Mpaka kieleweke..Hivi ni kina nani waliosimamia uchaguzi? Hivi ni kina nani waliokuwa wanasambaza, kukusanya na kuhesabu kura? Hivi kati ya hao walikuwa na jukumu hilo ni wangapi walikuwa wakimuunga mkono Zitto na Kafulila na wangapi walikuwa wakiwapinga?
Unataka kusema kuwa kura zilizongezeka zilikuwa za Kafulila na sio za mgombea wenu? Na jee haiwezekani kuwa kura ziliongezwa kumuongezea nguvu Heche bila ya kung'amua kuwa mahesabu yatakataa na baadae ikaonekana bado mmeshindwa ndio mkaamua kutumia busara zisizo na hekima?
omarilyas
Omar
Mimi nilialikwa kwenye mkutano wa BAVICHA. Aliyesimamia mkutano alikuwa Mbunge Mwera, yeye aliyonyesha wazi kumchukia John Heche toka wakati anajieleza, labda sababu ya mivutano yao ya Tarime. Hawa wanajuana kwa kuwa waliogombea ubunge pamoja mwaka 2008.
Msimamizi msaidizi alikuwa Aidan Ndowa, huyu anatoka Kigoma anapotoka kafulila, msimamo wake hata wewe ulipokuwa Kigoma unaujua vizuri. Huyu ndiye aliyekuwa na makaratasi ya kura na kushikilia ya ziada.
Mwingine ni Ali Chitanda, huyu ni mpambe wa Zitto ambaye alimteua kuwa Afisa Vijana wakati Dr Slaa akiwa safarini na kumbadilisha idara aliyekuwa chini ya Mnyika. Maamuzi yale ya kumuondoa Mnyika kurugenzi ya vijana yamefanya mpaka leo CHADEMA haina mkurugenzi wa vijana. Pengine hii ndio imefanya hata Mnyika hakugombea Uenyekiti wa vijana, pengine alijua mapema kuwa Zitto hamtaki kama ambavyo amedhihirisha kwa maneno yake hapa JF. Chitanda ndiye aliyegawa karatasi kwa wajumbe
Wa mwisho ni Danda Juju Martin, huyu ni afisa aliyetumwa na Zitto kufanya kampeni Nyanda za juu. Unakumbuka huyu iliandikwa kuwa alipigwa chombe kwa sababu ya kusambaza maneno ya kuwachafua Mbowe na Mnyika. Huyu alisambaza na kukusanya karatasi za kura, huyu alituhumiwa kuwa ndiye aliyeandika kura za nyongeza.
Kura zilizozidi haziwezi kuhusishwa na John Heche kwa sababu yeye alilalamika kabla kuwa kuna taarifa kuwa kuna kura za nyongeza. Akapuuzwa. Akalalamika pia kuwa mbele ya meza kura zinaongezwa. Hakusikilizwa.
Gazeti la Leo limemnukuu Mwenyekiti wa Vijana wa Singida akieleza kura zilivyoibiwa, na jinsi Zitto alivyofurahia hali hiyo na kuondoka akisema kuwa 'leo vijana lazima watwangane'!
Nenda kamuulize Zitto, je anamtetea Kafulila kwa sababu anatoka naye wilaya moja au kwa sababu ndiye aliyekuwa akimtuma Habari Corporation kwenye kufanya majadiliano na kina Muhingo kuhusu namna ya kutetea mitambo ya Dowans dhidi ya hoja za CHADEMA na kina Mwakyembe?
serayamajimbo