Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Kama mlidhani mpango wenu wa kumfrustrate KABOUROU hadi akaamua kuwazilia na kujiunga na CCM basi mjue tu kwa Zitto mmenoa. Chadema ni chama cha wote na zaidi ni chama cha wanaotaka mabadiliko ya kweli na ambayo yataanzia ndani kabla ya kwenda nje.

Na mkiendelea na spin zenu za style ya zilipendwa msidhani kuwa Zitto atawanyamazia mmumalize kimyakimya kama mlivyofanikiwa kwa wengine. Zitto wako maelefu na kamwe hamuwezi kusimama kimbunga chake...

Tatizo mnachukulia uaminif wa watu wa Kigoma kama weakness. Hapo mmevaa kisiki na kitawatoa hata ulimi...

Hamuoni haya hadi mnamtumia Mzee wenu Mtei kuspin maneno yake.....yaani msivyokuwa makini mpoa tayari hata kuharibu stature ya MTEI ili mradi mfanikiwe mradi wenu wa kummaliza Zitto kisiasa na baadae mfanye mengine.

Na huu uroda wa kutumia magazeti ya mfadhili wenu ambaye ana crusade yake binafsi dhidi ya Zitto kwa sababu ya Zitto kukataa kumsujudia soon utawatokea puani......

omarilyas

Omarilyas,

Mbona vitisho mkuu.... si mfanye tu mnachotaka kufanya mapema kuliko kusubiri? Kama CHADEMA imewashinda, mnaweza kutoka tu na kwenda kwa Kikwete na chama lake la kijani.

Zitto ametoa tuhuma kali sana hapa jukwaani, sioni tofauti ya hicho na kile unachodai hapa kuwa upande mwingine wa CHADEMA umefanya.
 
Kitendo cha CHADEMA kumtuhumu Zitto waziwazi kuwa anatumiwa na mafisadi na kwamba katoa rushwa kwenye uchaguzi wa Vijana pamoja na kumhusisha mama yake mzazi ndo kimepelekea Zitto kuja na haya.Swali je?,ilikuwa ni sahihi kwa baadhi ya viongoiz/wazee wa CHADEMA kumtuhumu Zitto waziwazi kuwa anatumiwa na mafisadi na ni mtoa Rushwa???,Zitto alitendewa haki katika kuchafuliwa hukU???

Hii ndio siasa mkuu. Ni contact sport. Zitto na CHADEMA hawakuanza kuwa mbali leo. Maandishi ya Zitto hapa jukwaaani yamefunua mengi sana kuhusu uhusiano wao.
 
Kitendo cha CHADEMA kumtuhumu Zitto waziwazi kuwa anatumiwa na mafisadi na kwamba katoa rushwa kwenye uchaguzi wa Vijana pamoja na kumhusisha mama yake mzazi ndo kimepelekea Zitto kuja na haya.Swali je?,ilikuwa ni sahihi kwa baadhi ya viongoiz/wazee wa CHADEMA kumtuhumu Zitto waziwazi kuwa anatumiwa na mafisadi na ni mtoa Rushwa???,Zitto alitendewa haki katika kuchafuliwa hukU???
Hapana mkuu wangu kwani kipi kilichotangulia? Uchaguzi wa vijana Chadema au Zitto kuchukua form na kukataliwa..Hizi habari za uchaguzi wa Vijana ni kibwagizo tu mkuu wangu hawa watu wanatafutana muda sasa hivi na imefikia mahala uungwana wao umeshindikana. Subira imtenguka na Mwenyezi Mungu hapendi mtu asokuwa na subira kwani humpa Sheitan nafasi kirahisi kushika usukani..!
Nimesoma mada kibao humu JF na nimeweza kuwajua watu wa Zitto na wale Mbowe.

Kinachonishinda kuelewa ni kwamba Zitto na Mbowe ni washikaji iweje hizi fujo zianzishwe na watu hawa.
Kwa mfano Zitto analalamika kuhusu mama yake lakini naona sehemu Nyingi akizungumzwa Baba mkwe wake Mbowe na sioni watu wa Zitto wakielewa utovu wa heshima ktk kutumia jina la mzee Mtei kama wanavyoona Utovu kwa mama yake Zitto.
Yaani ni comedy tupu kiasi kwamba inachekesha, inachefua na kikubwa zaidi kutueleza kwamba Tanzania hatuna Upinzani..
 
siamini kama zitto anaweza kuandika hayo...maana maadui zake na chama chake wanaweza kuyatumia vibaya....wataunganisha dots na maneno ya yule kijana ..aliyefungwa dodoma itakuwa hatari hapo...

sawa sawa kabisa mkuu PM, heshima mbele yaani siamini amini hivi!
 
Mama Zitto afyatuka, uchaguzi Chadema wafutwa
MAMA mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto amesema, mwanae si fisadi na hanunuliki.

Amesema, viongozi katika makao makuu ya chama hicho ni 'wachafu', wanakiharibu chama.

Shida Salum amesema, Zitto hanunuliki na hawezi kununuliwa. Amesema leo Dar es Salaam kuwa, ofisi ya Makao Makuu ya Chadema itakiharibu chama hicho na anasikia aibu mwanae kutajwa kuwa ni mmoja wa mafisadi katika chama hicho.

Mwanachama huyo wa Chadema amesema, ofisi ya Makao Makuu Chadema imeingiliwa, na kwamba, chama hicho kimechafuka.

Salum ameyasema hayo mara baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kufungua mkutano wa uchaguzi wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA).

“Mimi fomu ya Zitto niliifukiza nyumbani kwangu, Zitto sio fisadi, hanunuliki na hawezi kununuliwa,” amesema mama Zitto.

Amesema,amekuwa katika chama hicho tangu mwaka 1992, na anasikia aibu sana zinapoibuka taarifa sasa kwamba mwanae ni miongoni mwa mafisadi.

Alisema amekuwa akifika katika ofisi ya makao makuu kila mara kuomba kuonana na Katibu Mkuu (Slaa) ili wazungumze kuhusu viongozi wanaomharibia chama,na wanaotaka kukigawa chama.

“Siwezi kumkataa Zitto, katika uchaguzi huu ofisi imeingiliwa, jirekebisheni, chama kimechafuka, hali ambayo inafanya watu kukiogopa chama,” amesema Mama huyo huku akishangiliwa na umati mkubwa wa kina mama waliofika kwa ajili ya uchaguzi huo.

Muda mfupi baada ya mama Zitto kuzungumza, Mwenyekiti wa Wanawake mkoa wa Dodoma, Sakina Sare, alisema yapo matatizo ya kiutendaji ndani ya viongozi wa makao makuu ya chama.

Amesema yeye aliingia kwenye chama tangu 1994,amewataka viongozi wa Chadema kuwasikiliza wanachama wake ikiwa ni pamoja na kupokea matatizo yao.

“Kwa mfano, leo tunakaa katika uchaguzi wa Baraza la Wanawake, wakati huo huo fomu za kushiriki katika uchaguzi hazikuwafikia walengwa, hazikupatikana,” amesema Sakina.

Amesema ipo haja kwa makatibu wakuu wa mikoa kuangaliwa kwa makini ili chama kisigawanyike au kutoa taswira mbaya kwa wengine.

Aliyekuwa Katibu wa wanawake katika mkoa wa Kagera, aliyefahamika kwa jina moja Ramlaza, alisema wanachama wamekuwa na manung'uniko mengi kuhusiana na uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kutopata fomu za ushiriki.

Amesema, maeneo mengine fomu za wagombea zilichelewa hivyo kuonesha utendaji dhaifu kwa ofisi ya makao makuu ya chama.

Dk. Slaa amewaomba radhi lakini amesisitiza kuwa, kama shutuma zilizotolewa na Mama yake Zitto ni za kweli basi hata mwanae ni mmoja wa viongozi wa chama hicho.

“Katika hili la Mama yake Zitto siwezi kusema lolote, mimi ni Katibu Mkuu, mwanae Zitto ni Naibu Katibu, hivyo kama anaushutumu uongozi wa chama makao makuu, hata mwanae yupo katika kundi hilo,” amesema Dk. Slaa.

Dk Slaa amesema, anafahamu kwamba, mafisadi wanawatumia vijana ndani ya chama hicho, atawafuatilia na kuchukua hatua dhidi yao kwa sababu chama hakitoruhusu kuyumbishwa ama kuwepo kwa makundi.

Wakati anafungua mkutano huo, Dk. Slaa aliwataka wanachama hao kutamka hadharani kama kuna mianya ya rushwa ndani ya chama hicho katika mchakato huo wa uchaguzi.

Alisema asiyetamka hadharani kama kuna sura hiyo, hizo zitakuwa propaganda za kisiasa, na kwamba, hawataacha kupambana na ufisadi.

Aidha, alisema chama kimeletewa taarifa kwamba watu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanasambaza kitabu cha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, marehemu Chacha Wangwe.

Alisema yeye binafsi hana matatizo na kitabu hicho lakini anahofia yayliyomo ndani kwa kuwa CCM ilianza kutoa waraka wa wangwe Julai 27, 2008 siku moja kabla ya kifo chake.

“Kwa maana hiyo CCM walijua fika kuwa Chacha angekufa? Na kwa nini waraka huo ulitolewa na ofisi ya katibu Mkuu CCM Dodoma,? Alihoji Dk. Slaa wakati akiwaeleza wanawake hao kujihadhari kwa kuwa si kila mwanachama ni mwema.

Amesema, hoja inapoingizwa ndani ya chama lazima wawe makini na waijadili kwa kina bila kuzembea.

Kuhusu uchaguzi wa Baraza Kuu la vijana, alisema alipata taarifa jana usiku saa 3:00 kwamba zimetokea vurugu hivyo wanahitaji ushauri.

Alisema alizungumza na vijana takribani 110 usiku huo, wakitoa malalamiko yao kadhaa.

Amesema miongoni mwa malalamiko waliyotoa vijana hao ni pamoja na kuwepo kwa sura ya fedha kutembea ndani ya uchaguzi, wagombea kugawa karatasi za kupigia kura, na idadi ya kura kuongezeka.

Dk. Slaa alisema kutokana na hali hiyo, ilibidi kuitisha kikao cha dharura huku akiwa amewashirikisha baadhi ya wazee ambao kwa pamoja walikubaliana kuufuta uchaguzi huo, utafanyika ndani ya miezi sita.
 
Kitendo cha CHADEMA kumtuhumu Zitto waziwazi kuwa anatumiwa na mafisadi na kwamba katoa rushwa kwenye uchaguzi wa Vijana pamoja na kumhusisha mama yake mzazi ndo kimepelekea Zitto kuja na haya.Swali je?,ilikuwa ni sahihi kwa baadhi ya viongoiz/wazee wa CHADEMA kumtuhumu Zitto waziwazi kuwa anatumiwa na mafisadi na ni mtoa Rushwa???,Zitto alitendewa haki katika kuchafuliwa hukU???

Ubarikiwe, we need people like you! the guy could be frustrated and his only hope was may be JF , JF is like this!!!!! jamani hata kwenye movie askari akipigwa vita mnamnyenyua!!!

Mkulu Zitto,

Ni wewe umeandika hayo! Siamini! Naomba Mungu waandishi wanaochukua habari hapa JF wasiione hii, maana wakiiweka kwenye media sijui utapita wapi?

Yaano mkuu unaandika in plural kuwa mlimtenda Wangwe kwenye public from kama hii, kisha ulitaka kuwa mwenyekiti wa chama? Are u kidding us or what?

Okay, sijui imekaaje lakini huoni kama inaweza kuwa activate polisi kufatilia what exactly hapenned?

Yaani unadhani hapa Jf watu watakuona wa maana kwa 'kuropoka' huku ulikofanya? OOh my God, nadhani tulikuwa hatukufahamu vizuri,

na tutajuuuuuuuuuuta kukuufahamu! au mtu kaiba password?

Hili bandiko will go down in history be it your rise or ur fall.

Umbumbumbu, people can say truth, this will make them free, many great politician they have done so! siasa ndivyo ilivyo kwani wewe ulikuwa hujui? MTEI kusema Zitto alipewa hela na CCM, wanampeleka wapi? kwa nini asiwaambie anajua mchezo wao? kwani CHADEMA WANAMUOGOPEA NINI ZITO??

Sidhani kama Zitto alifikiria hili kabla ya kuandika hayo hapo juu. Ile kesi ya kifo cha Wangwe inaweza kufunguliwa muda wowote na maneno ya Zitto yakatumika kuisaidia polisi.

Anyway ... kijana bado anajifunza siasa za bongo. Akikuwa na kukomaa ataelewa cha kufanya na kusema.

Unaogopa kesi, yeye anagopa kuuliwa? yeye alichosema ni kuwa walisema Wangwe kapewa hela na CCM! hajasema swala la kumuua! inaonekana un apenda vijiwe

Yaani nakwambia .... muda si mrefu utasikia waziri wa fedha Mkullo katupwa nje na Zitto kapewa uwaziri na Kikwete (si unajua tena kulipa fadhila za jinsi Zitto alivyoimaliza issue ya Buzwagi kwa kuingia kwenye kamati ya madini ya Kikwete).

Zito kwa maneno yake hataenda CCM, naamini hivyo , I know the guy, wewe uko upande wa Mtei wa kudhania Zitto kapewa reushwa. Hivi hatuwezi kuuliza baadhi ya mambo kwa wapinzani wenzangu, nikitofautiana nao tu basi mimi fisadi???

Hizi sasa ni double standards!Walipotoka ktk vikao vyao CCM zilianzishwa thread za yale yaliyosemwa na yalisemwa na nani....Zikamwagika thanx kama mvua!Leo yanasemwa ya vikao vya CHADEMA wanaanza oh,siri oh yandani....Two wrongs don make a right,yes...Lakini hii ya kushangilia ya upande mmoja tu as if they are public infos sio sahihi kwa mtazamo wangu.

There you are!

Mkandara hueleweki kosa gani Zitto kafanya? Robin Cook aliyekuwa waziri wa nje wa Labour aliweka wazi uozo wa Chama chake kwenda Iraq.soma ROBIN COOK THE POINT OF DEPARTURE ISBN 0-7432-5255-1
plz mwache Zitto yeye wamemzuia na mgombea wake kazuiliwa haki iko wapi?
Nadhani umemjibu na KAizer pia! this is ommon , waliozowea vijiweni tu ndio wanaona ajabu!

duh zitto kwa uhakika tu na kama unaelewa huu ndo mwisho wa kuvuma kwako,nadhani umri unakuponza kichwa kikakua,sasa unaleta vurugu katika chama na wala hauleti uelewano,wewe kama kiongozi wa juu na mwenye akili na mtaka mageuzi hukupaswa kwanza kuwa na MAKUNDI sasa,unataka kutuambia ungeshinda uenyekiti ndo ungefanyaje?ungeadhibu wale usiowapenda then chama kinadhoofika,wewe kwa ufupi huwezi madaraka,hufai kabisa,kama umepewa hela kuharibu demokrasia si useme?

Mwisho wake kwa sababu wewe umesema? kwani Zito alitaka kuvuma au nyie ndio mmevumisha?? yeye anapiga kazi na kusimamia mawazo yake kuvuma na wewe , mwenzako mbunge, wewe nani?

Hakuna cha mwisho
hao wanaoandika humu na kuleta habari ni viongozi wa juu wa chadema,ama kosa la kuisha kwa Zitto ni kujisajiri kwa jina lake halisi.?

Haishi mtu ukweli lazima tuuseme ukweli ,hakuna cha siri hizi siri mnazoongelea ni hizo za staili ya kumpoteza Wangwe ama siri zipi?

Hata mimi nashangaa!
 
Sasa nimeamini kuwa wananchi tuna safari ndefu ya kufika kanani...

Juzi CCM walikuwa na mtafaruku mkubwa kuliko huu wa CHADEMA ....wakapigana kwenye kamati kuu wametoka ..angalau hawakuja hapa kuanikana...

Wapinzani sasa mmejeuza jamboforums kuwa kamati kuu ya CHADEMA????....KWANINI mambo yenu ya ndani yasiishie ndani....hamuoni kuwa kwa mara nyingine mnawakatisha tamaa wananchi!!????

Tangu mwaka 1992 tunapambana tumeona wapinzani wakiendelea kuumizwa kwa mambo kama haya ...NCCR ya mwaka 1989 ilikuwa moto na wasomi wote ....lakini kumbe lilikuwa gari la UT la kusanya wapinzani waliokuwa wakichomoza....walishindwa kuifanya NCCR KUWA CHAMA PEKEE...

KAMAHURU na baadaye CUF ...baada ya kuungana na JAMES MAPALALA....yuko wapi mapalala?????

MREMA ..aliyevuma kama tsunami ...yupo wapi????

CHADEMA ambacho mwanzo kilikuwa chama wachache makini kisicho kuwa na watu....wengi ,miaka yote nyuma kilikuwa hakioneshi cheche..tunashukuru vijana mliochukua madaraka baada ya wazee...MTEI NA BOB MAKANI....miaka hii mitano tumeona mnapanuka na kuwapa matumaini wananchi kwa kasi ya ajabu .....sasa kwanini mnafikia kuja kuvuana nguo hapa....mmekosa vikao...

kwanini CHADEMA mnataka kuwasaliti watanzania??/

ni CHAMA gani hakina siri za ndani??? haata ndoa ina siri....na siri ni siri..???...miliosoma vitabu vya siasa mnajuwa ...wanachowashinda CCM ndio hicho...?? watu wao wameapa kutunza siri...hata waulizeni waliokuwa humo..watawambia...

chukulia mfano wa mtu kama MREMA ..Pamoja na uropokaji wake ...mambo aliyoyajuwa kwa kiapo ambayo anajuwa akiongea itakuwa kinyume hajapata kuyasema..nasema hivyo kwa sababu kuna mengi tumepata kumuuliza..anazungusha...!..anajuwa maana ya siri na adhabu ya kutowa siri anaijuwa!

Tena wapinzani mjuwe ikiwa umeenda ccm unaweza kuongea porojo zote lakini ukisema siri ambayo imekuwa rated secret...simply they kill you!!! mifano mnayo...!!!...sitaki wapinzani mfikie huuko lakini lazima mjuwe hamtakiwi kukwaruzana na kuwayumbisha wananchi namna hii......

CCM waanajuwa kuwagombanisha .....na wanaofanikiwa huzawadiwa vyeo lakini tayari wanakuwa wameshajiaharibia historia na kubeba usaliti...

watu kama ....lamwai,hizza,akwilombe.,kaborou[aliyekuwa kipenzi cha wananchi]....leo hii wakitokea mbele ya wananchi hata wanaona haya ...ukiachilia mtu kama hizza ambaye anajulikana ni mpiga domo...hawa wasomi wengine...dhamira zinawasuta....na tayari wamekosa uhalali mbele ya macho ya watu!!

....tunaomba vita dhidi ya ufisadi isitumike vibaya kuyumbisha wananchi...narejea maneno ya POLYCAP CARDINAL PENGO.."wanaopingana na ufisadi lazima wajiulize wanapigana toka moyoni au wanapigana kwa kuwa tu na wao wamekosa fursa ya kuwa mafisadi....""

CHADEMA MSIKUBALI KUTUMIWA NA MAFISADI AU HATA HAO MAKAMANDA WA MAFISADI...KWANI WANANCHI WOTE WANAJUWA NYIE NDIO WAAZILISHI WA HII VITA....MBOWE .,SLAA,...ZITTO NA WABUNGE WOTE WA CHADEMA ....SASA IWEJE LEO MNAKUBALI KUWA UNDERDOGS......ITAKUWA NI FURAHA SANA KWA MKIFARAKANA KAMA HIZI...NAPATA PICHA WANAKUNYWA MVINYO SASA.......

MSITUPELEKE HUKO!!!
Ndugu yangu kwa haya mashairi hasa ya leo, nina uchungu mkubwa sana. Bora ningekuwa mwanamke mwenye ujauzito kwani ningejifungua.
 
Yaani nakwambia .... muda si mrefu utasikia waziri wa fedha Mkullo katupwa nje na Zitto kapewa uwaziri na Kikwete (si unajua tena kulipa fadhila za jinsi Zitto alivyoimaliza issue ya Buzwagi kwa kuingia kwenye kamati ya madini ya Kikwete).

Unajua vyama vya upinzani vimezoea cut and paste style katika propaganda. Ndio maana CCM wanawapiga mabao kilaini.

Hii style ya kujenga taswira ya usaliti dhidi ya washindani wa ndani imekuwa kama historia.

Kila anayeamua kusimama kidete dhidi ya uovu wa ndani basi huyo ni wa kupandikizwa ama amenunuliwa. Kama vile humo kwenye vyama vyao ni sawa na makazi ya malaika yasiyo na doa.

Hivi tumejiuliza ni kwanini kila anayetofautiana na wenzake katika vyama hivi kuanzia enzi za Marandu, Mrema, Kaborou, Tambwe, Chacha, Akwilombe na wengine wengi huwa wanakuwa na kosa moja kubwa.....wanatumiwa na CCM ama Mashushu...Its che cut and paste propaganda...

Wangekuwa madarakani wangeishia yaleyale ya Lukuvi kuwa hawa ni wahaini. Ni bora tukang'amua ukweli sasa kabla hatujafika kuaminiana dola.

Wakati umefika kuyasma haya wazi na kuwalazimisha watu wajifanyie sekf reflection kujua ni wapi nao wanakuwa sehemu ya tatizo badala ya kukimbilia kutafuta uchawi....hasa kwa kumsingizia kizee wa jirani.

Zitto yupo na atakuwepo humohumo, mtabanana naye hukohuko na kama mnadhani huo umafia wa kuchonga utawasaidia mjue wapo wengi wa aian yenu nyuma yake.....

omarilyas
 
Umbumbumbu, people can say truth, this will make them free, many great politician they have done so! siasa ndivyo ilivyo kwani wewe ulikuwa hujui? MTEI kusema Zitto alipewa hela na CCM, wanampeleka wapi? kwa nini asiwaambie anajua mchezo wao? kwani CHADEMA WANAMUOGOPEA NINI ZITO??

Mkuu Waberoya, heshima mbele. Ukweli unaposemwa bila hekima hupoteza maana yake mara moja. Sio suala la kutoka kifua mbale na kujidai unasema 'ukweli' bila kupima kwanza athari zitakazotokana na wewe kusema huo ukweli, bila kutaja kuwa unaposema ukweli busara inadai pia uwe huna mawaa yanayokuzungua. Kwa hili, hata kama Zitto kasema 'ukweli', ametujuza kuwa katika ukweli huo alishiriki kumtenda Marehemu Chacha Wangwe!

Hilo la Mtei, wenye busara wamejua namna ya kulihandle, hawakuja 'kuropoka' hapa JF!
 
Where is Dr. slaa???

Maana Chadema inabidi tuwaulize, Slaa kwa nini umemwacha Zito?? what happened??
Zitto is alone, seems frustrated, no where to runm, JF juzi alikuwa shujaa, leo tunamtupa,

Slaa wehere is your stand regarding Zito, mtei, Mbowe SAGA???

Wewe uko upande gani, na maoni yako ni nini kufuatana na Zito kuambiwa ajitoe??

PIGA UA CHADEMA IS SLAA and ZITTO!!!!!!!!! na kati yenu nyie angechukua form, mgepata viti vingi sana vya ubunge, Zito angekomba vijana na angeleta msisimko, au wewe pia unge penya na kuchota watu wa rika zote!

Tukiona watu kama wewe mko humo humo na mambo yako hivyo we must question where is Slaa and where is he standing???
 
Ubarikiwe, we need people like you! the guy could be frustrated and his only hope was may be JF , JF is like this!!!!! jamani hata kwenye movie askari akipigwa vita mnamnyenyua!!!

Umbumbumbu, people can say truth, this will make them free, many great politician they have done so! siasa ndivyo ilivyo kwani wewe ulikuwa hujui? MTEI kusema Zitto alipewa hela na CCM, wanampeleka wapi? kwa nini asiwaambie anajua mchezo wao? kwani CHADEMA WANAMUOGOPEA NINI ZITO??

Unaogopa kesi, yeye anagopa kuuliwa? yeye alichosema ni kuwa walisema Wangwe kapewa hela na CCM! hajasema swala la kumuua! inaonekana un apenda vijiwe

Zito kwa maneno yake hataenda CCM, naamini hivyo , I know the guy, wewe uko upande wa Mtei wa kudhania Zitto kapewa reushwa. Hivi hatuwezi kuuliza baadhi ya mambo kwa wapinzani wenzangu, nikitofautiana nao tu basi mimi fisadi???

There you are!

Nadhani umemjibu na KAizer pia! this is ommon , waliozowea vijiweni tu ndio wanaona ajabu!

Mwisho wake kwa sababu wewe umesema? kwani Zito alitaka kuvuma au nyie ndio mmevumisha?? yeye anapiga kazi na kusimamia mawazo yake kuvuma na wewe , mwenzako mbunge, wewe nani?

Hata mimi nashangaa!

Kama uko upande wa Zitto na haya ndiyo unaandika, basi umethibitisha kuwa Zitto anatafuta pa kutokea ili aende chama la kijani.
 
Where is Dr. slaa???

Maana Chadema inabidi tuwaulize, Slaa kwa nini umemwacha Zito?? what happened??
Zitto is alone, seems frustrated, no where to runm, JF juzi alikuwa shujaa, leo tunamtupa,

Slaa wehere is your stand regarding Zito, mtei, Mbowe SAGA???

Wewe uko upande gani, na maoni yako ni nini kufuatana na Zito kuambiwa ajitoe??

PIGA UA CHADEMA IS SLAA and ZITTO!!!!!!!!! na kati yenu nyie angechukua form, mgepata viti vingi sana vya ubunge, Zito angekomba vijana na angeleta msisimko, au wewe pia unge penya na kuchota watu wa rika zote!

Tukiona watu kama wewe mko humo humo na mambo yako hivyo we must question where is Slaa and where is he standing???

Mkuu Waberoya,

You know very well kuwa Dr. Slaa ni msimamizi wa uchaguzi, hivyo yupoi fairly busy,

Pili, sidhani kwa busara zake atakuja kujibu mambo ya ndani ya chama chao hapa jamvini, tunamjua yule mzee hawezi kusema sema tu hapa mambo ya jikoni! Yule ana hekima,, ndivyo ninavyoamini!

wataka aje ajibu masuala aliyoleta Zitto hapa?
 
Ubarikiwe, we need people like you! the guy could be frustrated and his only hope was may be JF , JF is like this!!!!! jamani hata kwenye movie askari akipigwa vita mnamnyenyua!!!
Mkuu hii sio movie..kinachoendela ktk uchaguzi mkuu sio sinema kabisa ila uharibifu wa wazi wazi..kama nzige walioingia shambani..
Kinachozidi kuharibu ni nyie Wapambe wake. Imefikiam sasa hivi mnaubeba msalaba kwa niaba yake na wakati huo huo kundi jingine linajikita kumharibia jina zaidi. Kifupi mkuu wangu hamkitendei mazuri chama hata kidogo.. Kama kuna vita ya Uongozi ndani ya Chadmea iwe Ukabila au Udini au lolote lile. Sehemu ya kuweka wazi mambo haya ni ktk mkutano huu.
JF haiwezi kumsaidia mtu ila inaweza kumtangaza mtu au kumharibia mtu pasipo ukweli kuwa wazi. Kama wewe unamuunga mkono Zitto kwa yote yanayomtokea basi itakuwa bora uwakilishe hoja hii ktk kikao na ijadiliwe kwa Uwazi bila kuficha hisia zenu hata kaa zinamhusu mzee Mtei mwenyewe..I would love to know the truth maanake tunasikia tu Chadema ni chama cha Ukabila, Udini na kadhalika lakini hatuna uhakika.. Sasa fikiria wananchi tuje kichagua chama ambacho viongozi wake wanabeba Takaba hizo rohoni..
 
Where is Dr. slaa???

Maana Chadema inabidi tuwaulize, Slaa kwa nini umemwacha Zito?? what happened??
Zitto is alone, seems frustrated, no where to runm, JF juzi alikuwa shujaa, leo tunamtupa,

Slaa wehere is your stand regarding Zito, mtei, Mbowe SAGA???

Wewe uko upande gani, na maoni yako ni nini kufuatana na Zito kuambiwa ajitoe??

PIGA UA CHADEMA IS SLAA and ZITTO!!!!!!!!! na kati yenu nyie angechukua form, mgepata viti vingi sana vya ubunge, Zito angekomba vijana na angeleta msisimko, au wewe pia unge penya na kuchota watu wa rika zote!

Tukiona watu kama wewe mko humo humo na mambo yako hivyo we must question where is Slaa and where is he standing???

Mkuu mwache Dokta afanye kazi. Yupo bize na kazi za kuratibu na kusimamia mkutano mkuu. Kumbuka kuwa Katibu ndiyo mtendaji na Zitto (msaidizi wake) ndo kamtosa na anaendeleza mambo binafsi zaidi. Ilipaswa Zitto awe karibu na Dokta na kuhakikisha wanakamilisha masuala yote inavyopaswa. Kama kunakuwa na migongano si wanaimaliza kwa vikao?
 
Unajua vyama vya upinzani vimezoea cut and paste style katika propaganda. Ndio maana CCM wanawapiga mabao kilaini.

Hii style ya kujenga taswira ya usaliti dhidi ya washindani wa ndani imekuwa kama historia.

Kila anayeamua kusimama kidete dhidi ya uovu wa ndani basi huyo ni wa kupandikizwa ama amenunuliwa. Kama vile humo kwenye vyama vyao ni sawa na makazi ya malaika yasiyo na doa.

Hivi tumejiuliza ni kwanini kila anayetofautiana na wenzake katika vyama hivi kuanzia enzi za Marandu, Mrema, Kaborou, Tambwe, Chacha, Akwilombe na wengine wengi huwa wanakuwa na kosa moja kubwa.....wanatumiwa na CCM ama Mashushu...Its che cut and paste propaganda...

Wangekuwa madarakani wangeishia yaleyale ya Lukuvi kuwa hawa ni wahaini. Ni bora tukang'amua ukweli sasa kabla hatujafika kuaminiana dola.

Wakati umefika kuyasma haya wazi na kuwalazimisha watu wajifanyie sekf reflection kujua ni wapi nao wanakuwa sehemu ya tatizo badala ya kukimbilia kutafuta uchawi....hasa kwa kumsingizia kizee wa jirani.

Zitto yupo na atakuwepo humohumo, mtabanana naye hukohuko na kama mnadhani huo umafia wa kuchonga utawasaidia mjue wapo wengi wa aian yenu nyuma yake.....

omarilyas

Omar rafiki yangu ... naona umeamua kabisa kucopy na kupaste toka kwenye talking point za CCM kuwa upinzani sio wa kuaminiwa kupewa dola.

Shauri yenu, mimi nawaangalia tu nyie wanasiasa na hizi flip flop zenu mnazofanya hapa. Kitu hiki kilitakiwa kiwe kidogo sana ila naona mnazidi kukikuza.
 
Mkuu Waberoya, heshima mbele. Ukweli unaposemwa bila hekima hupoteza maana yake mara moja. Sio suala la kutoka kifua mbale na kujidai unasema 'ukweli' bila kupima kwanza athari zitakazotokana na wewe kusema huo ukweli, bila kutaja kuwa unaposema ukweli busara inadai pia uwe huna mawaa yanayokuzungua. Kwa hili, hata kama Zitto kasema 'ukweli', ametujuza kuwa katika ukweli huo alishiriki kumtenda Marehemu Chacha Wangwe!

Hilo la Mtei, wenye busara wamejua namna ya kulihandle, hawakuja 'kuropoka' hapa JF!

Walimtenda nini?au na wewe uko katika lile kundi la kuogopa wafu? yeye alisema walimtenda kisiasa kumzima! kuwa anachukua hela CCM!!!

Yeye naye wanamfanyia the same thing, huoni anajikwepesha , huwa hauangalii movies kuwa majambazi wanaweza kukosana na kuweka wazi kila kitu??

This is good! inabaki kuwa ni somo kwetu wote kuwa tuangalie vitu in 3D, mTEI KUSEMA KUWA ccm WALIPENYEZA FEDHA SI KWELI; NANI HUYO, KIJANA GANI ALIYEKAMATWA NA CCM? huoni wanakibariki kuwa ni chama cha kikabila zaidi na Zito ameliona hilo, amekasirika! alijua yuko nao pamoja kumbe wako ng'ambo mbili tofauti

In politics you better be open sometime, walichofanya CHADEMA HAIINGII AKILINI, kuwa ajitoe ,mgombea awe mmoja! wakati wanalia demokrasia!

Zito alisema kama kujitoa wajitoe wote! which was good

Msaidieni huyo, mpeni moyo, hawa wapiganaji wasipotiwa moyo, tutaandika post kama hizi humu maisha yetu yoooote bila kuona mabadiliko!

Mtei mbona karopoka kwenye vyombo vya habari , au wewe unaona JF iko TZ nzima?

Or who is perfect??
 
Where is Dr. slaa???

Maana Chadema inabidi tuwaulize, Slaa kwa nini umemwacha Zito?? what happened??
Zitto is alone, seems frustrated, no where to runm, JF juzi alikuwa shujaa, leo tunamtupa,

Slaa wehere is your stand regarding Zito, mtei, Mbowe SAGA???

Wewe uko upande gani, na maoni yako ni nini kufuatana na Zito kuambiwa ajitoe??

PIGA UA CHADEMA IS SLAA and ZITTO!!!!!!!!! na kati yenu nyie angechukua form, mgepata viti vingi sana vya ubunge, Zito angekomba vijana na angeleta msisimko, au wewe pia unge penya na kuchota watu wa rika zote!

Tukiona watu kama wewe mko humo humo na mambo yako hivyo we must question where is Slaa and where is he standing???

Zitto ndiye kamwacha Dr Slaa na sio the other way around. Zitto amekotiwa kwenye gazeti moja akisema kuwa uamuzi wa kugombea ulikuwa wake binafsi na hakuomba ushauri toka kwa mtu yoyote yule na hakutaka kujadili na yoyote kuhusu hili (ubinafsi?).

Sasa kama hayo ni kweli, ungependa Dr Slaa afanye nini?
 
Pamoja na kuwekewa mizengwe, Zitto anaonekana kukosa busara. Na hili si jambo jema kwa kiongozi wa kitaifa kama yeye.

Washauri wa Zitto mko wapi? Maana duh!
 
Mkuu mwache Dokta afanye kazi. Yupo bize na kazi za kuratibu na kusimamia mkutano mkuu. Kumbuka kuwa Katibu ndiyo mtendaji na Zitto (msaidizi wake) ndo kamtosa na anaendeleza mambo binafsi zaidi. Ilipaswa Zitto awe karibu na Dokta na kuhakikisha wanakamilisha masuala yote inavyopaswa. Kama kunakuwa na migongano si wanaimaliza kwa vikao?

Asante PS
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom