nafasi zaidi Mbowe ambaye katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, amefanya kazi kubwa ya kukiimarisha chama hicho kwa kiasi cha kukubalika na Watanzania wengi.

"Kamati Kuu imepitisha jina la Mbowe, pia imeridhia barua ya Zitto, hakukuwa na matatizo kupitisha jina hilo, na Zitto ametoa kauli nzuri yenye kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama, tofauti kabisa na taswira iliyokuwa inaonyeshwa na baadhi ya vyombo vya habari," alisema mmoja wa wajumbe wa mkutano huo.

Hata hivyo, Kamati Kuu hiyo ilikuwa ikiendelea kupitisha wagombea wa nafasi nyingine ya Makamu Mwenyekiti, ambayo inawaniwa na watu wanne.

Zitto, aliwasilisha barua yake ya kujitoa katika mchuano huo juzi asubuhi.

Kabla ya Zitto kuwasilisha barua yake hiyo, alikuwa ameitwa kuhojiwa na Baraza la Wazee wa chama hicho linaloongozwa na Mwenyekiti mstaafu, Edwin Mtei.

Wakati akiwa katikati ya mahojiano hayo, Zitto aliwasilisha barua yake ya kuamua kujitoa, akisema anafanya hivyo ili kurejesha umoja na mshikamano ndani ya chama, ambao unaweza kupotea kutokana na kugombea nafasi hiyo na mwenyekiti wake.

Uamuzi wa Zitto kujitoa katika mchuano huo, umekuja siku kadhaa baada ya hatua yake ya kugombea kiti hicho kuzusha mjadala mkali ndani na nje ya nchi.

Kuibuka kwa mjadala huo, kwa kiwango kikubwa kumetokana na hatua ya mwanasiasa huyo kijana na mwenye ushawishi bungeni, kuamua kukabiliana na Mbowe.

Uamuzi huo wa Zitto, ulionekana kuwashtua viongozi mbalimbali wa juu na wazee wa chama hicho.

Mbali ya hao, uamuzi huo ulikwenda mbele zaidi na kugusa mijadala ndani ya vyama vingine vya siasa, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM), CUF, NCCR- Mageuzi na TLP.
Makada kadhaa wa CCM waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti walisema, mabadiliko ya uongozi ndani ya CHADEMA ni jambo linalofuatiliwa kwa karibu.

Ukikiacha chama hicho tawala, uamuzi huo wa Zitto kugombea uenyekiti na kuchuana na Mbowe, ulionekana kuungwa mkono na wakati mwingine kushangiliwa na viongozi wa vyama vingine vya upinzani.
Hata hivyo, kikubwa kilichokuwa kikivuta hisia za watu wengi ni madai ambayo Zitto mwenyewe aliyakanusha mara kadhaa kwamba, uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama hicho ulikuwa na msukumo kutoka nje ya CHADEMA.

Maandishi ya Kibanda kwenye Tanzania Daima amefurahi kiasi cha kurudiarudia maneno.Mzee Mtei ameonesha ubaguzi wa wazi kwa kuwa mwenyekiti wa kikundi cha wazee wenye Chama ambao wamemzuia Zitto.kisheria kutokana na mgongano wa kimaslahi Mzee Mtei hakutakiwa kushiriki kikao hicho kwani Mbowe ni Mwanawe/Mkwe wake.ilitakiwa Mwanasheria wa Chadema apinge ushiriki wa Mzee Mtei kwenye hili kwani Zitto hatendewi Haki.
blank.gif
 
Last edited:
wana sheria swali? Mzee Mtei kaongoza kikao cha wazee wa Chadema kumuondoa Zitto.wakati yeye akiwa ni mkwe/ mzazi wa Mbowe jee hakuna mgongano wa Kimaslahi?
 
Edwin Mtei ambaye aliongoza kundi la wazee wanne wa Chadema ambao walimshurutisha Zitto Kabwe kujitoa kwenye uchaguzi wa Chadema na kumpa nafasi Mbowe.

swali la kisheria Mzee Mtei kuongoza kikao hicho na kuwa upande wa Mtoto wake/Mkwe bwana Mbowe inakubalika kisheria?hakuna mgongano wa kimaslahi?

maamuzi ya wazee hawa ni halali? jee kazi ya CC na mkutano mkuu wa Chadema ni nini? kwanini CC ya Chadema isifanye kazi hii ya wazee wanne kuwanyima haki wanaChADEMA wengi?
 
Naomba niseme kwamba mimi sio mwana Chadema. Si mwanchama wa chama chochote cha siasa. Ninachojali ni udhoofu wa sasa wa hali ya siasa na maendeleo ya Tanzania.

Nategemea CCM wangolewe na upinzani mwakani. Na kutokana na hali ilivyo, tegemeo langu ni kwamba Chadema itaongooza wapinzani ili waikomboe nchi toka kwenye mikono ya hao wanaozidi kuiangamiza.

Mbinu zozote za kuigawa Chadema zinanichukiza. Mbinu za kuwagawa Watanzania waliojiunga na JF ili kushirikiana kuleta mabadiliko, zinaniudhi. Kwa maoni yangu, ni CCM ndiyo inaweza kuwa na mipango ya kuwagawa Watanzania, hasa hawa walioko hapa JF.

Support inayopata Chadema hapa sio kitu kidogo. Kama kukiweko na habari za kupotosha hapa na kuwahimiza wana JF kwamba Chadema imekuwa chama cha kidikteta, na wana JF wengi wakahadaika kirahisi, basi sina budi kusikitika sana.

I do not have the latest news, as I live half a world away from Dar. But from what I have read on JF, there was no ban on Zitto’s wish to be the Chairman of Chadema. Why was the fact that he was advised to withdraw presented as dictatorship? Why was there a rush to persuade people that Chadema is bad? Why should I not suspect that there are evil intentions?

I call on all of us to set this matter aside and revert to our initial focus on how to bring change to our motherland.
 
Kwa mtazamo wangu,mkutano wa CHADEMA wa sept 04 unafaa kususiwa na kila mpenda demokrasia,kwani badala ya kuhubiri uchaguzi huru umegeuka kuwa "mchakato wa kasumba ya nje ya demokrasia wa kurithishana madaraka"na kutumia njia za hila za kuingiliwa na waasisi kuombwa kujitoa kwa mwanachama yeyote anayetaka kupambana na incumbents kwenye sanduku la kura !

Kwa nini uitwe uchaguzi ili hali mwanachama halali akiamua kugombea hasa kushindana na incumbents wanaombwa wajitoe kwenye kinyang'anyiro hicho?Kwa nini unaitwa uchaguzi hasa pale wazee wa chama wanapotueleza kwa vitendo kuwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA-kitaifa kuwa hawapingiki kwenye sanduku la kura?

Huu ni ubabaishaji mkubwa sana wa kisiasa kushuhudiwa na mimi hasa kwa chama cha mageuzi kama CHADEMA kwa kasumba hii mpya ya kamati kuu kuteua wateule wasiopingwa then mkutano mkuu kazi yao kuthibitisha tu.

Unaweza kuupa jina jipya mkusanyiko wa CHADEMA wa sept 4,lkn hamna hata sababu moja kwangu utakaoufanya mkusanyiko huu mkubwa wa CHADEMA uitwe ni uchaguzi,labda tuite"uchaguzi maalum wa CHADEMA wenye menifesto mpya unaosema "Mwenyekiti Mbowe kwa vyovyote hatakiwi kuwa na mpinzani ndani ya chaguzi za CHADEMA"!

Nimekuwa wa kwanza kutangaza kuwa nasusia habari zozote za uchaguzi huu na rasmi nauita sio uchaguzi bali ni mkusanyiko wa baadhi ya watu wenye madaraka ndani ya CHADEMA walioitana ili kuendelea kurithishana madaraka!
 
Nilipinga sana Zitto kuwa mwenyekiti wa Chama, kwenye chama bwana huhitaji watu kama Zitto... Zitto anatakiwa kwenye utendaji sio kuwa mwenyekiti... in short ulikosea kaka... na kwa kweli nilivyofikiri imekuwa hivyo hivyo... Zitto Rungu la spika limekupitia mara nyingi sio kwa sababu ya hoja za kupinga bali... kushindwa kutumia maneno stahiki kwenye kutetea hoja... kwenye chama ndio ingekuwa ovyo zaidi.

Sijui ni kwanini saa nyingine hatukubali kutokubaliana na matakwa yako binafsi...
 
Hivyo basi tunapenda kuwafahamisha Wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa hii ndio ratiba yetu rasmi ya kuingia kwenye uchaguzi Mkuu wa Chama na pia ni hatua muhimu sana katika Mapambano yetu dhidi ya Mafisadi na Ufisadi na kuhamasisha uwajibikaji na kutetea rasilimali za Taifa.

Ni muhimu ikazingatiwa kuwa ndani ya CHADEMA kila Mwanachama anayo haki ya kugombea nafasi yeyote ile kwa mujibu wa Katiba ya Chama,hivyo basi kila Mwanachama atumie haki yake ya kidemokrasia kuchukua fomu .

Ahsante sana kwa ushirikiano wenu.

………………
Dr. Willibrod P. Slaa (Mb)
Katibu Mkuu.
19/08/2009.


In the light of the recent “not-so-private” power struggle between Zitto, the “charismatic and aspiring” Wannabe Chairman and Mbowe the “firmly entrenched and not going anywhere (over my dead body)” current Chairman, would it be prudent to take the above statement with a grain of salt? Or would that be an unreasonable overreaction to a minor personality conflict that will be no more destructive to CHADEMA than the recent CCM NEC meeting held in Dodoma?

Should I trust the CHADEMA politicians brand more than other parties since I want to believe that they always tell truth, the whole truth, nothing but the truth? I am struggling with the uncomfortable feeling that I have of being taken to the cleaners once again by politicians and my initial instinct having been burnt so many time is to try to resist so I don’t fall for it hook, line and sinker!

Any enlightening views or advice from JF readers?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom