Kuelekea Ujamaa Mamboleo - Toward Neo-Socialism

Kuelekea Ujamaa Mamboleo - Toward Neo-Socialism

Zakumi,
Mkuu, kwangu Mimi NDIVYO TULIVYO ina maana nyingi zaidi ya ubunifu maanake unaweza kuwa mbunifu lakini ukashindwa kuendeleza ubunifu huo..nitawazungusha kidogo unajua tena Mkandara kwa kuandika gazeti la mipasho!

Mathlan nchi kama Iraq ni wabunifu wa sayansi na technologia nyingi ambazo wao walishindwa kuzifanyia kazi kitaifa lakini sifa zote zinakwenda ktk nchi za magharibi na magwiji wa kuendeleza ubunifu..Canada walibuni mchezo wa basketball lakini waka invest more katika Hockey kwa sababu ndio mchezo wenye kuingiza revenue zaidi kulingana na soko la mazingira yao. Marekani wakatumia ubnifu huo wa canada kwao kutokana na sababu kama za Canada wakati sisi tunachukua mpira wa soccer kama ni ushabiki na mapenzi ya Kiujamaa..kudumisha udugu, jamii na Upendo.

Kwa hiyo ubunifu wowote hufuatana na investment inayotazama soko na mazingira ya sehemu sii maswala ya kufikiria kwamba Muarobaini unatibu Maleria kisha ukashindwa kuufanyia kazi ukaagiza madawa toka China yanayotokana na Muarobaini..

Hivyo, tofauti kubwa inayojitokeza wazi kati yetu na nchi zilizoendelea ni kwamba sisi tunajaribu sana ku apply makubwa yanayowashinda Ulaya ili twenda na wakati hali yale madogo yenye soko na yanayowaathiri zaidi wananchi tunayaacha wazungu wafanye investment kwa ajili yetu..
Tatizo kubwa la Ujamaa ni kutotazama nje ya box kiuchumi, kila kitu ni mfano wa imani ya mchezo wa mpira wa miguu (soccer) nchini yaani tunafanya mipango ya mchezo kutokana na mapenzi ya mchezo kuunda ushabiki unaolenga ujamaa wa kuunda umoja, undugu na kadhalika. Ukiwa Simba basi wewe Yanga hata wafanye nini huna thamani nao hata kama wana generate billions of revunue..Tupo radhi kushabikia Arsenal au ManU bila sababu zaidi ya Mapenzi ya mchezo lakini wenzetu utakuta ushabiki wao unatokana na yale Arsenal inayoyafanya katika jamii yao...Mpira kwetu ni kujenga urafiki, kudumisha upendo na umoja swala la fedha halipo ktk mikakati yetu...Ni mfumo uliotufanya tuwapende viongozi wetu hata kama they have done nothing ktk jamii yetu kutuendeleza isipokuwa kujenga upendo, Undugu na amani..huo ndio Ujamaa. Sasa turudi kwenye - Ndivyo Tulivyo..

Hii haifanani hata kidogo na Ujamaa. Imesimama peke yake, sii Kenya, South Afrika wala Tanzania tuna tofautiana sana..Priority zetu sisi Ndivyo Tulivyo...Kwa mfano kuna nguvu kubwa ya kuzuia Ukimwi, mabillioni ya fedha yanawekezwa ktk kupambana na Ukimwi lakini in reality wananchi wengi wa Tanzania wanakufa kwa Maleria..Sasa tujiulize inakuwaje wananchi wengi wanakufa kwa Maleria lakini nguvu kubwa inawekwa kwa HIV ambayo kwanza tunategemea misaada toka nje hata hizo Condom tunashindwa kutengeneza lakini tunaweza kutengeneza mifuko ya kubebea nyanya ambayo hugawiwa bure kwa kila mnunuzi..

Hakuna mikakati tunachokifanya zaidi ya ile ya kujipanga kanisani kusubiri misaada na mara zote tunatazama maradhi ya Kiuchumi yanayozikabiri nchi za Ulaya kutibu maradhi....Nikiwa na maana maradhi kama HIV hata kama tusipofanya mikakati ya nguvu, elimu, fedha na dawa zake zitaletwa tu kinachotakiwa ni sheria (policy) kuruhusu dawa hizo zitumike kwani soko lake lipo na elimu ya maradhi haya tunaitegemea kutoka nje..

Nguvu yetu inatakiwa kuelekezwa zaidi kwa Maleria kiuchumi, Tiba, kinga na hata kuuondoa kabisa ni kazi ndogo sana ya kibamaabara ambayo ingeweza ku generate revenue kubwa kwetu kwa sababu Asia na kusini kote kwa sahara tunategemea madawa toka nje wakati raw material inatoka kwetu... Maleria ni ugonjwa unaotibika, ugonjwa unaoweza kukomeshwa kirahisi zaidi, lakini ktk nchi za kusini mwa jangwa la Afrika watu wanakufa wengi kuliko hesabu ya vita ya Iraq na Afghanstan combined!..

Now, nikirudi ktk Ujamaa kitu pekee ambacho nilikipenda kuhusiana na Ujamaa ni ktk kuelewa mazingira unayoishi na kutafuta tiba ya matatizo hayo kulingana na hali iliyopo.. Miaka ya Nyerrere, Maleria ulikuwa ugonjwa mdogo sana, Kipundupindu kilipokuja (1975-76)tulikimaliza within 5yrs kikawa history.. Ukoma na maradhi mengine yote ya tropical yalikuwa na chanjo za kinga na dawa kila zahanati utakayokwenda tena bure kwa kila mwananchi..Hivyo ukiwa na jamii yenye afya ni rahisi kupanga mikakati ya uzalishaji..
Kwa ujumla wa yote Ndivyo Tulivyo ni pale tuliposhindwa kuwa wabunifu au kutumia Ubunifu ktk investments zetu.. Tumeshindwa kufikiria nje ya box kwamba maradhi kama Maleria yanahityaji nguvu zetu kupata dawa za Kinga na ponya kwa sababu soko lipo ndani na nje.Kuna nchi jirani na Asia ambazo zina maradhi kama yetu na wanahitaji dawa hizo hivyo nguvu kubwa iwekwe ktk kufikiria uzalishaji wa dawa za kinga na ponya ya maradhi hayo badala yake tunazidi kusisitiza uagizaji wa dawa hizi toka nje bila kuweka regulations ambazo zitawakinga wananchi na taifa zima kuingia hasara ya dawa feki au kutazama uwezekano wa uzalishaji wa dawa hizo nchini..

Na ukitazama Elimu, mkuu wangu mambo mengi tunayosoma Tanzania ni kuhusu mazingira ya Ulaya. Kuna masomo mengi tunayafundisha Afrika hayafundishwi Ulaya kwa kutazama Afrika wala Asia...Tena unaweza kuta graduates wao hawajui lolote kuhusiana na Wayunani isipokuwa wabunifu wa yale wanayo invest kwao..Sisi tunasoma kila kitu cha wageni hata ktk maswala ambayo hayahusiani kabisa na mazingira yetu wala hatuna interest ya ku invest katika maswala hayo..

Kwa hiyo ktk kila mfumo wa Kisiasa kulikuwepo na mazuri yake na muhimu zaidi tunapozungumzia Ujamaa nadhani tutazame zaidi pande zote mbili ktk mazuri na mapungufu yake.. Binafsi naamini kabisa kwamba Ujamaa uligota zaidi ktk huduma bila kufahamu kwamba biashara ni invisible hand inarahisisha huduma zote kutokna ana ubunifu unaohamasisha investment ktk soko na mazingira itokane na elimu au mtaji..

Hofu kubwa ya Unyonyaji ktk Ujamaa ndicho kiilikuwa kilema cha mapenzi ya Ubepari (biashara) mfano wa Mwanamke anayeogopa kuingia ktk relationship kwa sababu anaogopa bwana atambwaga mara yetu akisha fungua miguu..Mara zote hofu kama hii mwanamke huyo hupata taabu kufanikiwa lakini hofu hiyo haimfanyi kutokuwa mwanamke mzuri mwenye tabia nzuri anayefaa kuolewa!..

Imetosha...

Mwanawasu
Acha kabisa hiyo kuinvest ktk madawa ya malaria ni mpaka tungekuwa si ndivyo tulivyo.
Unajuwa mtu anapogunduwa dawa ana laisensi ya miaka 20 ambayo mtu mwingine hawezi kuiproduce baada ya miaka 20 ndio unaruhusiwa kuiproduce.
Sasa mkuu kwa vile sisi ndivyo tulivyo ni ngumu tena sana kwa mtu jamii yetu kukaa chini kubuni dawa yake kuanzia A hadi Z.

unajuwa tatizo la shule yetu inatufundisha kufanya application ya wale wamekwisha vumbuwa.Kweli ni ngumu.
 
MkamaP,
Mkuu nipo nawe mia kwa mia, kile nilichoandika kitabu kizimaaa, wewe umekieleza kwa ufupi sana.. kusema kweli ningekuwa na kipaji kama chako ningeshukuru sana lakini ndio siwezi tena! - Ndivyo Tulivyo inakuja na mengi wee... haaa haaa haa!
 
Mwanawasu
Acha kabisa hiyo kuinvest ktk madawa ya malaria ni mpaka tungekuwa si ndivyo tulivyo.
Unajuwa mtu anapogunduwa dawa ana laisensi ya miaka 20 ambayo mtu mwingine hawezi kuiproduce baada ya miaka 20 ndio unaruhusiwa kuiproduce.
Sasa mkuu kwa vile sisi ndivyo tulivyo ni ngumu tena sana kwa mtu jamii yetu kukaa chini kubuni dawa yake kuanzia A hadi Z.

unajuwa tatizo la shule yetu inatufundisha kufanya application ya wale wamekwisha vumbuwa.Kweli ni ngumu.

Mkamap:

Kwa kuongezea tu. Moja ya njia ya kuzuia malaria ni kuwa na mifereji ya maji machafu. Mifereji kwenye miji hipo lakini hakuna mtu anayefanyia usafi.

Kuna kitabu ninacho hapa kimeandikwa karne ya 13. Kinaelezea sababu ya kujenga milimani kwa kipindi hicho na kilichotangulia.

Wazungu, walijenga milimani kwa sababu, mabondeni kulikuwa na maji. Na sehemu yenye maji yaliotuama ni chanzo cha magonjwa mengi.

Angalia simple ubunifu hapo. Mtu anajenga mlimani kukimbia magonjwa na baadaye anatafuta mbinu ya kuvuta maji ya kutumia mlimani.

Ukija Tanzania, watu wanajenga mabondeni bila kufikiri athari zake. Mabonde yakiopo Keko, Msimbazi, Kinondoni hayafai kuishi watu bila kufanyiwa matengenezo makubwa.
 
Nani anatawala hizo neighborhoods za weusi? Si weusi wenyewe au?

Mkuu fuatilia zaidi kuhusu system ya utawala hapa USA,Sasa ngoja nikupe mfano,kama kuna majimbo huko bongo ambayo serikali inaweza kuwaminyia kwasababu wameuchagua upinzani,nani atakuwa wa kulaumiwa hapo? Nimekutolea mfano wa bongo lakini hata hapa ipo mingi tu nashangazwa sana hujui,kinachotofautiana utakuta tu kuwa bongo ni more about vyama na huku races,seems to me like you're well priviledge na kwahiyo mambo mengine yanakupitia ama hauyapi uzito unaostahuli. Nitakuwekea links hapa za mifano ambayo jamii za minorities zimeachwa nyuma ama kuwa ignored nk. Safari inakuwa ndefu zaidi kwasababu miafrika ambayo iko ilivyo haiwaelewi mifrika myenzao.Lol!
 
Sasa hii post yako mbona inadhilisha kuwa ndivyo tulivyo. Kwanza kabisa ukitumia logic tu ya kawaida kucolonaiziwa ni moja ya sababu kuwa ndivyo tulivyo. Unaona kabisa Wazungu kumi waliweza kushinda vita dhidi ya mababu zetu, wewe unafikiri kwanini walishinda vita kiurahisi??

Sijaelewa mfano wa mashamba unataka kusema nini?

Kwani unaposema "Miafrika ndivyo tulivyo" unamaanisha nini? kwamba kwasababu tulipigwa na wazungu kumi ama kwasababu tulikubali kutawaliwa ama kupelekwa utumwani?

Mkuu kumbuka kuwa kuna waafrika amabo walipambana sawia dhidi ya ukoloni na utumwa, na kuwachanganya na waafrika ma cowards ambao sio tu walikubali kutuuza kwa mkoloni,bali bado wanaendelea kuuza rasilimali, haifai. Miafrika ilivyo ni hiyo inayouza nchi na kujdai eti ndo ilipigania uhuru,na miafrika inayokubaliana nayo ndiyo hiyo ilivyo. Mimi nimeshagoma na nimesema mimi simo humoo!

Kuhusu mashamba ni kwamba wakulima hao hawana hata elimu ila wananufaika na kilimo na rsilimali,hakuna jamii inayosemekana eti wwananchi wote wakiwa wasomi basi ndo itaendelea,unajuwa kuna wasomi wangapi Nigeria? Miafrika miviongozi yetu mifisadi na yote inayowapigia kura either kwa dini,chama ama kabila ndivyo ilivyo.

Na pia kama unashangazwa na kushindwa kwa waafrika na hao wazungu wachache,mbona hujashangazwa na Israel kuwapiga waarabu wote na kuchukua ushindi ndani ya siku sita? Je miarabu nayo ndo ilivyo?
 
Companero:

Ujamaa na historia ya Tanzania siku zote zime-play victim cards. Kwanza watanzania tuna tatizo la kuwa tulivyo. Halafu tunaongeza matatizo kwa ku-play victim cards.

Hivyo kuweka Truth nje kuhusu chanjo matatizo yetu inaweza kutusaidia. Kuliko kung'ang'ania miundo isiyo yetu kama Ujamaa.

1. Mkuu mbona unajikanganya, huoni kuwa parandesi yako ya kwanza hapo juu inaonesha kuwa hatuongezi tatizo la ku-play victim cards maana tayari hivyo ndivyo tulivyo i.e. ku-play victim?

2. Kama Ujamaa sio muundo ulio wetu, muundo wetu ni upi basi?
 
MkamaP,
unajuwa tatizo la shule yetu inatufundisha kufanya application ya wale wamekwisha vumbuwa.Kweli ni ngumu.
Kwa kuongezea tu kuna wakati nilikuwa azumngumzia sana hii habari ya kujali Mazingira ktk kutafuta ufumbuzi wa Umaskini wetu..Ni somo kubwa na refu sana lakini linahitaji ufahamu wa misingi midogo sana...
Mimi kama Mjamaa ambaye kwa kiasi kikubwa nakubaliana na Companero kifikra lakini nashindwa kufikia maamuzi kwa sababu ya fikra za Nyani Ngabu kuhusiana na sisi NDIVYO TULIVYO..
Sioni sababu kabisa ya wagonjwa wetu kwenda kutibiwa India ktk maradhi ambayo yangeweza kutibika hapa nyumbani Tanzania tena yaweza kuwa bei rahisi kwa sababu ni maradhi ya tropical.. sasa unakuta Muhimbili wanahitimu wanafunzi kwa maelfu kila mwaka, Madaktari tunao mia kidogo lakini wote wamesomea maradhi ya Ulaya zaidi..
Mwaka 1989, nikiwa mitaa hii , kuna rafiki yangu alitoka Bongo mzimaaa alipofika hapa Malaria iliibika akaenda Hospital.. mshikaji karibu afe, alifanyiwa vipimo namadaktari wa kila ujuzi kwani virusi walivyoviona hawakuwahi kuviona na ikawa big deal kichizi..Katika ushauri ndipo walipomrusha daktari mwingine toka mji meingine ambaye alikuwa na ujuzi na maradhi ya tropical akaja na kugundua kuwa ni Maleria..ndipo akafanyiwa tiba.. yaani madaktari wote na elimu yao walikuwa hawajasomea kabisa Maleria na viruzi vyake...Bila huyo daktari jamaa alikuwa anaondoka maanake kila siku walikuwa wakimjaza maji ya chupa tu bila dawa ati wanafanya uchunguzi..
Sasa tazama hii ulaya wao wanasomea maradhi yao sisi ndio kwanza maradhi yetu tunapeleka wagonjwa nje.. Madaktari wetu wengi wamekaa hawana kazi wengine hufunga vidonda, wanafungua drugmart kwa sababu hawana kazi Muhimbili hutibu mgonjwa mmoja kwa mwezi ktk fani yake..
Tanzania ambayo tunategemea kilimo tunajikita sasa hivi ktk mambo mengine wakati tunafahamu fika kwamba madini yanatuingizia only 2 percent ya mfuko wa Taifa, ukiuliza kwa nini jitihada zisiwekwe ktk kilimo wanakupa mfano wa Marekani au nchi tajiri... jamani Amerika ina wakulima asilimia 10 na nchi inategemea kilimo kwa silimi asiyodzidi 10 vilee vile leo wewe uliyetegemea kilimo kwa asilimia 80 unashindwa kuwatumia wananchi asilimia 80 kujihusisha na kilimo kwa sababu Marekani wanatumia asilimia 10...
Kinachotakiwa au kutazamwa ni kipi hapa?.. ardhi unayo hekta 2,000 za ukulima wa zabibu uwe na watu 10 au familia 200 kinachotakiwa ni uzalishaji bora wa hizo hekari 2,000. Pato litokanalo na uzalishaji wa hekari 2,000 ndio mwanzo wa kuziwezesha zile familia 200 ambazo ni part of 80% ya population..
Ukienda Kenya utaona mashamba yasiyokuwa na mwisho ya miwa lakini kati ya mashamba hayo wamiliki wake ni familia nyingi tu... muhimu uzalishaji unalipa nguvu na uwekezaji ktk kilimo cha miwa. sisi ndio kwanza tunatafuta wazungu, waarabu waje kuwekeza ktk kilimo cha Ulaya wakati hatuna viwanda, biashara na services ambazo ni mwajiri mkubwa wa nchi za Ulaya..Huyo mwarabu akisha lima Kyela Mpunga sijui wakulima wa sehemu hiyo utawapa ajira gani...
Kifupi kama nilivyosema ktk moja ya mada za hapa. Sisi tunaendesha uchumi wetu ktk barabara zetu za one lane traffic tukienda kwa wazungu kwa speed ya 120 kuwafikia wakati wenzetu wamejenga Highways na flyover zinazoweza kuhimili traffic zao na mwendo wa kasi ya 120km/hr..Matokeo yake ndio hayo ya kushikana uchawi kwa ajali za kiuchumi kama kina Mwakyembe, Mbatia, Wangwe..
 
Zakumi,
Mkuu, miji gani Ulaya iko juu milimani hata kama ipo kando ya ziwa, bahari au mito..au unazungumzia nyumba za wazungu walizojenga hapa Afrika!.
 
Mkandara sijui ni wapi una refer kuhusu madaktari hao kutojua ugonjwa wa malaria,lakini FYI Malaria ilikuwa hapa USA ila waliivalia njuga na ikamalizwa,na si kwamba hawaijui,ila wameshaiovercome.Kuna magonjwa mengi tu ambayo ni kweli kama ikitokea pandemic basi haitajalisha hata hapa USA watakufa wengi tu,chukulia mfano wa polio ambayo wameshaisahau.
Kwa kifupi ni kwamba malaria iliwauwa sana hapa USA kabla hawajaitokomezea mbali,hata sisi tunaweza,ni kupata uongozi mpya tu wenye madhumini ya kweli na Taifa na pia nakubaliana na uchambuzi wako kwa kiasi kikubwa only hapo kwenye kuhusu malaria.
 
Mwanawasu
Acha kabisa hiyo kuinvest ktk madawa ya malaria ni mpaka tungekuwa si ndivyo tulivyo.
Unajuwa mtu anapogunduwa dawa ana laisensi ya miaka 20 ambayo mtu mwingine hawezi kuiproduce baada ya miaka 20 ndio unaruhusiwa kuiproduce.
Sasa mkuu kwa vile sisi ndivyo tulivyo ni ngumu tena sana kwa mtu jamii yetu kukaa chini kubuni dawa yake kuanzia A hadi Z.

unajuwa tatizo la shule yetu inatufundisha kufanya application ya wale wamekwisha vumbuwa.Kweli ni ngumu.

Naam ndivyo tulivyo - Wajamaa hata katika uvumbuzi. Jamii zetu zinavumbua na kutumia uvumbuzi wao kwa Mjamaa. Ndio maana mwarobaini, dawa ya malaria, haukuwa unahodhiwa. Hebu cheki nukuu hii:

"Throughout Africa, people have also developed knowledge around ... bio-resources. The knowledge has been widely shared within communities and freely transferred from one generation to the other. In this way innovation and what was produced was never meant to benefit individuals and were not claimed to be individual properties of the innovators. For example, communities of hunters and gatherers used and continue to use, in some ways, thousands of plants and animals for food, medicine, and shelter...These resources and knowledge have remained, over the years, community property. They were and are produced, owned and controlled by communities themselves. These resources and the knowledge that people have been able to develop and accumulate over time, and passed through one generation to the other, are at the verge of being dispossed of the rightful owners...mainly through commoditization and privatization...through patenting (the modern form of enclosure) ...this takes the form of intellectual property rights..." - The Mute Plunder: Bio-resources and Dispossession in Tanzania, pp. 1-4
 
JMushi1,
Mkuu nazungumzia mwaka 1989..wakati huo kulikuwa na specialist wachache wa maradhi ya tropical. Na unaposema US umenigusa haswa kwa sababu ilitokea New York kwa mshikaji wangu ambaye alikuwa DJ Bongo, mzee FMES anamjua vizuri..
Maswala ya kuweza kutibu yamekuja baada ya immigrants kuanza kuingia na magonjwa ya ajabu ajabu kwao...ndio maana siku hizi wana vitengo vinavyojumuisha madaktari kwa ajili ya pendamic...
Ukisema leo kuhusu Malaria, oooh, kila mtu anajua lakini sio miaka kabla ya 1990s mkuu..
 
Companero,
Mkuu lakini uloandika sii ndio niliyosema hapo juu?..yaani sisi tunavumbua vitu lakini tunashindwa kuweka nguvu zetu kuinvest hata kama vina faida kubwa kwetu.
Nikatoa mfano wa canada na basketball. wao walivumbua lakini hawakuwekesha ktk basketball kwa sababu haikuwa na mazingira wala soko kwao, Marekani wakachukua uvumbuzi huo na kwa sababu ya mazingira na soko wakaufanyia kazi leo hii nchi hizo zinafaidika na revenue zinazotokana na michezo hiyo...

Sisi Watanzania, tunavumbua muarobaini ambao tuna shida kubwa ya Maleria tunashindwa kufanya investment badala yake tunaagiza madawa Ulaya yaliyotengenezwa kwa Muarobaini ambao unastawi Bongo..
Hivyo tumevumbua kuwa Muarobaini ni dawa na uzalishaji wake upo Tanzania..tumeshindwa nini kuinvest ktk kutengeneza dawa ya maradhi ambayo ni number one cause of death nchini?..nini sababu ya kuvumbua haswa?.. ndio najiuliza hata sababu ya shule zetu.. hivi tunasoma ili kufanikishe kipi haswa?
Sasa hiii mkuu wangu kama Sivyo Tulivyo ni kitu gani?.. ikiwa elimu ya kuvumbua tunayo, uzalishaji tunao lakini inapifikia kuweka mezani as a finished product stage inayolipa nguvu na jitihada zote zilizotangulia kiuchumi, tunamwachia mzungu au Mchina..
 
Mkandara, try this info,kuna links pia with even more information....So unaposema walikuwa hawajui malaria before 1990's nashangazwa kidogo na kwamba info hizo umepata wapi...

Malaria in the USA:
In the first quarter of this century, malaria was rampant in U.S.A. with nearly 6 million cases annually. Due to determined antimalaria measures and permanent vector control measures like screening of all constructions, malaria has been controlled effectively. In fact, the Centres for Disease Control (CDC) in U.S.A. was founded as the Office of Malaria Control! Since 1940 57 localized outbreaks have been reported. In1970, 4247 cases were reported and more than 4000 of these were US military personnel returning from Vietnam.
YearCases
Graph showing incidence of malaria per 100000 population
19901292
usa.jpg
19911278199210871993141119941229199514191996180019972001
(Source: CDC MMWR Summary of Notifiable Diseases, United States, 1997, November 20, 1998/ 46(54);1-87)

Sources:
  1. www.cdc.gov/travel/diseases/maps/malaria_map_afr_asia_2003.htm
  2. www.cdc.gov/travel/destinat.htm
  3. www.who.int/ith/countrylist01.html
 
Zakumi,
Mkuu, miji gani Ulaya iko juu milimani hata kama ipo kando ya ziwa, bahari au mito..au unazungumzia nyumba za wazungu walizojenga hapa Afrika!.

Hizi umeshatembelea Castles zilizopo Europe na sehemu zilipojengwa? Na tukirudi Afrika kwanini walijenga milimani kwanza?

Anyway, point niliyotoa hakuwa na tafsiri unayotaka kui-spin hapa. Point yangu ni kuwa Malaria na magonjwa mengine yana kinga nyingi kabla ya kutumia madawa.

Na matumizi ya kinga yanaonyesha ubunifu wako. Na Tanzania inaweza kupunguza idadi ya magonjwa yote kwa kutumia kinga za ubunifu tu bila kutegemea sana madawa. Na huu ubunifu ndio unaotutenganisha sisi na wenzetu.
 
A specter is haunting Tanzania. The Specter of African Socialism. Workers and Peasants of Tanzania Unite.

Mzuka unaindama Tanzania. Ni Mzuka wa Usoshalisti wa Kiafrika. Wafanyakazi na Wakulima wa Tanzania Unganeni.

It is now a fact of life that Neoliberal Capitalism has committed suicide. JK's Stimulus Package attest to this. There is an ideological vacuum.

Ni jambo la uhakika katika maisha yetu kuwa Ubebari wa Kinioliberali umejiuwa wenyewe. Mpango wa JK wa Kuzindua Uchumi unadhihirisha hilo. Sasa kuna Ombwe la Kiitikadi.

But Nature abhors Vacuum. So, what will fill this Vacuum? In fact what is filling this Vacuum?

Lakini Asili huchukia Ombwe. Hivyo, ni nini kitaliziba Ombwe hili? Kiusahihi zaidi, ni nini kinaliziba Ombwe hili?

It is Neo-Socialism!

Ni Ujamaa Mamboleo!

Asante kwa somo - msamiati wa kiswahili -Ombwe, Mzuka umetulia!
 
Companero,
Mkuu lakini uloandika sii ndio niliyosema hapo juu?..yaani sisi tunavumbua vitu lakini tunashindwa kuweka nguvu zetu kuinvest hata kama vina faida kubwa kwetu.
Nikatoa mfano wa canada na basketball. wao walivumbua lakini hawakuwekesha ktk basketball kwa sababu haikuwa na mazingira wala soko kwao, Marekani wakachukua uvumbuzi huo na kwa sababu ya mazingira na soko wakaufanyia kazi leo hii nchi hizo zinafaidika na revenue zinazotokana na michezo hiyo...

Sisi Watanzania, tunavumbua muarobaini ambao tuna shida kubwa ya Maleria tunashindwa kufanya investment badala yake tunaagiza madawa Ulaya yaliyotengenezwa kwa Muarobaini ambao unastawi Bongo..
Hivyo tumevumbua kuwa Muarobaini ni dawa na uzalishaji wake upo Tanzania..tumeshindwa nini kuinvest ktk kutengeneza dawa ya maradhi ambayo ni number one cause of death nchini?..nini sababu ya kuvumbua haswa?.. ndio najiuliza hata sababu ya shule zetu.. hivi tunasoma ili kufanikishe kipi haswa?
Sasa hiii mkuu wangu kama Sivyo Tulivyo ni kitu gani?.. ikiwa elimu ya kuvumbua tunayo, uzalishaji tunao lakini inapifikia kuweka mezani as a finished product stage inayolipa nguvu na jitihada zote zilizotangulia kiuchumi, tunamwachia mzungu au Mchina..

Ndio. Nilikuwa nasisitiza kuwa hilo tatizo unaloliongelea linatokana na ukweli kuwa sisi ni wajamaa hata katika uvumbuzi. Hivyo tunapaswa kuwekeza katika uvumbuzi, usambazaji na ulinzi wa dawa hizo Kijamaa. Tatizo letu tunajaribu kuwa 'mabepari wanigro' katika hilo ilhali hivyo sivyo tulivyo. Alafu hata wale wanaojaribu kuendeleza ujamaa wa dawa hizo tunawabana kwa kutumia hizo sheria za hatimiliki binafsi ya uvumbuzi - ndio yale yale ya kukubali Nyanza iitwe Victoria, lile jiwe pale Mwanza liitwe Bismarck, lile eneo pale Mlima Kilimanjaro liitwe Rebmann n.k utadhani hao ndio waliovumbua hizo rasilimali zetu!
 
Hizi umeshatembelea Castles zilizopo Europe na sehemu zilipojengwa? Na tukirudi Afrika kwanini walijenga milimani kwanza?

Anyway, point niliyotoa hakuwa na tafsiri unayotaka kui-spin hapa. Point yangu ni kuwa Malaria na magonjwa mengine yana kinga nyingi kabla ya kutumia madawa.

Na matumizi ya kinga yanaonyesha ubunifu wako. Na Tanzania inaweza kupunguza idadi ya magonjwa yote kwa kutumia kinga za ubunifu tu bila kutegemea sana madawa. Na huu ubunifu ndio unaotutenganisha sisi na wenzetu.

Acha kutufunga kamba. Hizo castle hata mimi nimeziona. Zilijengwa mlimani kama ng'ombe ya kuwalinda na maadui. Na hazikuwa nyumba za kawaida za watu wa kawaida kuishi. Zilikuwa kama boma la kijeshi/kifalme la ulinzi. Kama unacheza mchezo wa Chess zingatia kete ya Castle inapowekwa.

Alafu haya mambo ya kuchukulia kuwa Waafrika wamekuwa wanakaa mabondeni miaka yote sio ya kihistoria. Zingatia kwa mfano Wapare walipojenga nyumba zao. Huku kujenga mabondeni ni matokeo tu ya kujiingiza katika kujenga miji mikubwa ya kibepari isiyo na nafasi na miundombinu ya kututosha badala ya kuishi kama vile tulivyo - kwenye vijiji vya Ujamaa!
 
JmUshi!,
Mkuu hiyo graph inaonyesha wagonjwa wa maradhi hayo kati ya miaka hiyo na sii tiba zilizokuwepo ktk hospital zao. Hawakusema ni watu wangapi walikufa na maradhi hayo au ni wakati gani waliweza ku control kabisa....
Nimesema hapo juu kwamba mshikaji wangu hakupewa dawa hadi mtaalam wa magonjwa ya tropic lakini madaktari wengine walishindwa kuelewa anaumwa maradhi gani.. hiyo Marekani unayozungumza na wala sii case moja tu nazifahamu nyingine ambazo zilitokea pia...kwa hiyo unaposoma maandishi kisha unataka tubishane wakati mimi nimeona hali halisi tutakesha!.

Mkuu kuna vitengo kibao vya maradhi ya tropical lakini hadi leo hii tunavyozungumza kuna maradhi wanajeshi waliokwenda Iraq bado hayajapatiwa tiba kwa sababu ni mageni kwao, Vitengo vipo na wanajaribu kwa kila hali kuponya wagonjwa hao lakini huwezi ku walk in ktk hospital yoyote ukatibiwa wapo specialist wa maradhi hayo..Swine Flue pekee imeshaua watu kibao na haikuwa kila hospital au daktari anajua tiba yake...

Zakumi,
Mkuu nimekuelewa unaposema wazungu walijenga nyumba zao milimani hapa Afrika na kusema kweli sababu yako inaleta maana kwani ndicho nilichokuwa nazungumzia tofauti baina yetu na mazungu..
wao ktk mazingira yetu walifanya kile kinachotakiwa pamoja na kwamba kwao wanaweza kujenga karibu na maziwa, mito au bahari kutokana na infrastucture iliyokwisha jengwa kulingana na mazingira yao. Kama alivyosema Companero ujenzi kwao huko milimani ulihusiana zaidi na ulinzi, uwezo wa kumwona adui toka mbali kabla hajakaribia mji hivyo wawe wepesi kutuma majeshi yao chini ambako wananchi wanaishi..lakini huko chini infrastructure ilikuwawepo kuweza ku deal na magonjwa yao labda itokee maradhi ya kigeni kama ilivyoingia ugonjwa wa Panya (rabies)..

Hapa Afrika walijua sii kwao hawawezi kujenga infrastructure ya kudumu isipokuwa ile yenye manufaa kwao kibiashara... lakini sisi wenyeji kujenga mlimani ni adha kubwa kwaza tunafikiria ule mwendo wa kupanda mlima... Kisha basi hata kama tunajenga karibu na mito, maziwa na bahari tunashindwa kutanguliza kujenga infrastructure inayokabiliana na matatizo yatokanayo..

Companero,
Tatizo letu tunajaribu kuwa 'mabepari wanigro' katika hilo ilhali hivyo sivyo tulivyo. Alafu hata wale wanaojaribu kuendeleza ujamaa wa dawa hizo tunawabana kwa kutumia hizo sheria za hatimiliki binafsi ya uvumbuzi - ndio yale yale ya kukubali Nyanza iitwe Victoria, lile jiwe pale Mwanza liitwe Bismarck, lile eneo pale Mlima Kilimanjaro liitwe Rebmann n.k utadhani hao ndio waliovumbua hizo rasilimali zetu!
Mkuu maneno yako hapo juu ni tafsiri safi ya NDIVYO TULIVYO pamoja na kwamba unajaribu kuibadilisha.. kwani ni kina nani waliokubali Lake Nyaza iitwe Victoria!..na kama hatukubali tunashindwa kipi kubadilisha jina leo hii miaka 48 ndani ya Uhuru..
Tukubali tusikubali sisi tuna matatizo, ikiwa kweli mwarabu mmoja na gobole la kushindilia risasi mbili anaweza kukusanya watumwa elfu akawatembeza kwa miguu toka Kongo hadi Bagamoyo
na kuwaingiza utumwani akiwatumia house nigger kina Tippu Tippu (wanyapala) kuna tofauti gani na mfumo huu wa leo..Tumebadilika kitu gani zaidi ya rangi ya watawala!
Tena bila aibu hao walikwenda Utumwani huko Marekani na visiwa vya carribean wanakataa kabisa asili yao, hakuna mzungu wala mtu yeyote anayefumba midomo yao kui recognise Afrika, kisha basi hata sisi Waafrika hatuwataki warudi hata kwa mbinde watakuja chukua ardhi zetu!..Israel na udogo wake kila siku wanalilia watu wake warudi..Kongo, Rwanda, Burundi na nchi kibao kila siku vita ya makabila kugombania ardhi ambayo urithi wake ni wazi kabisa...
 
Acha kutufunga kamba. Hizo castle hata mimi nimeziona. Zilijengwa mlimani kama ng'ombe ya kuwalinda na maadui. Na hazikuwa nyumba za kawaida za watu wa kawaida kuishi. Zilikuwa kama boma la kijeshi/kifalme la ulinzi. Kama unacheza mchezo wa Chess zingatia kete ya Castle inapowekwa.

Alafu haya mambo ya kuchukulia kuwa Waafrika wamekuwa wanakaa mabondeni miaka yote sio ya kihistoria. Zingatia kwa mfano Wapare walipojenga nyumba zao. Huku kujenga mabondeni ni matokeo tu ya kujiingiza katika kujenga miji mikubwa ya kibepari isiyo na nafasi na miundombinu ya kututosha badala ya kuishi kama vile tulivyo - kwenye vijiji vya Ujamaa!

Unasema ukitaka kuwaficha waAfrika andika maarifa vitabu. Nimetumia vitabu kuonyesha unasema nafunga kamba.

Ulinzi ulikuwa ni sababu moja na sababu nyingine ni magonjwa. Sehemu yoyote yenye maji yasiotiririka na yanayotoa harufu ni hatari kwa magonjwa.

Wapare ni kabila moja kati makabila 121 ya Tanzania. Hivyo wao kuishi milimani ni coincident na sio design. Na ndio maana wanyakyusa kwao Mbeya wanaishi kwenye mazingira mazuri ya milimani yasio na magonjwa, lakini wakifika DSM wanasahau na kujazana Keko Mwanga.
 
Zakumi,
Mkuu sio kweli, miji mingi Ulaya ipo kando ya mito au bahari tena basi ukitaka kupata uhakika zaidi tazama old Town zote za miji yao utaona zipo karibu zaidi na bahari au mito kwa sababu wao wanatazama urahisi wa kusafirisha mali zao.. Ila ukienda mashambani ndiko unakuta miji ipo juu na mashamba yako chini kwa sababu ya upatikanaji wa maji na ardhi yenye rutuba.. Hii yote inatuonyesha kwamba biashara na uzalishaji hutangulia sehemu za makazi yao..
Sisi tunajenga miji yetu bila malengo, Dodoma ile pale hadi leo tumeshindwa kuhamia.. Hatuna sababu ya kuhamia wala sababu ya kutohamia..Bandari yetu imefinywa kichizi yaani haina mpango lakini hatufikirii kuipanua nje ya pale..
 
Back
Top Bottom