Zakumi,
Mkuu, kwangu Mimi NDIVYO TULIVYO ina maana nyingi zaidi ya ubunifu maanake unaweza kuwa mbunifu lakini ukashindwa kuendeleza ubunifu huo..nitawazungusha kidogo unajua tena Mkandara kwa kuandika gazeti la mipasho!
Mathlan nchi kama Iraq ni wabunifu wa sayansi na technologia nyingi ambazo wao walishindwa kuzifanyia kazi kitaifa lakini sifa zote zinakwenda ktk nchi za magharibi na magwiji wa kuendeleza ubunifu..Canada walibuni mchezo wa basketball lakini waka invest more katika Hockey kwa sababu ndio mchezo wenye kuingiza revenue zaidi kulingana na soko la mazingira yao. Marekani wakatumia ubnifu huo wa canada kwao kutokana na sababu kama za Canada wakati sisi tunachukua mpira wa soccer kama ni ushabiki na mapenzi ya Kiujamaa..kudumisha udugu, jamii na Upendo.
Kwa hiyo ubunifu wowote hufuatana na investment inayotazama soko na mazingira ya sehemu sii maswala ya kufikiria kwamba Muarobaini unatibu Maleria kisha ukashindwa kuufanyia kazi ukaagiza madawa toka China yanayotokana na Muarobaini..
Hivyo, tofauti kubwa inayojitokeza wazi kati yetu na nchi zilizoendelea ni kwamba sisi tunajaribu sana ku apply makubwa yanayowashinda Ulaya ili twenda na wakati hali yale madogo yenye soko na yanayowaathiri zaidi wananchi tunayaacha wazungu wafanye investment kwa ajili yetu..
Tatizo kubwa la Ujamaa ni kutotazama nje ya box kiuchumi, kila kitu ni mfano wa imani ya mchezo wa mpira wa miguu (soccer) nchini yaani tunafanya mipango ya mchezo kutokana na mapenzi ya mchezo kuunda ushabiki unaolenga ujamaa wa kuunda umoja, undugu na kadhalika. Ukiwa Simba basi wewe Yanga hata wafanye nini huna thamani nao hata kama wana generate billions of revunue..Tupo radhi kushabikia Arsenal au ManU bila sababu zaidi ya Mapenzi ya mchezo lakini wenzetu utakuta ushabiki wao unatokana na yale Arsenal inayoyafanya katika jamii yao...Mpira kwetu ni kujenga urafiki, kudumisha upendo na umoja swala la fedha halipo ktk mikakati yetu...Ni mfumo uliotufanya tuwapende viongozi wetu hata kama they have done nothing ktk jamii yetu kutuendeleza isipokuwa kujenga upendo, Undugu na amani..huo ndio Ujamaa. Sasa turudi kwenye - Ndivyo Tulivyo..
Hii haifanani hata kidogo na Ujamaa. Imesimama peke yake, sii Kenya, South Afrika wala Tanzania tuna tofautiana sana..Priority zetu sisi Ndivyo Tulivyo...Kwa mfano kuna nguvu kubwa ya kuzuia Ukimwi, mabillioni ya fedha yanawekezwa ktk kupambana na Ukimwi lakini in reality wananchi wengi wa Tanzania wanakufa kwa Maleria..Sasa tujiulize inakuwaje wananchi wengi wanakufa kwa Maleria lakini nguvu kubwa inawekwa kwa HIV ambayo kwanza tunategemea misaada toka nje hata hizo Condom tunashindwa kutengeneza lakini tunaweza kutengeneza mifuko ya kubebea nyanya ambayo hugawiwa bure kwa kila mnunuzi..
Hakuna mikakati tunachokifanya zaidi ya ile ya kujipanga kanisani kusubiri misaada na mara zote tunatazama maradhi ya Kiuchumi yanayozikabiri nchi za Ulaya kutibu maradhi....Nikiwa na maana maradhi kama HIV hata kama tusipofanya mikakati ya nguvu, elimu, fedha na dawa zake zitaletwa tu kinachotakiwa ni sheria (policy) kuruhusu dawa hizo zitumike kwani soko lake lipo na elimu ya maradhi haya tunaitegemea kutoka nje..
Nguvu yetu inatakiwa kuelekezwa zaidi kwa Maleria kiuchumi, Tiba, kinga na hata kuuondoa kabisa ni kazi ndogo sana ya kibamaabara ambayo ingeweza ku generate revenue kubwa kwetu kwa sababu Asia na kusini kote kwa sahara tunategemea madawa toka nje wakati raw material inatoka kwetu... Maleria ni ugonjwa unaotibika, ugonjwa unaoweza kukomeshwa kirahisi zaidi, lakini ktk nchi za kusini mwa jangwa la Afrika watu wanakufa wengi kuliko hesabu ya vita ya Iraq na Afghanstan combined!..
Now, nikirudi ktk Ujamaa kitu pekee ambacho nilikipenda kuhusiana na Ujamaa ni ktk kuelewa mazingira unayoishi na kutafuta tiba ya matatizo hayo kulingana na hali iliyopo.. Miaka ya Nyerrere, Maleria ulikuwa ugonjwa mdogo sana, Kipundupindu kilipokuja (1975-76)tulikimaliza within 5yrs kikawa history.. Ukoma na maradhi mengine yote ya tropical yalikuwa na chanjo za kinga na dawa kila zahanati utakayokwenda tena bure kwa kila mwananchi..Hivyo ukiwa na jamii yenye afya ni rahisi kupanga mikakati ya uzalishaji..
Kwa ujumla wa yote Ndivyo Tulivyo ni pale tuliposhindwa kuwa wabunifu au kutumia Ubunifu ktk investments zetu.. Tumeshindwa kufikiria nje ya box kwamba maradhi kama Maleria yanahityaji nguvu zetu kupata dawa za Kinga na ponya kwa sababu soko lipo ndani na nje.Kuna nchi jirani na Asia ambazo zina maradhi kama yetu na wanahitaji dawa hizo hivyo nguvu kubwa iwekwe ktk kufikiria uzalishaji wa dawa za kinga na ponya ya maradhi hayo badala yake tunazidi kusisitiza uagizaji wa dawa hizi toka nje bila kuweka regulations ambazo zitawakinga wananchi na taifa zima kuingia hasara ya dawa feki au kutazama uwezekano wa uzalishaji wa dawa hizo nchini..
Na ukitazama Elimu, mkuu wangu mambo mengi tunayosoma Tanzania ni kuhusu mazingira ya Ulaya. Kuna masomo mengi tunayafundisha Afrika hayafundishwi Ulaya kwa kutazama Afrika wala Asia...Tena unaweza kuta graduates wao hawajui lolote kuhusiana na Wayunani isipokuwa wabunifu wa yale wanayo invest kwao..Sisi tunasoma kila kitu cha wageni hata ktk maswala ambayo hayahusiani kabisa na mazingira yetu wala hatuna interest ya ku invest katika maswala hayo..
Kwa hiyo ktk kila mfumo wa Kisiasa kulikuwepo na mazuri yake na muhimu zaidi tunapozungumzia Ujamaa nadhani tutazame zaidi pande zote mbili ktk mazuri na mapungufu yake.. Binafsi naamini kabisa kwamba Ujamaa uligota zaidi ktk huduma bila kufahamu kwamba biashara ni invisible hand inarahisisha huduma zote kutokna ana ubunifu unaohamasisha investment ktk soko na mazingira itokane na elimu au mtaji..
Hofu kubwa ya Unyonyaji ktk Ujamaa ndicho kiilikuwa kilema cha mapenzi ya Ubepari (biashara) mfano wa Mwanamke anayeogopa kuingia ktk relationship kwa sababu anaogopa bwana atambwaga mara tu akisha fungua miguu..Mara zote hofu kama hii mwanamke huyo hupata taabu kufanikiwa lakini hofu hiyo haimfanyi kutokuwa mwanamke mzuri mwenye tabia nzuri anayefaa kuolewa!..
Imetosha...